SERIKALI imesema itaendelea kuijengea uwezo Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya , ili iweze kutoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa ikiwemo vipimo vya CT-SCAN na MRI na kuondoa adha kwa wananchi ya kwenda jijini Dar es salaam kufuata huduma hizo.
Naibu Waziri wa Afya Dk Hamis Kigwangala amesema haya wakati akizindua bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya , iliyoteuliwa na Wizara ya Afya, akisema Wizara itahakikisha huduma za saratani zinatolewa kwenye hospitali hiyo, ili kuwaondolea wagonjwa usumbufu wa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es saalam.
Mwenyekiti wa Bodi DK Amos Kwendea Mwakilasa akaishikuru Wizara ya Afya kwa kuwateuwa na kuwataka wananchi watarajie mabadiliko, lakini pia akiamini kuwa hospitali hiyo kwa sasa itatoa huduma zenye ubora kwa wagongwa.
Hata hivyo Naibu waziri ameshauri bodi hiyo kupanua hopitali kwa kuongeza ardhi na kuwa na vitengo vingi kama ilivyo kitengo cha wazazi meta, na kupima maeneo yao ili yazivamiwe, hii itasaidia vizazi vijavyo kutopata usumbufu kwa kuwa eneo la hospitali hiyo limeanza kuelemewa.

0 Comments
on