Header Ads Widget

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania asimamishwa kazi kwa uzembe

Waziri wa Ujenzi Prof. Makame Mbarawa
amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Ndege ATCL Kapten Johnson Mfinanga
na Mkurugenzi wa Uendeshaji Kapten Sadick Muze
kwa kosa la kumchagua rubani asiye na sifa
kwenda kupata mafunzo Canada.

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Mbarawa
amesema marubani watano walichaguliwa kwenda
nchini Canada kwa ajili ya kupata mafunzo ya
kurusha ndege mpya zitakazoingia nchini mwezi
Septemba kama alivyoahidi Rais Dkt. John
Magufuli.

Waziri ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa
malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya
za shirika la ATCL alitoa maelekezo kwa Kaimu
Mkurugenzi huyo kuchagua marubani watano
wenye sifa kwa ajili ya kwenda kupata mafunzo
nchini Canada ambapo kati ya watano
waliochaguliwa mmoja amebainika hana vigezo
hivyo ameamua kuwasimamisha viongozi hao
kutokana na uzembe.

Aidha waziri Mbarawa amewataka watendaji wa
serikali kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria
na kanuni za kazi na mtumishi atakayefanya
kinyume hatasalimika kuwajibishwa.

Post a Comment

0 Comments