Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond
Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la
‘Babu Tale’ hivi sasa yupo mikononi mwa polisi
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Babu Tale amekamatwa leo na kufikishwa
mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini
asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya
Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250
milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya
Hakimiliki.
Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na
kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde,
kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha
(DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo
ni kinyume na haki miliki.