Chama
Cha Wananchi (CUF) kimewasimamisha uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa
chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa chama hicho
upande wa Bara, Magdalena Sakaya.
Uamuzi
huo umetolewa jana na Baraza Kuu la Chama hicho lililofanya mkutano
wake visiwani Zanzibar kwa lengo la kuwajadili wanachama kadhaa wakiwemo
vigogo hao. Sakaya amevuliwa nyadhifa zote ndani ya chama kabla ya
kusimamishwa.
Taarifa
kutoka ndani ya Mkutano huo zimeeleza kuwa Baraza hilo limewaadhibu
wanachama 15 wakiwemo Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua.
Mbali
na vigogo hao, wengine waliopigwa rungu na Baraza Kuu la CUF ni pamoja
na Katibu wa Baraza la Wazee, Shashi Lugeye, Thomas Malima na Naibu
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano, Abdul Kambaya.
Aidha,
Baraza hilo limemsimamisha uanachama Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah
Nachuma. Hatua hii inaweka matatani ubunge wa Sakaya na Nachuma kwani
wakifikia hatua ya kufukuzwa watakosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.
Lipumba
na Sakaya hawakupata nafasi ya kujitetea kutokana na kutohudhuria
mkutano huo wakati Shashi alipata nafasi ya kujitetea kutokana na uwepo
wake lakini utetezi wake haukuzaa matunda. Katiba ya chama hicho haiwapi
nafasi wabunge hao kukata rufaa kutokana na uamuzi wa Baraza hilo.
Uamuzi
huo umekuja ikiwa ni siku chacha baada ya Mkutano Mkuu Maalum wa Chama
hicho uliolenga kumchagua Mwenyekiti Mpya kuvunjika kutokana na kuwepo
vurugu kubwa baada ya Profesa Lipumba kuingia ndani ya ukumbi huo na
wafuasi wake wakitaka barua yake ya kutaka kurejea kwenye nafasi yake
ijadiliwe na kukubaliwa.
0 Comments
on