Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa
Mgeni rasmi siku ya Kilele cha maadhimisho ya
siku ya Vijana Kitaifa yatakayofanyika Mkoani
Simiyu Oktoba 14 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira
na Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde wakati
wa mkutano na waandishi wa Habari.
Mhe Mavunde alibainisha kuwa Kauli mbiu ya Siku
ya Vijana mwaka huu ni “Tokomeza umasikini kwa
uzalishaji endelevu na matumizi yenye tija”.
Akifafanua kuhusu kauli mbiu hiyo Mhe. Mavunde
alisema lengo la kauli mbiu hii ni kuzihimiza nchi
wanachama wa umoja wa mataifa kushirikisha
kikamilifu Vijana katika shughuli za uzalishaji na
kuhakikisha kuwa panakuwepo na matumizi sahihi
ya rasilimali za nchi kama vile ardhi,maji,madini
na Nishati ili kufikia shabaha ya kuwa na
maendeleo endelevu ifikapo 2030.
Akizungumzia maadhimisho hayo Kitaifa Mhe .
Mavunde alisema kuwa vijana watapata fursa ya
kushiriki shughuli mbalimbali kama
makongamano,matamasha,michezo,maonnyesho
ya Kazi za Vijana,Shughuli za kujitolea na
maandamano ya amani.
“Tanzania tutasherekea siku ya Vijana Duniani
Kitaifa kuanzia tarehe 8/10/2016 na kilele kitakuwa
tarehe 14/10/2016 Mkoani Simiyu ambapo Sherehe
hii itaenda sambamba na Maadhimisho ya
kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl.
Julius Kambarage Nyerere, Wiki ya Vijana Kitaifa na
kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016.”
Alisisitiza Mhe. Mavunde.
Wazo la kuwa na siku ya Vijana Duniani lilitolewa
katika Mkutano wa Vijana wa Kimataifa mwaka
1991 Mjini Vienna Australia kwa madhumuni ya
kutafuta njia ya kuchangisha fedha za kusaidia
mifuko ya Taifa ya Vijana ambapo mwaka 2000
nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo
Tanzania zilianza kuadhimisha siku ya Vijana
Duniani kulingana na mazingira yake kwa
kuzingatia kauli mbiu ambayo huandaliwa na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
0 Comments
on