Header Ads Widget

Neymar kwenda jela miaka miwili

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Neymar, anatakiwa kupata kifungo cha miaka miwili hii ni baada ya waendesha mashtaka wa nchini Uhispania kudai kuhusika kwake katika kesi ya ufisadi kuhusu uhamisho wake kutoka klabu ya Santos nchini Brazil mwaka 2013
.
Jaji Jose Perals pia ametaka aliyekuwa rais wa Barcelona sandro Rosell kwenda jela kwa miaka mitano mbali na kupigwa faini ya Yuro milioni 7.2 kwa klabu hiyo.
Imetaka kutupiliwa mbali kwa mashtaka dhidi ya rais wa sasa wa klabu hiyo Josep Maria bartomeu.
Rosell,Neymar na babake wanatarajwa kushtakiwa.
Kesi hiyo inatokana na malalamishi ya kundi la uwekezaji la Brazil DIS ,ambalo linamiliki asilimia 40 ya haki za uhamisho wa Neymar na linadai lilipata fedha chache ikilinganishwa na zile lililotarajia.

  1. Aliyekuwa rais wa Barcelona, Rosell alijiuzulu kama rais wa klabu hiyo mwaka 2014 kwa jukumu lake katika uhamisho huo na kutoa ushahidi mahakamani mnamo mwezi Februari pamoja na Bartomeu,Neymar na babake Neymar.

Post a Comment

0 Comments