Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia...
Nikafanya kama dorecy anavyo niagiza, gafla tukaiona gari moja mbele yetu, aina ya pick up ikiwa na watu wenye bunduki zao huku mmoja wao akiwa ameshika bomo aina ya rocket ambalo upigaji wake analiweka begani na kulifyatulia.Sote tukafunga breki za magari yetu na majamaa wakaanza kushuka huku mwenye bomo akiwa ametuelekezea kwetu akijiandaa kutufyatulia
Endelea....
Macho yangu yangu yakawatazama jamaa walio shika bunduki mikononi mwao, wote wanaonekana wapo makini katika kutushambuli sisi.Kwa kupitia kioo pembeni, nikaangalia nyuma na kuona kuna kona ambayo ipo karibu na sehemu tulipo simama, nikakanyaga mafuta na gari kuanza kuirudisha nyuma kwa kasi kubwa, jamaa wakaana kutushambulia kwa risasi ambazo kwa bahati nzuri hazikuingia kwenye gari, kitendo cha kukunja tu, bomu alilo lifyatua jamaa likapita mita chache kutoka sehemu gari letu lilipo na kwenda kugongwa kwenye miamba na kusababisha mlipuko mkubwa na mawe yakaziba barabara kwa nyuma na kushindwa kurudi nyuma.
Ilipoishia...
Nikafanya kama dorecy anavyo niagiza, gafla tukaiona gari moja mbele yetu, aina ya pick up ikiwa na watu wenye bunduki zao huku mmoja wao akiwa ameshika bomo aina ya rocket ambalo upigaji wake analiweka begani na kulifyatulia.Sote tukafunga breki za magari yetu na majamaa wakaanza kushuka huku mwenye bomo akiwa ametuelekezea kwetu akijiandaa kutufyatulia
Endelea....
Macho yangu yangu yakawatazama jamaa walio shika bunduki mikononi mwao, wote wanaonekana wapo makini katika kutushambuli sisi.Kwa kupitia kioo pembeni, nikaangalia nyuma na kuona kuna kona ambayo ipo karibu na sehemu tulipo simama, nikakanyaga mafuta na gari kuanza kuirudisha nyuma kwa kasi kubwa, jamaa wakaana kutushambulia kwa risasi ambazo kwa bahati nzuri hazikuingia kwenye gari, kitendo cha kukunja tu, bomu alilo lifyatua jamaa likapita mita chache kutoka sehemu gari letu lilipo na kwenda kugongwa kwenye miamba na kusababisha mlipuko mkubwa na mawe yakaziba barabara kwa nyuma na kushindwa kurudi nyuma.
Nikafunga breki na kulisimisha gari, sote tuakashuka kwenye gari huku bastola zetu zikiwa mikononi,tukaifungua milango ya gari na kujificha nyuma ya milango kwani uzuri wake haipitishi risasi.Bastola zetu zikawa zimeelekea kwenye kona ambapo tunatarajia majambazi kutokea.Ukimya wa kama dakika tatu ukatawala, hatukuona watu ambao wanajitokeza kwenye kona, nikataka kunyanyuka
“eddy kaa chini”
Dorecy alizungumza kwa sauti ya ukali, nikatii kwa haraka na risasi ikapiga kwenye kioo cha gari katika mlango ambao nipo mimi.Dorecy akaanza kufyatua risasi zilizo elekea walipo majambazi, kila risasi ambayo ninaipiga mimi haikumpata mtu yoyote zaidi ya kupiga pembeni, hata kama mtu nimemlenga vizuri ila haikumpata
“nakosea wapi?”
Nilizungumza kwa sauti ya juu
“kaza mkono”
Dorecy alizungumza, huku akiendelea kufyatua risasi kwa majambazi ambao wanatoa vilio vya maumivu kila aliye pigwa na risasi.Nikaingia ndani ya mlango na kuufunga mlango wa upande ambao nipo
“unafanya nini?”
“ngoja nikuonyeshe”
Nikaiwasha gari na screen(kioo), kilichopo pembeni yangu kikawaka na kuniandikia maneno yaiyo nichosha
‘system weapon empty’ ikimaanisha hakuna silaha yoyote inayoweza kufanya kazi kwani zimeisha.
“shitiii”
Nilizungumza huku nikiupiga mskani kwa kitako cha bastola
“vipi?”
“kuna, ishu nilikuwa ninaicheki kwenye hii gari.Imeisha”
“ni nini?”
