Header Ads Widget

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 5 & 6

Mtunzi: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“Samahani kaka sijui wewe ni nani mwenzangu?”
“Unaniuliza mimi ni nani ndani ya nyumba yangu?”
Moyo ukanipiga paaaa kama jiwe lililotua juu ya
bati tena la nyumba ya uswahilini.Nikajua jamaa
anaweza akawa mume wa Madam Mery mapigo ya
moyo yakazidi kunienda mbio pale jamaa
alipoanza kupiga hatua za kwenda chumbani kwa
Madam Mery kwani boxer na tisheti ya shule vyote
vipo ndani ya chumba hicho na vipo sehemu ya
wazi kwa mtu yoyote anayeingia lazima
ataviona,na kingine kilichozidi kunipagawisha ni
kitanda nilivyo kiacha kimevurugika kwani
kinaonyesha hivi hivi kilikuwa ni kiwanja cha mechi
za wakubwa
ENDELEA
Jamaa kabla hajafunua pazia ili aingie ndani
simu yake ikaita.Akaitoa kwenye mfuko wa suruali
kisha akaipokea na kuanza kuzungumza
mazungumzo ambayo yalianza na ndio
bosi.Jamaa akanitazama kisha akatoka nje
nikahisi mazungumzo yake ni muhimu sana na ya
siri sana ndio maana akatoka nje huku begi lake
akilivua na kuliweka pembeni ya mlango wa
kuingilia chumbani kwa Madam Mery.
Ikawa nafasi kwangu kuingia chumbani nikachukua
kila kilicho changu huku shuka lililo changungaka
nikilitoa na kulisokomeza mvunguni mwa kitanda
na kuliacha godoro likiwa na foronya yake tu
pasipo kuwa na shuka,Nikarudi hadi sebleni na
kumuona jamaa akirudi ndani kwani mlango
aliuacha wazi kidogo.Ikanibidi boxer yangu niiweke
mfukoni mwa suruali yangu huku tishet yangu
nikiwa nimeishika mkononi huku nikitaka kuivaa
“Dogo unakwenda wapi?”
“Ehee”
”Hujasikia…! Unakwenda wapi?”
“Kununua vitafunio vya chai”
“Dogo mbona unajifanya mjanja sana?”
Maswali ya jamaa yakazidi kunichanganya akili na
kunizidisia presha ambayo sikuelewa kama
inapanda au inashuka.
“Mjanja wa nini brother?”
“Huendi kununua vitafunio ila sema ninakwenda
kununua vitafunwa kwani vitafunio ni hayo meno
yako”
“Sawa bro nimekuelewa”
“Ehee kwanza hujaniambia wewe ni nani? Nakuona
upo upo tu humu ndani?”
“Mimi ninaitwa Eddy”
“Yuko wapi Mery?”
Nkaanza kufikiria cha kumjibu huku maswali
mengine nikijiuliza mwenyewe na kujijibu
mwenyewe ndani ya moyo wangu hadi nikapata
muafaka wa nijibu nini
“Amelazwa kwenye hospitali ya shule”
“Lini?”
“Leo asubuhi”
Lengo la kumjibu jamaa kiufasaha kila swali analo
niuliza ni ili akienda kumuangalia Madam Mery
iwe nafasi ya mimi kuondoka katika nyumba hiyo
ili nikatafute hata sehemu ya kuishi nikisubiria siku
zangu za kusimamishwa masomo ziishe
“Powa dogo vaa tisheti yako unipeleke huku
alipolazwa”
Sikuwa na ujanja zaidi ya kuivaa tisheti yangu na
kumalizia kuvaa viatu vyangu na kitu kilichozidi
kuniweka mpole mbele ya jamaa ni pale alipoitoa
bastola yake na kutazama kama inarisasi za
kutosha kwenye magazine yake na kuirudisha
kiunoni bastola yake huku akionekena kuridhika na
risasi zilizomo.
Safari ikaanza huku sote tukiwa kimya ila mimi
