Ikiwa leo mkali wa Freestyle, Albert Mangwair ametimiza miaka saba tangu alipofariki, sasa miongoni mwa marafiki zake wa karibu aitwae Dark Master Mei 28, 2020 alihojiwa kwenye kipindi cha XXL kinachorushwa Radio Clouds FM na akaulizwa kuhusu Mangwair kama aliacha mtoto.
‘Unajua kuna stori moja iko ndani kidogo enzi hizo  katika maisha yetu ya shule kidato cha kwanza kuna mtoto alizaliwa anaitwa nyemo, tatizo la Cowboy alikuwa ni msiri sana,  sasa unajua ni matatizo tu yalitokea na huyo mtoto alienda Iringa mvumi ambapo hiyo sehemu baba yangu anaishi huko na mpaka sasa nawasiliana nao’- Dark Master
‘Sasa huyo mtoto wa Cowboy ambae ni mtoto wa kike nae kwasasa ana watoto wawili’- Dark Maste