WATU watatu wamekufa papo hapo na wengine
wanane kujeruhiwa baada ya basi lenye namba za
usajili T 402 CRY aina ya Scania mali ya Kampuni
ya Kisbo – Safari kupinduka mkoani Morogoro.
Basi hilo lilikuwa likitoka mkoani Tabora kwenda
Dar es Salaam.
Imeelezwa kuwa basi hilo lilipinduka wakati
likijaribu kukwepa gari lingine eneo la Kwambe,
wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro kwenye
barabara kuu ya Dodoma – Morogoro.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro,
Leonce Rwegasira alisema kuwa tukio hilo lilitokea
majira ya saa 12: 30 jioni, juzi, mwaka huu eneo
la Kwambe, kata ya Dumila, tarafa ya Magole
wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwenye barabara
kuu ya Dodoma- Morogoro.
Alisema basi hilo likiendeshwa na Davis Samora
(38) mkazi wa Dar es Salaam liliacha njia na
kupinduka wakati likijaribu kukwepa gari lenye
namba za usajili T957 BUV aina ya Scania lenye
trela namba T 919 BVA likiendeshwa na dereva
asiyefahamika akitokea Morogoro kwenda Dodoma
na ambaye alikimbia baada ya ajali kutokea.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Morogoro, dereva huyo alijaribu kuyapita
magari matatu mbele yake bila tahadhari na
kusababisha ajali hiyo.
Kaimu huyo alitaja majina ya waliokufa kuwa ni
Francis Shija (70) mkazi wa Nzega, mkoa wa
Tabora, mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na
umri wa miaka 45 hadi 50 ambaye hajatambulia
jina , pamoja na mtoto mdogo wa kiume ambaye
bado hajatambuliwa kwa jina na umri wake ni kati
ya miaka mitatu hadi minne.
Aliwataja majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Morogoro ni Kinazi Machum
(38), ambaye ni Mhandisi na Mkazi wa Tabora,
Mathei Fidelis (30), mkazi wa Singida na Baraka
Ruta (4) mkazi wa Mwanza.
Wengine ni Juma Bilal (30) mkazi wa Nzega,
Ebebeza Richard (22) mkazi wa Mbeya, Hamis
Mogela (30) mkazi wa Nzega, Pili Waziri (44)
mkazi wa Tabora na Prisca Shija (30) mkazi wa
Nzega na wote wanaendelea vyema, wakati maiti
wakiwa wamehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhi maiti cha Hospitali hiyo ya Rufaa.
Kaimu Kamanda alisema kuwa, polisi wanaendelea
kumtafuta mtuhumiwa ambaye ni dereva wa gari T
957 BUV aina ya Scania lenye trela namba T 919
BVA ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria
0 Comments
on