JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa wanaendelea na
upelelezi kufuatia kuuawa kwa mwanamasumbwi Thomas Mashali na watatoa
taarifa ya kifo hicho siku ya Jumatano.
Akizungumza
na waandshi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro alisema taarifa
zilizopo kufuatia kifo cha bondia huyo ni za kufikirika na zinasemwa tu,
hivyo Jumatano atatoa taarifa hiyo.
Kamishina
Sirro alisema kuwa bondia huyo ni mtu mkubwa na hakuna mtu
aliethibitisha kuwa ni mny'ang'anyi, hivyo mpaka sasa ni maneno ya
mtaani tu.
“Mimi
ndio napata taarifa juu ya kifo cha bondia huyo. Ngoja nisubiri taarifa
niweze kutoa siku ya Jumatano, ambapo nitakuwa na majibu sahihi. Kwa
leo niache tu”alisema Kamishna Sirro.
0 Comments
on