Header Ads Widget

Olimpiki Rio 2016: Kina dada wa Zimbabwe wacharazwa 6-1

Sweden walilaza Afrika Kusini kupitia bao la Nilla
Fischer kipindi cha pili
Timu ya taifa ya kina dada ya Zimbabwe
imecharazwa 6-1 na timu ya taifa ya Ujerumani
kwenye mechi zilizochezwa siku ya kwanza ya
michezo ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro, Brazil.
Ujerumani, waliokuwa mabingwa 2000, 2004 na
2008, walikuwa na kibarua rahisi dhidi ya timu hiyo
ya Afrika. Wakati mmoja, mabao yalikuwa 2-1
lakini mabinti hao wa Zimbabwe walionekana
kulemewa na uchovu dakika za mwisho mwisho na
wakabebeshwa magoli matatu katika kipindi cha
dakika 16.
Wachezaji wa Sweden baada ya kuifunga Afrika
Kusini
Michezo ilianza kwa mechi kati ya Sweden na
Afrika Kusini ambapo Sweden walishinda 1-0.
Baadaye, wenyeji Brazil walilaza Uchina 3-0.
Uwanja wa Olimpiki, wenye uwezo wa kupokea
mashabiki 60,000, ulikuwa hauna mashabiki wengi
mechi ya kwanza, lakini zaidi walifika kabla ya
mechi hiyo ya Brazil.
Janine Beckie wa Canada naye alifunga bao
sekunde 20 pekee baada ya mechi yao dhidi ya
Australia kuanza, na kuweka rekodi ya bao la kasi
zaidi lililofungwa katika historia ya soka ya
wanawake Olimpiki.
Marekani wanapigiwa upatu ksuhinda michuano
hiyo.

Post a Comment

0 Comments