Hivi sasa mnamo tarehe ya jana 15/11/2016 simu nyingi zilipata updates mpya inayokuwezesha kupiga simu ya video kupitia WhatsApp.
whatsapp-video-calls
Mmiliki wa mtandao huo Bw. Mark Zucherberg kupitia ukurasa wake wa facebook aliandika kuwa “…sasa tunawaletea video call kupitia whatsapp, ikiwa simu ya sauti ya kawaida ilikuwa kwa haraka zaidi na ombi kubwa la watumiaji ilikuwa ni video call, hata hivyo itafanya kazihata kwenye mazingira magumu ya mtandao…”
Unachotakiwa kufanya ni kufanya update ya application yako ufurahie uhondo mpya. Tupe mtazamo wako hapa chini juu ya mabadiliko haya.