Na Jonas Kamaleki-Maelezo
Serikali yajipanga kupunguza ajali za barabarani
kwa kiwango cha takribani asilimia 10 hapa nchini
ili kupunguza vifo na majeruhi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Yusuf Hamad
Masauni kuwa baraza la Usalama Barbarani
linakerwa sana na kadhia ya ajali za barabarani
ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.
“Kukithiri kwa ajali za barabarani kwa siku za hivi
karibuni, umewezesha Baraza kuibuka na Mkakati
wa Miezi Sita (6) unaolenga katika kukabiliana na
ajali za barabarani nchini, mkakati huu ni wa muda
mfupi kuanzia mwezi Agosti, 2016 hadi Februari
2017 tutakapokaa na kutathmini matokeo yake”,
alisema Masauni.
Masauni amesema ajali za barabarani zimewaacha
watoto wakiwa yatima na kuwafanya akina mama
kuwa wajane, hivyo juhudi za makusudi inabidi
zifanywe ili kupunguza kama sio kuondoa kabisa
ajali hizo.
Ametaja vyanzo vikuu vya ajali za barabarani nchini
kuwa ni pamoja na Makosa ya Kibinadamu,
mazingira ya barabara na ubovu wa vyombo vya
moto.
Naibu waziri huyo amesema takwimu za ajali
barabarani katika miaka mitatu tangu 2012 ajali
ziliongezeka toka 23,578 hadi 23, 842 kwa mwaka
2013, vifo vilikuwa 3,969 kwa mwaka huo hadi
kufikia 1,043 mwaka 2013.
Vifo hivyo vilipungua hadi kufikia 3,760 mwaka
2014, upungufu huo ulitokana na usimamiaji
madhubuti wa Sheria na kanuni za Usalama
barabarani pamoja na juhudi zilizofanya na Baraza
kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Kwa mujibu wa Masauni, Mkakati uliozinduliwa
unalenga kudhibiti makosa yanayosababisha
madhara makubwa na ambayo husababisha
kuongezeka kwa ajali za barabarani.
Ameyataja mambo hayo kuwa ni:
1. Udhibiti wa madereva walevi na kuendesha kwa
uzembe.
2. Udhibiti wa mwendokasi kwa madereva na
wamiliki wa magari; kuwa na madereva wenza
3. Uendeshaji magari bila sifa/leseni ya udereva
na bima
4. Udhibiti wa usafirishaji wa abiria kutumia magari
madogo yenye muundo wa tairi moja nyuma kwa
mfano; Noah, Probox
5. Kudhibiti ajali za pikipiki za magurudumu mawili
‘bodaboda’ na magurudumu matatu
6. Abiria kufunga mikanda ya usalama
wanapotumia vyombo vya usafiri
7. Kuyabaini na kuyadhibiti maeneotete na
hartarishi ya ajali za barbarani ‘black spots/
kilometers’
8. Kuangalia uwezekano wa kufanya marekebisho
ya sheria za usalama barabarani.
9. Kuanza kwa mfumo wa nukta ‘point system’
kwenye leseni za udereva.
10. Kutoa mafunzo ya msasa yanayolenga katika
kuimarisha utendaji wa askari wa usalama
barabarani.
11. Kuhakikisha kuwa waendesha bodaboda
wanafikiwa na kupewa mafunzo yaa uhakika juu
namna na jinsi ya kuzitumia barabara kwa usalama
zaidi.
12. Kudhibiti rushwa na kuwaadhibu watoaji na
wapokeaji wa rushwa katika barabara zetu nchini.
13. kuwahusisha wamiliki wa magari ya abiria na
ya mizigo, katika kuutekeleza mkakati.
14. Mkakati mwingine waliouweka ni kuwa Dereva
ukikamatwa unapelekwa rumande na baadae
mahakamani kujibu shitaka litakalokuwa
linakukabili.
0 Comments
on