“silaha, naomba hilo jaketi lako la kuzuia risasi”
Dorecy alinitazama kwa muda kisha akavua bullet proof yake na kunirushia upande niliopo, nilalivaa vizuri na mara nyingi nilikuwa nikimuona mzee godwin akilivaa jinsi nilivyo livaa nikiwa mtoto mdogo.Kwani kuna siku nyumbani tulivamiwa na majambazia nyumbani, akatuvalisha sote kisha yeye alielekea kupambana nao na siri moja aliyo niambia ni kwamba jaketi hili linamionzi ambayo hata ukiwa umelengwa kupigwa risasi ya kichwa basi inaivuta na kukimbilia kifuani.
“vipi huku, mbele mimi ngoja nipande hapo juu”
Nilimuambia dorecy, nikapanda kwenye gemo ambalo lipo pembeni yetu, nikapanda hadi pasipo majambazi kuniona, nikatafuta sehemu nzuri ya kusimama ambayo nikawa ninawaona kwa chini, nikawahesabu kwa haraka na kuwaona wakiwa wamebaki wanne wamejibanza kwenye gari lao wakimsubiria dorecy kujitokeza, dorecy naye akawa amejibanza kwenye gari akiwasubiri wajitokeze
Nikaishika bastola vizuri, nikafumba jicho langu moja huku nikiitazama sehemu yenye mfuniko wa tanki la mafuta kwenye gari, nikameza mate mengi kisha nikafyatua risasi tatu mfululizo huku nikiwa nimeikaza mikono yangu, risasi mbili zikapiga pembeni, jambo lililo wachanganya jamaa.Risasi ya tatu ikapiga kwenye tanki la mafuta na kulifanya gari kulipuka, huku likinyanyuliwa juu na jamaa wote wakarushwa pembeni.Hadi gari linatua chini milango na matairi yake yalichanguka vibaya.
Nikashuka kwenye gemo kupitia njia niliyo pandia na kumkuta dorecy akiwa bado ameshika bastola yake akiielekezea walipo majambazi, nikatembea kwa mwendo wa tahadhari hadi ilipo gari ya majambazi, nikaanza kuhakikisha jambazi mmoja baada ya mwengine kama amekufa, ambaye ninamkuta kwenye hatua za mwisho za maisha yake nilampiga risasi ya kumsindikiza kuzimu
Nikageuka nyuma na kumkuta dorecy akiwa ananitazama kwa macho ya mshangao, kwani haamini kama nitaweza kuwapiga risasi wezake ambao amewasaliti, nikarudi lilipo gari na kuingia, nikaliwasha hadi sehemu alipo, akafungua mlango na kuingia.Nilalipitisha pembeni gari langu taratibu kulikwepa gari linalo teketea na kuandelea na safari.Dorecy akaendelea kunielekeza njia hadi tukatokea barabara inayotokea tanga kuelekea moshi
“eddy, ulisha wahi kuua?” dorecy aliniuliza
“swali gani sasa hilo?”
“hapana, kwa mtu ambaye hazifanyi hizi kazi hawezi kuwa kufanya kama ulivyo fanya wewe”
“nimefanyaje?”
“ulivyo wapiga wale, risasi waliokuwa wakikaribia kufa”
“kawaida”
Nilimjibu huku nikendelea kuendesha gari kwa umakini, macho yangu yote yakawa ni barabarani kuangali kama polisi wa usalama barabarani wapo au hakuna.Tukaingia kwenye motel iitwayo mombo motel iliyopo kwenye barabara ya mombo
“una pesa?”
Nilimuuliza dorecy
“ndio”
“kachukue chakula basi”
“utakula nini?”
“bufee,nyama chukua na soda za take way”
Dorecy akalivua shati lake na kubaki na vest ya kiume, akaziweka vizuri nywele zake ndefu, akaichomeka bastola yake kwenye buti la jeshi, mguu wa kulia na kushuka ndani ya gari.Kwa kupitia kioo cha pembeni nikawaona askari wa usalala barabarani, wakiingia kwenye geti la motel wakiwa na pikipiki.
Wakaisimamisha pikipiki nyuma ya gari langu na kunifanya nianze kupata wasiwasi, kwani sihitaji kumwaga damu tena katika eneo hili.Mmoja akaanza kulitazama gari langu vizuri, akaanza kulizunguka taratibu huku akilitazama kadi zake za usajili zilizo bandikwa kwenye kii cha mbele
“anataka nini huyu?”
