Katika ulimwengu wa sasa mapichapicha huwa ndio stori ya mjini, watu wengi hupenda kupata picha nyingi za aina tofauti, picha hizo zaweza kuwa zinaelezea kitu fulani au ikawa katika kujitunzia tu kumbukumbu. Si kila upataji/upigaji wa kila picha unafaida bali changamoto pia zimo hasa katika picha maarufu za SELFIE #selfie, hizi zaweza kugharimu maisha yako ghafla bila kutarajia.
Jeshi la polisi la Urusi limeangaza hasa katika madhara ya upigaji wa picha hizo za selfie na kutoa bango linalotoa katazo kwa baadhi ya mazingira hatarishi kwa upigaji wa selfie zitakazo gharimu uhai wa mwananchi.
Katika video hapo juu, ni miongoni mwa udhibiti wa kijana alipigwa na treni huku akijipiga selfie.
0 Comments
on