Muda mfupi baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro kuwaambia waandishi wa habari kuwa hawezi kusema ni lini mwanamuziki Roma na wenzake watapatikana, taarifa kutoka kwa mmiliki wa studio walipokamatiwa, amethibitisha kuwa wamepatikana.
J Murder ambaye ndiye mmiliki wa Tongwe Records walipokuwa Roma na wenzake kabla ya kukamatwa na watu wasiojulikana, amesema kuwa wasanii hao wamepatikana na wapo katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Aidha,Mkuu wa polisi (OCD) wilaya ya Kinondoni, Abubakar Kunga amethibitisha kupatikana kwa wasanii hao, lakini kwa sasa amesema wanafanya nao mahojiano ya kipolisi katika kituo cha Oysterbay.
Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru.
Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.
“Mimi ni Kamishna wa Polisi siwezi kusema wasanii watapatikana lini, kama kuna kiongozi alitaja siku watakayopatikana, muulizeni yeye.
“Upelelezi ndio utakao amua hawa watu watapatikana lini. Tunafanya kazi kufuata taaluma ni si kutoa maneno tu." Alisema kamanda Sirro mapema Asubuhi wakati akiongea na waandishi wa habari
“Upelelezi ndio utakao amua hawa watu watapatikana lini. Tunafanya kazi kufuata taaluma ni si kutoa maneno tu." Alisema kamanda Sirro mapema Asubuhi wakati akiongea na waandishi wa habari
0 Comments
on