Nilijizungumzia kimya kimya, akanionyesha ishara ya kufungua kioo cha gari langu, akanitazama kwa sekunde kadhaa
“anataka nini huyu?”
Nilijizungumzia kimya kimya, akanionyesha ishara ya kufungua kioo cha gari langu, akanitazama kwa sekunde kadhaa
“habari yako afande?” nilianza kumsalimia
“salama, gari yako ilipata nini?”
“kivipi?”
“imebonyea pembeni huku?”
“ilipata ajali, afande”
Nilizungumza huku mkono wangu wa kulia ukiwa umeishika bastola, huku nikiwa nimeficha pembeni ya siti yangu
“unatakiwa ukaiyooshe, kwa maana gari ya kifahari inakuwa haileti picha nzuri”
“sawa afande”
“insuarence yako nayo ipo katika siku za ukingoni”
“yote nitayafanya, nikifika ikulu”
Niliingiza swala la ikulu kwa maana askari, anahisi kama mimi ni miongoni mwa askari, hii nikutoka na bullet proof niliyo ivaa
“ahaaa, upo ikulu wewe?”
“yaaa”
“wezetu nyinyi wa ikulu muna kula kula pesa”
“tunakua pesa wapi kaka, kazi nyingi kama hizi unazo ziona”
“ila si kwa kila kazi unapata mkwanja mrefu?”
“inategemea, na kazi”
“ahaa sisi wa barabarani huku ni shida”
“shida gani?”
“ahaaa, madereva wenyewe wabishi kama nini”
“wabaneni”
Nilizungumza huku nikijiamini sana, kwani tayari nimesha muingiza choo cha kike huyu askari.Dorecy baada ya kuwaona askari akastuka, ila akajikaza na kwajinsi alivyo vaa askari ninaye zungumza naye akazidi kuamini kuwa sisi ni askari kutoka ikulu.
“habari yako, afande?”
Dorecy alimsalimia askari
“salama tuu, jamani ngoja niwaache muende”
“asante afande kwa muda wako”
“ila kaka kama kukiwa na nafasi basi, huko ikulu tukumukane”
“usijali kaka yangu”
“naomba namba yako ya simu”
“nitajie yako kwa maana ninabadilisha badilisha namba za simu, si unajua kazi zetu hizi”
Askari akanitajia namba yake ya simu, tukaagana naye na kuondoka bila ya wao kutustukia juu ya kitu chochote
“eddy, nimesikia ikulu?”
“ahaaa mzembe yule, alivyo niona nimevaa hivi akazani mimi ni askari”
Dorecy akaanza kucheka sana,
“eddy your geniuse boy”
“kwa nini?”
“umemtekaje tekaje hadi kakuamini?”
“njaa zake tuu yule, nahisi”
Safari ikaendela kwa mwendo wa kawaida, hadi tunafika korogwe akawa ememalia kula, nikasimamisha gari pembeni na kumpisha dorecy upande wangu wa dereva kisha mimi nikakaa upende alio kuwepo na kuanza kula.
“eddy, tunaelekea dar au wapi?”
“dar”
“unajua mimi sio mwenyeji wa dar”
“wewe ni mtu wapi?”
“kagera na nimwanajeshi, ambaye nilikuwa upande wa baba yako.Alitushawishi hadi tukawa tunafanya kazi zake isitoshe yeye ni mkubwa hatukuwa na kauli juu ya hili, ndio maana ikafikia kipindi nikaamua kuwasaliti, niachane na kazi zake”
“kwani, mulikuwa munafanya kazi gani?”
“kazi nyingi tu za kigaidi, hadi kazi ile ya kukuteka wewe, mimi ndio nilikuwa muendeshaji wa gari la mbele”
“wewe ndio ulikuwa kihere here sana kwenye kunimulika mataa”
“ahaa tutafanyaje sasa, wakati bosi ndio kashasema”
“na ile siku niliwapeleka”
“ahaa wee acha tuu, nilikuwa ninaendesha gari hadi mikono inaniuma”
“sasa, mulijuaje kuwa ninarudi?”
“unajua ilikuje, mzee alimpigiwa simu na askari ambao, sijui walikuwa wanakukimbiza arusha.Sasa, wale askari walikuwa wanataka kukufukuzia, ila mzee akasema wamuachie kazi yeye.Ndio maana ulistukiza gari zikiwa zinakufwata tuu”
“mmmmm.....”
