Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ambaye pia ni
Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema amemtaka
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akubali
kwamba alishindwa katika uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015 na akae kimya hadi mwaka 2020.
Mrema aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam
na kusisitiza kwamba alimtaka Waziri Mkuu
Mstaafu watoke CCM pamoja kwa kuwa nguvu ya
upinzani ilikuwa kubwa sana.
‘’Mimi nitamuuliza 1995 wakati natoka nilikuambia
tutoke sasa maji yamechemka tukiweka unga
tutakula ugali ukagoma, ukasema unaendelea kula
kidogo hadi alipojiuzulu akaendelea na CCM hadi
alipotaka kugombea Urais akakataliwa na wenzake
ndipo akaja upinzani’’
Mrema aliongeza kwamba Chama cha Mapinduzi
kilitakiwa kuondoka madarakani mwaka 1995
ambapo yeye ndiye alikuwa na nguvu kubwa ya
kisiasa nchini.
Aidha Mrema amewataka vijana kuwa makini na
upinzania kwa kuwa Lowassa alijiunga na upinzani
baada ya kunyimwa nafasi ya kugombea Urais
ndani ya CCM hivyo wajiepushe na maandamano
kwani hayana faida kwao.
0 Comments
on