Header Ads Widget

Mlinzi awafungia walimu ofisini

MLINZI wa Shule ya Msingi Medeli iliyopo katika
Manispaa ya Dodoma, Zebedayo Bendera,
amewafungia ofisini baadhi ya walimu wa shule
hiyo baada ya kushindwa kumlipa mshahara wake.
Wakati Bendera anafunga ofisi hiyo jana asubuhi,
ofisini walikuwamo walimu kadhaa pamoja na
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Rehema William.
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika
shuleni hapo jana, mlinzi huyo alisema aliamua
kuchuku uamuzi huo baada ya walimu hao
kushindwa kumlipa mshahara kuanzia Januari
mwaka huu.
“Mshahara wangu ni shilingi 70,000 kwa mwezi na
kwa kuwa sijalipwa kwa miezi saba, nawadai
shilingi 490,000.
“Kwa hiyo, nimeamua kuwafungia ndani ili
kuwashinikiza wanilipe fedha zangu kwa sababu
hawataki kunilipa kwa makusudi kwani fedha
wanazo.
“Kitendo cha hawa walimu kutonilipa mshahara
kimeathiri maisha yangu na familia yangu kwa
sababu sina kazi nyingine ya kufanya zaidi ya huu
ulinzi.
“Kwa hiyo, nitaendelea kuwafungia ofisini hadi
nitakapolipwa mshahara wangu maana hii siyo
mara ya kwanza kuwafanyia hivi.
“Hata mwezi uliopita mimi na mlinzi mwenzangu
tuliwafanyia hivi, wakaita polisi wakaja kutukamata
na mwishowe wakatulipa 50,000 na kuachiwa,”
alisema Bendera.
Akizungumzia tukio hilo, Mwalimu Mkuu Rehema
alisema hiyo ni mara ya nne mlinzi huyo
kuwafungia ofisini.
“Ni kweli huyo mlinzi anatudai kwani hesabu
zinaonesha yeye na mwenzake wanatudai zaidi ya
shilingi laki tatu kila mmoja.
“Siyo kwamba hatutaki kuwalipa bali tunashindwa
kufanya hivyo kwa sababu Serikali haileti fungu la
walinzi kwenye fedha zinazopelekwa mashuleni,”
alilaalmika Mwalimu Rehema.

Post a Comment

0 Comments