“yaani hapa umeichokoza vita, na mzee wako anamkono mrefu sana”
“mungu bariki nitayashinda”
“yaa, kikubwa ni kupambana hadi dakika ya mwisho.Fungua hapo kuna bastola yako”
Nikafungua kwenye sehemu ya kuhifadhia vitu iliyopo mbele kwenye siti niliyo kaa, nikaikuta bastola ya mama
“niliiweka, mimi hapo”
“asante”
Hadi tunaingia dar es salaam, hatukupata tatizo la kusimamishwa na askari yoyote njiani, moja kwa moja tukaelekea nyumbani.Hadi tunafika nyumbani ilishatimu saa kumi na moja jioni, dorecy akasimamisha gari sehemu ya magesho ya magari baada ya geti kufunguliwa.
“karibu ndani”
“asante”
Tukaingia ndani na dorecy, sikumkuta mtu yoyote ndani, nikatoka na kwenda gaetini na kumuuliza mlinzi
“mama yupo wapi?”
“ni siku ya pili tangu aondoke jana na yule sister hajarudi”
“sister gani?”
“yule uliye kuja naye,majuzi”
“sheila?”
“ndio”
“powa”
Nikarudi ndani na kuchukua simu ya mezani na kumpigia mama simu, ikaita kwa muda kisha ikapokea
“mama upo wapi?”
“eddy.....Eddy.Umecheza pata potea”
Niliisikia sauti ya mzee godwin ikizungumza kwa dharau huku akicheka,wasiwasi ukaanza kunivaa
“yupo wapi mama yangu?”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali
“mama yako ame reast in peace”(.......Amepumzika kwa amani)
Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio, huku jasho jingi likimwagika midhili ya maji, dorecy akasimama kwenye sofa na kunifwata sehemu nilipo, akanipokonya simu na kuishika mkononi
“haloo.....Eddy........Ulisema ufe wewe, kwa ajili ya mama yako.Ila kwa bahati mbaya mama yako ndio hivyo amesha tangulia mbele za haki”
Sauti ya mzee godwin iliendelea kusikika kwenye simu akizungumza kwa sauti iliyo jaa dharau
“do you know, who will be the next to die?”(je una unajua, ni nani atafwata kufa?)
“hhahaahaaaa is your sheila, na leo nimepata tunda lake kwa mara nyingine tena, yupo so mwaaaaaaaaaa”(hhahaahaaaa ni sheila wako, ........)
“enjoy your day, mr eddy”(furahia siku yako, bwana eddy)
Simu ikakatwa, nikashindwa kuyazuia machozi yangu, kwa mara nyingine mzee godwin anawateka watu wangu wa karibu.Dorecy akanishika mkono na kunikalisha kwenye sofa, hasira taratibu ikaanza kupanda na kujikuta mwili wangu wote, ukianza kunitete, dorecy akanitazama kwenye macho yangu.Mlango wa kuingilia ndani ukafunguliwa na kujikuta nikichomoa bastola yangu na kumuelekezea mlinzi aliye fungua mlango
“ohooo, ni mimi kaka”
Alizungumza huku akiinyanyua mikono yake juu, huku mkononi akiwa ameshika gazeti
“unataka nini?”
Nilimuuliza kwa sauti ya ukali
“ka..Ka kuna hili gazeti hapa.....”
“la nini?”
“kukuuu.....”
“nitolee kigugumizi chako, kabla sijakuua”
Mlinzi akaanza kutoka ndani
“wee kaka samahni, hembu hilo gazeti”
Dorecy akanyanyuka na kwenda kulichukua gazeti, akalifungua na kuanza kulisoma huku akipiga hatua za taratibu akirudi sehemu ambayo alikuwa amekaa.Akakaa sehemu yake, sikuwa na haja ya kulitazama gazeti lake.
“eddy”
Dorecy aliniita na kunifanya nimtazame, nikaikuta sura yake ikiwa imejaa mikunjano akionekana kuna habari iliyopelekea sura yake kuwa katika sura kama hii,akanyanyuka na kukaa kwenye sofa nililopo mimi.
