Header Ads Widget

Majambazi wawili wauawa Tanga

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paul
Tanga. Wakazi wa Tanga wamelisaidia Jeshi la
Polisi kuwakimbiza na kuwaua majambazi wawili
kati ya wanne waliokuwa wakitumia gari aina ya
Toyota Probox baada ya kukurupushwa katika
jaribio la kuiba vitu katika magari yaliyoegeshwa
ofisi za halmashauri.
Baada ya majambazi hayo kukurupushwa, vijana
wakiwa kwenye pikipiki na magari waliunga
msafara wa polisi ili kuwakamata hali iliyozua
taharuki.
Taharuki hiyo ilianza jana saa 2.00 asubuhi wakati
majambazi hayo walipovunja kioo cha gari la
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Maweni,
Dominica Tarimo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Leonard
Paul amesema majambazi wawili kati ya wanne
waliuawa kwa kupigwa risasi walipotaka
kuwashambulia askari kwa silaha zenye ncha kali,
huku wengine wawili wakiwa na silaha
walitokomea kwenye msitu ulio jirani na Kiwanda
cha Saruji cha Sungura.

Post a Comment

0 Comments