Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuber jana amekabidhiwa ripoti ya awali iliyoandaliwa na tume ambayo ameiunda kwa ajili ya kufanya uchunguzi na kuzibainisha mali zote za Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).
Akizungumza wakati wa kumkabidhi ripoti hiyo, Mwenyekiti wa tume hiyo Sheikh Abubakari Khalid Hajj alisema kuwa ripoti hiyo imefanyika kwa muda wa miezi mitatu licha ya kukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa muda.
Aidha aliwambia wanahabari kuwa uchunguzi huo umehusisha ufuatiliaji wa mali za Bakwata katika Mkoa wa Dar es salaam pekee,ikiwemo majengo,viwanja, pamoja na kupitia mikataba mbalimbali ili kujiridhisha kama imefuata taratibu za kisheria.
Akizungumza mbele ya wanahabari mara baadi ya kupokea ripoti hiyo Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuber alisema kuwa ataipitia ripoti hiyo ili kujua yale yaliyobainishwa na tume yake, na kuahidi kuyafanyia kazi mapema iwezekanavyo.
Hata hivyo Mufti huyo ameiongezea muda wa miezi mitatu tume hiyo ambayo ina jumla ya wajumbe wanane kwa ajili ya kukamilisha kuandaa ripoti ya mkoa wa Dar es salaam kabla ya kuhamia mikoa mingine kwani zoezi hilo litafanyika nchi nzima.
0 Comments
on