Taasisi ya utafiti ya sera za umma Marekani imetoa matokeo ya utafiti uliofanywa February 2017 kuhusu utendaji kazi wa Rais wa nchi hiyo ambapo  zaidi ya nusu ya Wananchi wameonesha kumkataa Donald Trump huku zaidi ya asilimia 44 wakilitaka Bunge la nchi hiyo kupiga kura za kumuondoa madarakani.
Kwa mujibu wa utafiti huo asilimia 44 ya watu wamejutia kumchagua Donald Trump baada ya kufuta sera ya afya iliyoanzishwa na Rais Obama “Obamacare” bila kuweka sera mpya huku asilimia 44 walisema ni mtu asiye muaminifu na asilimia 64 wakimtaka Rais huyo kuonesha hadharani mlolongo wake wa ulipaji kodi.
Utafiti huo pia umeonesha Donald Trump anashika namba tatu kati ya wanasiasa wanaochukiwa na wananchi kwa sasa huku akiongozwa na Msemaji Mkuu wa Bunge Paul Ryan.