JESHI la Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro, linamshikilia
mtu mmoja kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake
mwenye umri wa miaka 12.
.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod
Mutafungwa, aliwaambia waandishi wa habari jana
kwamba aliyebakwa ni mwanafunzi wa darasa la
tano na ana umri wa miaka 12.
Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, mtuhumiwa
huyo ambaye ni mlinzi, Philipo Stephano ,
alikamatwa Agosti 2 mwaka huu, saa tisa mchana
katika maeneo ya Soweto, Kata ya Soweto,
Manispaa ya Moshi mkoani hapa.
“Yule mtoto ambaye jina lake tunalihifadhi,
alibakwa na babu yake mzaa mama yake, mkazi
wa Soweto.
“Kabla ya mtuhumiwa kufanya tendo hilo,
alimwambia mjukuu wake huyo amwelekeze na
alipokubali, alimpeleka katika eneo analolinda na
kumfanyia unyama huo.
“Baada ya uchunguzi wa daktari, ilithibitika
mwanafunzi huyo alibakwa na kusababishiwa
maumivu makali katika sehemu zake za siri.
“Kwa hiyo, mtuhumiwa tumemkamata na
tunaendelea na upelelezi kabla hatujampeleka
katika vyombo vya sheria,” alisema Kamanda
Mutafungwa.
0 Comments
on