nimetangulia mbele kama hatua moja huku yeye
akifwatia kwa nyuma.Akili yangu ikawa inanituma
nipige hatua za haraka haraka na kama kuna
uwezekano nikimbie kwani vichochoro vyote
ninavijua katika mji huu wa Arusha
“Dogo nasikia kuna majambazi sana wamezuka
kipindi cha hivi karibuni?”
“Kusema ukweli bro mimi mwenyewe ninasikia
sikia ila sina uhakika kivile.Ila ni juzi kuna benki
pale mbele ilivamiwa na pesa zote zikaibiwa”
“Dogo subiri ninunue P.K hapa dukani si utakula?”
“Ndio”
Jamaa akaingia kwenye moja ya
duka,nikamchungulia kwenye duka hilo nikamuona
yupo bize na muuza duka.Nikaanza kupiga hatua
za taratibu huku nikizuga zuga watu waliopo katika
eneo hilo wasistukie kitu chochote ili nikifika
mbali na duka hilo nianze kukimbia.Kabla sijafika
mbali kidogo gafla nikastukia nikiguswa bega kwa
nyuma.Nikageuka na kukutana na muuza mahindi
“Oya broo yule jamaa pale mjeda ameniambia
nikuletee maindi uchague”
Nikatamani nimtukane muuzaji wa watu ila nikaona
hana kosa taratibu nikaanza kuyatazama mahindi
yaliyo chomekwa kwenye spoke za baiskeli
zipatazo kumi na kuunganishwa katika mti
mmoja.Nikachagua muhindi laini laini kwani
sikuwa nimekula kitu cha aina yoyote tangu
asubuhi.Jamaa akaja hadi tulipo akatoa noti ya
elfu kumi na kumpa muuza maindi na kumuambia
chenchi akae nayo
“Aisee kamanda wangu Mungu akubariki sana”
Muuza maidi alizungumza kwa lafudhi ya kichaga
huku akipiga saluti na kumfanya jamaa acheke ila
mimi sikuwa na hata hamu ya kuyakenua meno
yangu.Tukaendelea na safari ya kwenda katika
hospitali ya shule ambayo haikuwa mbali sana na
shule kwani ilikuwa pia inatoa msaada wa
kuwahudumia wananchi wa kawaida tofauti na
wanafunzi
Tukafika hospitalini na tukakutana na Madam
Rukia akiwa nje ya wodi ya
wagonjwa,nikamsalimia nikabaki nikiwatazama
jinsi anavyo salimiana na jamaa huku wakicheka
kwa furaha na kuonekana wakifahamiana kwa
muda mrefu
“Huyo mwenzako anaendeleaje?”
“Kidogo joto lake limeshuka kwani asubuhi hali
yake haikuwa nzuri kivile”
“Tatizo lake ni nini haswa?”
“Maleria alikutwa na vidudu sita ndio vimemlaza.”
“Sasa mbona umekaa huku nje?”
“Nilitoka mara moja kupunga punga hewa ila
twende ukamuone”
Wakati wote wanazungumza nilikuwa kimya
nimetulia kama maji ya mtungini huku moyoni
nikifurahia jamaa aingie ndani na mimi niondoke
.Jamaa na Madam Rukia wakaanza kuingia ila
jamaa akasimama na kuniangalia
“Oya dogo twende ukamuangalie mgonjwa”
“Huyu mwalifu umemtoa wapi?”
Madam Rukia alimuuliza jamaa na kumfanya
atabasamu ila kwangu nikazidi kuogopa,cha
kumshukuru Mungu jamaa hakulijibu swali la
Madam Rukia kwani tayari tulishafika ndani ya
chumba alicholazwa Madam Mery.Jamaa akakaa
kitandani na kumkumbatia madam na wote kwa
pamoja wakawa wanatokwa na machozi ya
furaha,sikujua kinacho waliza ni nini
Wakaachiana huku jamaa akianza kumfuta Madam
Mery machozi kwa kutumia kitambaa chake na
kunifanya roho yangu kuanza kuhisi maumivu ya
wivu

Post a Comment

0 Comments