Label ya WCB Wasafi ya Diamond Platnumz inafungua ofisi mpya Kijitonyama jijini Dar es salaam ambayo itakuwa inajihusisha na masuala ya kiuongozi zaidi.
Akiongea Jumatatu hii, mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam, amesema wanafungua ofisi mpya ili kuipa nafasi ofisi ya zamani ya kufanya shughuli zake bila kuingiliana na shughuli zingine.
“Tunafungua ofisi nyingine ya WCB Kijitonyama,” alisema Sallam.“Hii itakuwa kwa ajili ya viongozi, halafu ile nyingine nitaendelea na kazi nyingine,”
WCB kwa sasa ni moja kati ya label za muziki ambazo zinafanya vizuri kutokana na wasanii wake wengi kufanya vizuri.