KUFUATIA kuwepo madai kuwa msanii wa Bongo
Fleva, Nuh Mziwanda kutishiwa kupewa kichapo na
mijemba inayodaiwa ilitumwa na aliyekuwa mpenzi
wake Shilole, hatimaye Nuh aamua kukodi
bodigadi wa kumlinda.
Nuh alionekana akiwa na bodigadi huyo kwenye
Tamasha la Mwendokasi lililofanyika Viwanja vya
Posta jijini Dar hivi karibuni jambo lililozua
minong’ono kwa baadhi ya mashabiki wake.
Katika tamasha hilo burudani kutoka kwa wasanii
mbalimbali wakiwemo Barnaba, Isha Mashauzi,
Juma Nature, Rich One, Man Fongo, G. Nako, Lord
Eyes, Navy Kenzo, Snura, Nay wa Mitego
ziliwapagawisha mashabiki.