Mwenyekiti wa Mtaa wa Sangabuye, kata ya
Igombe wilayani Ilemela mkoani Mwanza
anayejulikana kwa jina la John Mayala anashikiliwa
na polisi kwa kosa la kumtorosha na kumpa
ujauzito mwanafunzi.
Mwanafunzi huyo amefahamika kwa jina la Lucy
Daudi, anayesoma kidato cha pili katika Shule ya
Sekondari Sangabuye ambaye anakadiriwa kuwa na
umri wa kati ya miaka 14 hadi 17.
Aidha jeshi la polisi pia linamshikilia mama mzazi
wa mwanafunzi huyo aitwaye Agnes Kadilana
mwenye umri wa miaka 48 mkulima, mkazi wa
Sangabuye kwa kosa la kushindwa kutoa
ushirikiano kwa polisi pindi alipohojiwa kuhusiana
na tukio hilo.
Inadaiwa kuwa mama huyo alishiriki katika
kumtorosha binti yake kwenda kuishi kinyumba na
mtuhumiwa baada ya kupewa fedha.
Mama huyo amedai kuwa binti yake aliamua
mwenyewe kuacha shule kwa madai kuwa shule
imemshinda. "Yeye mwenyewe alisema hawezi
kusoma, akasema ajifunze cherehani, sasa sijui"
Amesema mama huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed
Msangi ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo
hususani wanaume wenye tabia ya kuwa na
mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi pamoja na
wasichana wenye umri chini ya miaka 18 kuacha
mara moja kwani ni kinyume cha sheria bila kujali
kama palikuwa na makubaliano au la.
0 Comments
on