Header Ads Widget

Trump asema kampeni yake ni imara

Donald Trump amekuwa akishutumiwa kwa kauli
zake
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini
Marekani Donald Trump amesisitiza kwamba
hakuna mgawanyiko kwenye kambi yake ya
kampeni, licha ya taarifa kudokeza kwamba kuna
mzozo mkubwa katika chama hicho.
Akihutubu katika mkutano wa hadhara Florida, Bw
Trump amesema kampeni yake "inafanya vyema
sana".
Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuwepo
kwa mvutano baada ya Trump kurejea matamshi
yake ya kushambulia wazazi wa Mwanajeshi
aliyeuawa nchini Iraq.
"Ningetaka kuwafahamisha tu kwamba kampeni
inaendelea vyema sana," amewaambia watu
waliohudhuria mkutano wake eneo la Daytona
Beach.
Awali, msaidizi mkuu wake Donald Trump Paul
Manaford alikuwa pia amekana taarifa kuwa kuna
mgawanyiko mkubwa kwenye kampeni baada ya
kile kinachodaiwa mfululizo wa kauli za mgombea
huyo wa chama cha Republican, zenye kukwaza.
''Kampeni ziko vizuri, tumejipanga, tunasonga
mbele,'' aliiambia kituo cha runinga cha Fox News.
Baadhi ya Maafisa wa Kampeni za Trump
wamesema ''wanahisi kuwa wanapoteza muda
wao''.
Hata hivyo, Manafort amemlaumu mpinzani wa
Trump wa Chama cha Democratic, Hillary Clinton
kwa ripoti hizo
Bw Manafort amesema watu wengi bado wana
imani na Bw Trump
''Hii ni kauli nyingine ya Clinton ambayo imebebwa
na vyombo vya habari, amesema ''Bwana Trump
amejitokeza wiki hii kwenye mikusanyiko mikubwa
sana ya watu walifurika mpaka mtaani''.
Siku ya Jumatano Bw Trump mwenyewe pia
aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa
''kuna umoja kwenye Kampeni yangu, pengine
mkubwa zaidi kuliko siku zote''.
Vita vyake vya maneno na Khizr na Ghazala Khan,
wazazi wa Kapteni Humayun Khan aliyeuawa nchini
Iraq, vimesababisha watu kutofautiana ndani ya
Chama cha Republican.

Post a Comment

0 Comments