Jana, ratiba ya hatua ya robo fainali ilipangwa ambapo Simba itakutana na Azam FC ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo walilolitwaa kwa kuitwanga Lipuli FC bao 1-0.
Sven Vandernbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anaamini utakuwa mchezo mgumu kutokana na Azam FC kuwa ni mabingwa watetezi na waliwafunga walipokutana kwenye mechi ya ligi.
"Utakuwa ni mchezo mgumu ukizingatia kwamba Azam FC tuliwafunga kwenye mechi yetu tulipokutana hivyo watajipanga kulipa kisasi.
"Tunajiandaa vizuri ili kuona namna gani tutapata matokeo kwani kila mechi kwetu tunachotazama ni matokeo," amesema.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Juni 27 Uwanja wa Taifa, mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya Yanga ama Kagera Sugar.
0 Comments
on