Bibi mmoja aliyejulikana kwa jina la Jennie Stejna mwenye miaka 103, amejipongeza kwa kunywa bia ya baridi iitwayo Bud Light, baada ya kupona ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Mzee huyo anapatikana Massachusetts Jijini Boston, alianza kuumwa ugonjwa huo mwanzoni mwa mwezi Mei,  kwa dalili za kukosa ladha pia na kuumwa na homa kisha kupelekwa hospitali.
Akitoa taarifa hiyo mkwe wa mjukuu wake Adam Gunn amesema, wote walikuwa wanajua tayari wanaelekea kumpoteza bibi yao,  na kuna siku aliwahi kumuuliza kama yupo tayari kwenda mbinguni kisha bibi akamjibu ndiyo.
Bibi huyo kwa sasa ni mjane na mumewe alifariki mwaka 1992 akiwa na miaka 82, amebahatika kupata watoto wawili, wajukuu watatu, vitukuu wanne na vilembwekezi wanne.