Askofu mmoja wa kanisa la Kianglikana nchini Uingereza amekuwa wa kwanza kutangaza hadharani kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja.
Kasisi Nicholas Chamberlain ,amesema kuwa walioshiriki katika mchakato wa kumteua mwaka uliopita walielewa fika mwelekeo wake wa jinsia.
”Watu wanajua nashiriki mapenzi ya jinsia moja ,lakini si kitu cha kwanza nachoweza kumwambia yeyote.Jinsia ni sehemu ya yule niliye,lakini ni kazi yangu ya kitume ambayo ninataka kuiangazia.”
Nicholas Chamberlain anasema hata hivyo anafuata kanuni za kanisa zinazosema kuwa haruhusiwi kuoa.
Msemaji wa kanisa la Anglikana nchini Uingereza amesema “Nicholas hajamkera yeyote na amekuwa wazi na mkweli ukiuliza, Suala lake si la siri ,ingawa ni la kibinafsi kama ilivyo kwa wale walio katika mahusiano ya kimapenzi.”
Inadhaniwa kuwa hakuna skofu yeyote anayehudumu aliyewahi kutangaza hadharani msimamo wake wa kingono.
Kanisa la Kianglikana kote duniani limegawanyika sana miaka ya hivi karibuni kuhusu masuala yanayohusu mwelekeo wa kijinsia na kutawazwa kwa makasisi walio katika mapenzi ya jinsia moja
0 Comments
on