ama wewe unatumia sim ya ANDROID basi hili si geni kwako, kusahau password za simu zetu (za maneno,namba au pattern) si jambo geni. Kama tatizo hili halijakukuta basi limeshawahi kumkuta rafiki ama jirani yako. Lakini wengi wetu tunapo pata tatizo hili huwa tuna hisi simu imesha haribika na huwa tunapenda kupeleka kwa fundi ili kuiflash. Niwaibie siri mafund huwa wanakula tu pesa zenu kwani hawaflash bali kuna kitu huwa wanafanya.
Unataka kujua ni nini wanafanya? Basi ungana nami hapa ili kukujuza ni nini kinafanyika ili kutoa hizo password kwenye simu yako ya android
ANGALIZO:
Kabla hujaanza kufaya hizi hatua nitakazo kuelekeza hakikisha
a. Simu yako ina chaji angalau asilimia 50 (50%)
b. Umetoa memory card na laini yako kwenye simu
Sasa fata hatua hizi zifuatazo ili kutoa password kwenye simu yako
HATUA YA 1
Zima simu yako kwa kubonyeza POWER OFF kama kawaida, kama hazimi kwa njia hiyo basi toa betri ya simu kasha irudishe tena kwenye simu
HATUA YA 2
Katika simu yako bonyeza batani zifuatazo.
a. Volume up + home +power
b. Volume down +power
c. Volume up + power
d. Volume down +home +power
e. Home +power
Option hizo zitakuwezesha kuiweka simu yako kwenye recovery mode. Jaribu kila hatua hapo juu hadi kupata itakayoiweka simu yako kwenye recovery mode. Tumeweka hivyo kwasababu simu zinatofautiana kuingia kwenye recovery mode
Endapo hatua hizo hazitokubali kwenye simu yako basi ingia google kasha andika
“how to hard reset ......” ikifuatiwa na aina ya simu yako mfano how to hard reset huawei 5C
Na google watakuletea link chaguzi zitakazo kuonesha jinsi yak u hardreset simu yako
Ikishafunguka menu ya recovery mode nenda ukachague palipo andikwa “wipedata/factory reset”
Tumia batani za sauti kupandishia juu na kushushia chini, kwa hapa tumia batani ya sauti ya chini kushusha hadi hapo palipo na hilo neon kasha bonyeza batani ya power ili kuchagua
HATUA YA4
Baada ya kuchagua wipe data/factory reset utaletewa menyu nyingine itakayo kutaka ukubali. Kama hapo juu tumia batani za sauti kupandishia ama kushushia hadi kwenye chaguzi. Lakini pia hapa tumia batani ya kushushia sauti kushusha hadi palipo andikwa “ yes – delete all user”
Kasha bonyeza batani ya power ili kuchagua
Baada ya hapo iache simu imalize kufanya kila kitu. Ikimaliza ita restart na kuwaka yenyewe. Hapo utakuwa umeshaweza kutoa password kwenye simu yako ya Android, sasa utaweza kuitumia simu yako.
Angalizo
a. Hatua hii itafuta kila kitu kwenye simu yako mfano contacts,picha,video n.k kama ulivisave kwenye simu pamoja an account zako zote,
b. Unashauriwa kufanya backup, kutoa memory card na sim card kwenye simu yako kabla ya kufanya hizi hatua
c. Hakikisha unafata hatua hizi kwa umakini ili kuhakikisha usalama wa kifaa chako. Hatutohusika na uharibifu wa kifaa chako hivyo kuwa makini, kama unaona huwezi kufanya hivi ni bora ukamtafuta mtu mwenye utaalamu ili akusaidie
d. Kwa maelezo na msaada zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0744573800
0 Comments
on