Huwenda una simu ya android lakini inakukhera kwa kuwa ina speed ndogo sana. pole kwa hilo. lakini zipo njia za kuweza kufanya ili kuongeza ufanisi wa simu yako na ikaweza kufanya kazi kwa speed.
ungana nami hapa ili kujua ni kipi ufanye ili kuongeza speed ya simu yako ya Android.
NJIA YA KWANZA
KU uninstall/kudisable app zote ambazo hazina umuhimu.
ndio simu nyingi za android huwa zinakuja na app ambazo hazina umuhimu kwa mtumiaji. kwa mfano kuja na games ambazo ni demo, extra keyboard, app za amazon market n. k hivyo ni vyema kuziondoa kwani mara nyingi app hizi huwa zina fanya kazi chini kwa chini. kama haziwezi kuondoka basi ziwekee option ya disable ili kuzizuia kufanya kazi chini kwa chini na pia zisiji update.
NJIA YA PILI
Futa cache data
Sina maelezo mazuri kuhusiana na cache data lakini haya ni mabaki ya data zinazohifadhiwa kwenye memory ya simu. ili kufuta hizi cache data nenda kenye PLAY STOTE kisha download android cleaner apps ambazo zina saidia kufuta hizo cache
NJIA YA TATU
SAFICHA INTERNAL MEMORY YA SIMU YAKO
Ili kusafisha internal memory ya simu yako nenda kwenye simu yako upande wa setting kisha storage alafu chagua internal storage. bonyeza bar yenye rangi kisha clear memory
\
NJIA YA NNE
Ondoa au punguza widget kwenye home screen ya simu yako
Widget ni nzuri sana kwenye simu kwani husaidia kuweka mwonekano mzuri wa simu na pia kuokoa muda pale unapotaka kufungua application yoyote ile. lakini kwa upande wa pili hizi widget husababisha simu kuwa slow kwani zipo ambazo huwa zinafanya kazi chini kwa chini muda wite. mfano widget za hali ya hewa na photo slider. hivyo ni vyema kutumia widget chache na zenye umuhimu sana kwenye simu yako
NJIA YA TANO
Kuondoa live wall paper kwenye simu yako
Live wallpaper sio nzuri kutumia kwenye simu kwani huwa zinafanya kazi muda wote na hivyo kusababisha cache nyingi kwenye simu yako na mwisho simu kupunguza ufanisi wake wa kiutendaji. mfano wall paper zinazo onesha water flow, fish swimming, n.k
hivyo tumia wallpaper za kawaida badala ya hizo za live
NJIA YA SITA
Jenga mazoea ya kuwa una update simu yako mara kwa mara
Unashauriwa kuwa angalau mara mbili kwa wiki uwe una uodate software ya simu yako na application zake. hii itakusaidia kupata feature mpya ambazo zinakuwa zikitolewa kupitia matoleo mapya ya hizo software/program.
fungua hapa kujua jinsi ya ku update simu yako
NJIA YA SABA
Restore/reset simu yako
Wakati mwingine kama ikitoka simu yako ikawa slow basi chukua uamuzi wa kuilistore/reset katika facory. hii husaidia kuirudisha simu yako kuwa katika hali yake ya mwanzo. ili kufanya hivi
NENDA: SETTING ---BACKUP AND RESET .
ila njia hii ni ya muda mfupi kwa tatizo lazima lirudi tena kadri utakapo kuwa ukitumia simu
NJIA YA NANE
Ondoa Animation zote
animation nazo huchangia simu kuwa slow. hivyo ili kuongeza speed ya simu yako ni vyema ukaondoa windows animation kwenye simu yako.
kuondoa hizi nenda kwenye simu yako upande wa setting kisha developer options( kama developer haipo on iweke on ) kisha tafuta maneno haya
window animation scale. hapa weka off au 0.5x
translation animation scale: pia nako weka off au 0.5x
animator duration scale : pia weka off au 0.5x
kama developer haipo kwenye simu yako neda kwenye About phone kisha tafuta BUILD NUMBER ibonyeze mara tatu hadi sita na hapo itakuletea option ya developer. kisha rudi nyuma na ingia kwenye developer ufanye kama hapo juu.
hii ni kwa sababu simu nyingi option ya developer huwa inafichwa.
0 Comments
on