Rapper Darassa ambaye kwa sasa anatamba na
ngoma yake ya Too Much amedai kwamba
harakati zake za muziki zinampa wakati mgumu
sana hasa kwa watu wake wa karibu kutokana
na ratiba ngumu aliyo nayo hivyo kutokuwa nao
karibu mara kwa mara.
Akihojiwa kwenye kipindi cha Ladha 3600 cha
EFM,Darassa amedai kuwa ndoto zake za
kimuziki zimemfanya awe anafanya kazi muda
mwingi zaidi hivyo kukosa muda wa kukaa na
watu watu wake wa karibu kama ilivyokuwa
zamani.
   
“ ..sasa hivi nimekuwa na wakati mgumu hata
na baby,wakati mgumu na ndugu zangu pamoja
na washikaji, hatuonani mara nyingi
sana..hatupigi sana stori kwa sababu kuna goli
nalihangaikia,so once nikiwa poa itakuwa ni
rahisi kufanya vitu vingine,ila kuna vitu nahitaji
kufanya kwa sasa”alifunguka Darassa na
kuwataka mashabiki zake wategemee ngoma
kali zaidi kutoka kwake.