http://www.mwanajamii.co.tz/
Huwenda ukawa unatumia simu kwa muda mrefu na ushapoteza au kuibiwa simu kadhaa lakini hukujua ni nini unatakiwa kukifanya. kwanza pole kwa hilo kwani unapo poteza au kuibiwa simu mambo mengi huaribika. mfano kama ulikuwa na deal la pesa basi unaweza kulipoteza pia kupoteza contact za watu wako muhimu pia. any way tuachane na hayo, nataka nikupe kitu cha faida kwako.
 Unajua ni nini unatakiwa kufanya pale unapo poteza au kuibiwa simu yako? basi ungana nami hapa nikuambie ni  nini unatakiwa kufanya pindi tu unapopoteza au kuibiwa simu.

Cha kwanza kabisa unacho takiwa kukifanya pale tu unapo ibiwa simu ni kuazima simu ya mtu aliye karibu yako anaweza kuwa ndugu,rafiki au hata jirani yako uliye nae mda huo, ukishapata simu kutoka kwa huyo uliye karibu nae utatakiwa kupiga simu kwa mtoa huduma wako kwa wateja kulingana na laini ya simu ambayo imepotea au kuibiwa na simu yako ili kutoa taarifa za kuibiwa/kupotea kwa simu yako (hawa ni TIGO,VODACOM,AIRTEL,ZANTEL,HALOTEL,SMART TANZANIA,TTCL)
http://www.mwanajamii.co.tz/

mfano kama simu iliibiwa ikiwa na laini ya tigo basi utatakiwa kupiga huduma kwa wateja ya tigo.
  Hii itafanya mtoa huduma kwa wateja aweze kuifungia haraka laini yako ili isiwe tena hewani, kwani asilimia kubwa ya wanao iba simu hutumia laini ya waliye muibia simu ili kufanya utapeli. 
   katika kutoa taarifa hii kwa mtoa huduma unatakiwa kuwa na taarifa za kutosha kuhusiana na usajiri wako wa laini lakini pia unatakiwa kuwa na taarifa za kutosha kuhusu simu yako. sasa hapa pole kwa wale ambao wamesajiri laini kwa kutumia vitambulisho visivyo vyao kwani ni ngumu kuweza kusaidiwa kwakuwa usajiri sio wako'
kuhusu taarifa za simu ambazo unatakiwa kuwa nazo ni
1.  imei/serial number za simu yako, hizi unaweza kuzipata kwa kupiga *#06# au nyuma ya simu yako baada ya kutoa betri
2. aina ya simu unayotumia/uliyoibiwa au kupotea
3. mda ambao umeipoteza au kuibiwa na mahali ilipo potelea au kuibiwa 

Cha pili unachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa kwa watu wako ili wajue kuwa umepoteza simu. hii itawawezesha wao kutopata shida hasa pale watakapo anza kutumiwa sms zinazo ashiria utapeli. kama nilivyosema awali kuwa wezi wa simu hupenda kutumia namba za waliye muibia kufanyia utapeli

Cha tatu unacho takiwa kufanya ni kwenda kutoa taarifa katika kituo cha polisi kilicho karibu na wewe' unalazimika kutoa taarifa polisi kwa ajiri ya usalama wako kwani simu ambayo umepoteza inaweza ikatumika katika matukio ya uhalifu. hivyo kama ukiwa hujatatoa taarifa i lazima utaonekana wewe ndo muhusika.
 hapa pia unatakiwa kuwa na taarifa zako muhimu zinazo husu simu yako
 http://www.mwanajamii.co.tz/
kuhusu taarifa za simu ambazo unatakiwa kuwa nazo ni
1.  imei/serial number za simu yako, hizi unaweza kuzipata kwa kupiga *#06# au nyuma ya simu yako baada ya kutoa betri
2. aina ya simu unayotumia/uliyoibiwa au kupotea
3. mda ambao umeipoteza au kuibiwa na mahali ilipo potelea au kuibiwa
4. namba yako/zako ambazo simu imepotea nazo

 Cha nne ni kwenda kwenye kituo cha kutolea huduma kwa wateja ili kurudisha (ku renew) namba zako za simu. sasa ili kuweza ku renew namba yako/zako utatakiwa kuwa na taarifa sahii za usajiri wa laini yako. ukisha faikisha kurenew lain yako utaweza kuwa hewani tena na hivyo utalazimika kuwajulisha watu wako kwa kuwapigia kuwa sasa upo hewani.
kumbuka endapo taarifa ulizo toa zitakuwa sahihi basi simu yako itafungwa na hakuna atakaye weza kuitumia tena kwa matumizi ya kupiga wala kutuma sms hii ni kwa sababu itageuka na kuwa kama kopo, ila pia kama simu yako ina tracking device una uwezekano mkubwa wa kuweza kuitrack na kuipata japo kwa hapa Tanzania ni simu chache sana zenye uwezo huo 

Hayo ndio mambo niliyokuandalia ambayo unapaswa kuyafanya pindi tu unapo ibiwa au kupoteza simu yako ya mkononi,
kama una cha kuchangia au una maoni yoyote waweza share na sisi kupitia kwenye comment box hapo chini. kumbuka maoni na mchango wako wa mawazo ni muhimu sana kwetu.
ahsante 
MWISHO

soma pia  FAHAMU KAMA SIMU YAKO YA ANDROID NI ORIGINAL AU FEKI