Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji
Peter Msigwa
Iringa. Baada ya kupata kibali cha polisi, Mbunge
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amefanya
mkutano wa hadhara akisema hakuna wa
kumpangia cha kuzungumza kwenye mikutano
yake.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa
kwanza wa kibunge tangu alipochaguliwa
uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembetogwa
mjini hapa jana, amesema hakuna wa kumpangia
hoja za kuzungumza kwenye mikutano yake.
Juzi, mbunge huyo alipewa barua na Jeshi la
Polisi iliyoeleza kuwa imempa kibali cha kufanya
mikutano hiyo, lakini ikimuwekea masharti
mbalimbali likiwamo la kutozungumzia viongozi
wengine na badala yake ajikite kwenye shughuli za
maendeleo na kuchukua maoni ya wananchi
anaowawakilisha.
0 Comments
on