Siku kadhaa zimepita tangu msanii Nay wa Mitego kuachiwa huru, ambapo alikuwa akishikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za wimbo wake wa ‘WAPO’ kudaiwa kutokuwa na maadili.
Msanii Nay wa Mitego aliachiwa huru baada ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe lakine leo April 3 2017 Nay kupitia instagram account yake ameandika maneno yanayoashiria kuwa hayuko katika hali ya usalama.
“Usalama wa Maisha yangu umekuwa Mdogo kwa sasa, Wanapanga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii Dunia. Nipo tayari kwa chochote wanachopanga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni Mwana Muziki si vingine”
“Kwa chochote kitachotokea Familia yangu itakuwa na chakuongea, Siwezi kuhama Nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa na siko tayari kupindisha Chochote.! Nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kuwa na mlinzi. OnlyGod🙏🏿 #Wapo #Truth


Jiunge na djadam64.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter's  na Instagram  ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka djadam64.com