“soma, hii habari”
Macho yangu yakatua kwenye maandishi meusi yaliyo andikwa kwa herufi kubwa zinazo onekana vizuri pasipo na shida yoyote
‘mtoto wa waziri wa afya (eddy godwin), anatafutwa na jeshi la polisi kwa mauaji ya kikatili ya mfanya biashara wa madini jijini arusha bwana derick lambart na mwili wa derick kuwa chakula cha mbwa wake’
Chini ya maandishi haya makubwa kuna picha yangu, ya mama na derick lambart zikiwa zimeambataishwa kwenye mstari mmoja
“eddy ni kweli?”
Dorecy alizungumza huku akinitazama machoni, sikumjibu zaidi ya kunyanyuka kwenye sofa, kabla sijamjibu dorecy nikasikia mlio wa gari ukisimama nje ya geti.Cha kwanza nikazima taa za sebleni na kufungua pazia kidogo la dirisha linalo tazama kwenye geti,nikawaona askari wawili wakizungumza na mlinzi huku wakionekana kulazimisha kuingia ndani kwa nguvu.
*****sory madam*****(52)
Dorecy akanyanyuka katika kochi alilo kaa na kunifwata nilipo simama,
“shiit, wamejuaje kama upo humu?”
“hata mimi sifahamu”
“so, inakuwaje?”
“tuwauoe?”
“eddy, usiongeze dhambi nyingine juu ya kuua.Uliyo yafanya yanatosha kwa sasa”
“sasa wewe unanishaurije?”
“ngoja nikuonyeshe”
Dorecy, akaanza kuvua nguo moja baada ya nyingine hadi akabakiwa na nguo za ndani(sidiria na chupi), na nguo zake akazificha nyuma ya masofa.Mlinzi alishindwa kuwazuia askari hao kuingia, dorecy akaniomba nijifiche nyuma ya mlango wa kuingilia.Nikafanya kama alivo niagiza dorecy, maaskari wakaanza kugonga mlango taratibiu.Dorecy akaisogelaa swichi ya kuwasha taa za sebleni, akaiwasha na kwenda kusimama ulipo mlango
“fungua”
Nilizungumza kwa sauti ya chini sana, huku nikiwa nimeishika bastola yangu vizuri mikononi mwangu.Dorecy akafungua mlango akiwa katika hali ya nguo zake za ndani, zilizo ufanya mwili wake kuonekana vizuri na kuwa kivutio kizuri mbele ya wanaume marijali.
“habai zenu maafande?”
Dorecy aliwasalimia, ila salamu yake haikujibiwa kwa sekunde kdhaa, kwa kupitia uwazi wa mlango nikwashuhudia askari wakiwa wamemtumbulia mimacho dorecy
“aha....Aahaa salama tu”
“mmmm, labda niwasaidie nini?”
“ahaaa”
Askari walibabaika, hawakujua hata wajibu kitu gani
“karibuni ndani”
“haya....Haya”
Mmoja alizungumza huku akijilamba lamba mdomo wake, wakaingia ndani na dorecy akaurudishia mlango, na kunnifanya niweze kuonekana vizuri na askari walio ingia ndani.Hawakuweza kufanya kitu chochote kwa sababu, nimeshika bastola, huku nikiwa sina masihara kabisa na kitu ambacho ninakifanya
“nyoosheni mikono yenu juu”
Niliwaamrisha, wakatii huku wakitetemeka, dorecy akaanza kuwapapasa na kuwachomoa bastola zao walizo zificha kwenye miguu yeo,dorecy akawavua mikanda yao ya suruali
“unawafanyaje?”
“subiri uone”
Dorecy akaichukua mikanda yao ya suruali, nikawaamrisha waende kukaa kwenye masofa
“nyinyi, mumekuja kufanya nini?”
Niliwauliza kwa sauti ya ukali
“tu..Lik..Uku..Ja, kukutaf...Uta wewe”
Mmoja alizungumza huku akibabaika sana,
“nani amewatuma?”
Dorecy alizungumza
“eheee?”
“nani amewatuma, au swali langu ni gumu kulijibu?”
Dorecy alizungumza, huku akiizungusha bastola ya mmoja wa polisi
“ni..Ni....Nimzee dodwin”
“nilijua, tuu”
Dorecy alizungumza, huku akinitazama usoni.
“simameni kwanza”
Niliwaamrisha na wakasimama, nikawaamrisha tena kuvua nguo zao, wakatii bila ya ubishi.Wakabakiwa na kaptula zao za ndani, nikaamrisha kulala chini, nikachukua pingu zao na kuwafunga mikononi, walio irudisha nyuma, dorecy akachukua mikanda yao na kuwafunga miguuni kisha akaikutanisha miguu na mikono kwa mamoja na kuwafunga,
“sasa ninahitai munijibu swali moja baada ya jengine?”
