Header Ads Widget

TV1 kuonyesha Ligi Kuu ya England

Dar es Salaam. Mashabiki wa soka nchini
wamepata ahueni ya kutazama Ligi Kuu ya England
kupitia kituo cha runinga cha TV1.
Meneja Mkuu wa TV1, Joseph Sayi amesema kituo
chao kimepata ruhusa kutoka kampuni ya Econet
Media yenye haki za kuonyesha ligi hiyo kusini
mwa Jangwa la Sahara.
“Kama inavyofahamika kuwa Ligi Kuu England
inatazamwa na watu zaidi ya milioni 260 duniani,
hivyo tumeona tuwafikishie uhondo huu mashabiki
wa soka nchini kwa urahisi,” amesema Sayi.
Meneja Masoko wa TV1, Gillian Lugumamu
amesema kituo hicho kitaonyesha mechi moja kila
Jumamosi, huku Ijumaa na Jumatano zikitengwa
kwa ajili ya uchambuzi wa mechi za ligi hiyo.

Post a Comment

0 Comments