Rais Magufuli leo May 30,2020 Mkoani Dodoma amewakabidhi Marais Wastaafu wa Tanzania kila mmoja Tausi 25 wanaopatikana Ikulu, ili wakawatunze kwenye bustani zao, Mama Maria Nyerere amekabidhiwa pia  Tausi hao kwa niaba ya Baba wa Taifa Mwl. Nyerere.

“Tausi hawa ambao kila Rais Mstaafu nimemkabidhi 25 wataanza kuondoka leo hii tumeshaandaa utaratibu kuwasafirisha kwenda Butiama, Msoga nk, ikitokea mmoja akafia njiani tutareplace (zimetolewa pia kilo 100 za chakula cha Tausi cha kuanzia kwa kila mmoja)”-JPM

“Tanzania hatukuwahi kuwa na Tausi waliltetwa na Baba wa Taifa, Mama Maria anaifahamu zaidi historia yake, Mzee Mwinyi aliwakuta angeweza kuwachinja na kuwala nyama maana nyama yake tamu kuliko kuku ila aliwatunza, Mzee Mkapa na Kikwete pia wakawatunza”-JPM