Header Ads Widget

Marufuku ‘Ukuta’ Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla
Mbeya. Mikutano ya Operesheni Ukuta
iliyotangazwa kuratibiwa na Chadema kuanzia
Septemba Mosi, imepigwa marufuku na Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
Akizungumza katika kikao cha kazi
kilichoshirikisha kamati ya ulinzi na usalama mkoa,
wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa
halmashauri, Makalla ametangaza kupiga marufuku
mkutano wowote utakaofanyika chini ya utaratibu
unaoitwa Operesheni Ukuta.
“Bila shaka wananchi Mbeya wanataka amani na
kazi, hivyo ni marufuku kufanyika mkutano wowote
wa kisiasa unaoandaliwa kwa kushirikiana na watu
wengine kutoka nje ya mkoa,” amesema Makalla
aliyewahi kuwa mbunge na mweka hazina wa
CCM.

Post a Comment

0 Comments