Header Ads Widget

Waziri mkuu akagua Kiwanda cha Mtibwa

Jana tarehe 3/4/2016 Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa ametembelea Kiwanda cha Kuzalisha
Sukari cha Mtibwa, kuangalia kiwanda chenyewe
na kupata Maelezo kwa nn kiwanda hicho
hakizalishi Sukari
Aidha alitembelea eneo ambalo linaendelea
kupanuliwa kwa ajili ya mashamba ya miwa ikiwa
ni pamoja na kutembelea ujenzi wa mitambo ya
kusukuma maji kutoka Mtoni hadi kwenye
mashamba ya miwa.
Hayo yote yalifanyika baada ya kupewa taarifa na
uongozi wa kiwanda ambao umeomba Serikali
iwasaidie masuala kadhaa kama; kuwahakikishia
Udhibiti wa Sukari inayoingizwa kutoka nje ya nchi
na wanaoingiza watozwe kodi ili kuwa na
ushindani sawa katika kuiuza kwa wananchi.
Wameiomba Serikali pia kuzibamyanya ya uingizaji
wa sukari kwa njia za panya.
Kuvutiwa umeme wa KV zaidi ya 32, Serikali
kudhamini viwanda Mara wanapotaka kukopa
fedha Bank za nchi za nje, kujengewa Daraja la
Dakawa, kuomba mashirika ya Kijamii kuwekeza
katika viwanda nk.
Mwisho Mhe. Waziri Mkuu aliwahutubia wananchi
wa Tuliani na muwata kufanya kazi kwa bidii,
kusaidia azma ya Serikali ya ukusanyaji wa kodi
ktk maana ya kutoa na kudai risiti kwa kila kitu
Mwananchi anachouza/kununua. Pia alisisitiza
kutotoza ushuru kwa wafanyabiashara wadogo.
Wananchi nao kupitia Mbunge wao Mhe. Saddiq
waliwakilisha kero zao zikiwemo: gharama kubwa
ya madawa ktk Hospitali Teule ya Bwagala,
migogoro baina ya wakulima na wafugaji,
mahusiano hafifu na kiwanda cha Sukari cha
Mtibwa n.k.
Kuhusu gharama ya madawa kuwa kubwa hospitali
ya Bwagala ameahidi kumtuma Waziri Mwenye
dhamana kuja kulitatua. Kuhusu migogoro ya
wakulima na wafugaji amerudia mpango uliopo wa
Serikali wa kutumia Ranchi zote kuzigawa ktk
Blocks na kugawa kwa wafugaji kadri ya idadi ya
mifugo. Kwa sasa ameshauri kuwa kila upande
uheshimu Mali ya mwenzake na anayekiuka agizo
hilo sheria ichukue mkondo wake.
Kuhusu mahusiano kati yao na kiwanda amekitaka
kiwanda Kujitahidi kuweka mahusiano mema na
wananchi kwa kushawishi Out growers kuendelea
kulima miwa lakini kiwanda kinunue miwa yao bila
kuwanyonya.
Lakini pia kulipa malipo wanayodai na wakylima,
wafanyakazi na wastaafu. kuwaletea wananchi
maendeleo yao ikiwa ni pamoja na kushirikiana
katika masuala ya kijamii kama kujenga shule,
hospitali, maji nk.
Kabla yakuongea na wananchi hao kulikuwa na
zoezi la kupokea madawati 880 kutoka kwa
wakala wa Misitu TFS ambapo Mhe.Kassim
Majaliwa aliyakataa madawati 84 kati ya yale
yaliyoletwa uwanjani hapo kwa kuwa hayakuwa na
ubora uliohitajika na kuyataka yarudishwe kwenye
karakana kutengenezwa kufikia ubora unaohitajika.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
ameutaka Uongozi wa Serikali ngazi ya Mkoa wa
Morogoro na Wilaya ya Mvomero kuhakikisha
inaondoa vikwazo vyovyote vitakavyojitokeza
kukwamisha Kiwanda cha nyama cha Nguru Hills
kutofikia malengo yake.
Mhe. Majaliwa ametoa agizo hilo Leo
alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Wilayani
Mvomero Mkoani hapa.
Amesema kiwanda hicho pamoja na kuliongezea
pato taifa lakini pia kitatoa ajira kwa vijana
takribani 300 na kuondoa migogoro kati ya
wakulima na wagugaji.
"Kiwanda hiki kitasaidia kuondoa migogoro baina
ya wakulima na wafugaji kwa kushawishi wafugaji
kuuza mifugo yao katika kiwanda hiki kwa bei
yenye tija na hivyo kupunguza ukubwa wa
migogoro katika Mkoa wa Morogoro" amesema.
Hata hivyo ameitaka Wizara ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi Kutoa elimu kwa wafugaji kukubali na
kutekeleza azma ya Serikali ya kutaka Ranchi zote
za taifa kugawanywa ktk Blocks na kutolewa kwa
wafugaji ili wafuge mifugo yao kwa tija na hivyo
kuepusha migogoro inayojitokeza.
Kwa upande wa wananchi wanaozunguka kiwanda
hicho cha nyama amewataka kutoa ushirikiano na
kuwa walinzi wa kiwanda kwa kuwa kina manufaa
kwao na kwa Taifa ikiwemo ajira, kuondoa
migogoro iliyopo sasa kununua mazao yao kwa
ajili ya kunenepesha mifugo inayotarajiwa
kuchinjwa kiwandani hapo na kiwanda kusaidia
masuala ya mengine ya kimaendeleo kama afya,
elimu maji n.k.
Kiwanda cha Nguru Hills kinatarajia kukamilika
Mwezi Disemba mwaka huu na kitakapokamilika
kitakuwa na uwezo wa Kuchinja ng'ombe 300 na
mbuzi 1500 kwa Siku.
Mhe. Waziri Mkuu amekamilisha ziara yake ya siku
tatu Mkoani hapa kwa kutembelea kituo cha
mabasi yaendayo mikoani cha msamvu ambacho
kinatarajiwa kukamilika wiki mbili zijazo.

Post a Comment

0 Comments