“munaweza kuniambia ni wapi alipo mama yangu?”
Wakaa kimya, hakuna aliye nijibu hata mmoja.
“ninarudia tena na tena kuwauliza hili swali.Ni wapi alipo mama yangu?”
“si hatujuii”
“hamujui eheee?”
“ndio”
“waangalie hawa”
Nikaondoka na kuingia jikoni, nikachukua ndoo ndogo na kuijaza maji mengi, kisha nikachukua fimbo moja ya fagio la kusimama na kurudi navyo sebleni, nikaanza kuwanyunyizia maji ya makalio
“sasa, hapo utawachapaje?”
Dorecy aliniuliza
“wafungue huo mkanda nilio wafunga na mikono”
Dorecy alizungumza huku akiendelea kuwanyooshea bastola aliyo ishika, nikamfungua mmoja mkanda ulio fungwa na pingu yake, nilipo hakikisha nimeiachanisha miguu na mikono, nikamvuta pembeni na kumwagia maji ya makalio.Nikaivunja fimbo, ya fagio kugawanyika katika vipende viwili nilivyo viona vinatosha
“ninakuuliza ni wapi alipo mama yangu?”
“sijuii mimi?”
Nikamchapa fimbo nne za nguvu kwenye makali, yenye bukta iliyo lowa maji mengi.Jamaa akawa amejikaza makalio yeka, nikamtandika fimbo nyingine nne kwenye mapaja yake, kidogo akaanza kutoa miguno ya maumivu
“sijuii mimi?”
“utajua tuu”
Nikaanza kumchapa fimbo zisizo na idadi maalumu ambazo ninajua ni lazima zitampa maumivu ya kusema ni wapi alipo mama yangu, japo mzee godwin ameniambia kuwa mama amesha fariki, ila sikutaka kuamini kama ni kweli, hadi niuone mwili wa mama yangu ndio nitaamini kwambe amefariki dunia.Fimbo zisizo na idadi nikazidi kuzishusha kwenye makalio ya ya polisi huyu, na akazidi kumwaga machozi ya maumivu
“huwa mimi ninawashangaa sana nyinyi, kazi yenu ni kulinda mali za raia.Huku kwenye matatizo mengine kama haya munafwata nini?”
“sijuii,”
“mimi leo nina wahakikishia kuwa mutajua”
Nikaendelea kumatindika fimbo zisizo na idadi hadi, sehemu ambazo nilizichapa zikaanza kuvimba na kuweka maalama ya fimbo
“eddy, huyo kakataa kusema bwana, hamishia zoezi kwa huyu”
Dorecy alizungumza, nikamuacha ninaye mchapa na kumfwata mwenzake, nikamuandaa kama nilivyo muandaa mwenzake kabla sijamchapa dorecy akanizuia
“lete hiyo fimbo”
Nikamabidhi dorecy fimbo moja, akamuweka askari vizuri, kwa nguvu zake zote akaishisha vimbo kwenye makalio ya askari na kumfanya atoe ukelele huku akiliita jina la mama yake.Dorecy akashusha fimbo nyingine mbili za nguvu na kumzidisha askari kutoa kelele
“nasemaa, nasemaa”
“sema sasa”
Dorecy alizungumza, huku akimwagikwa na jasho jingi,
“yupo, kwenye mikono ya mzee godwin”
“hilo tunalijua, tunacho kitaka sisi ni kujus ni sehemu gani ambayo yeye yupo?”
“kule kwenye ule msitu”
Dorecy akanitazama usoni
“napajua”
Dorecy alizungumza, akamtandika fimbo nyingine ya makalio na kuzidi kumliza askari huyu anaye onyesha bado ni kijana sana.
“hawa dawa yao ni kuwafungia stoo”
Nilizungumza, huku nikikiondoa kindoo cha maji na kukipeleka jikoni, nikarudi sebleni na kumkuta dorecy akimalizia kuvaa nguo zake.Nikatoka nje ya nyumba na kumfwata mlinzi getini
“hawa wehu wamekuja na nini?”
“kina nani?”
“hawa askari?”
“na gari yao ndogo, ipo hapo nje”
“sasa ilikuwaje ukaacha waingie ndani?”
“walinionyesha vitambulisho vyao”
Nikatoka nje ya geti na kukuta gari aina ya corola ikiwa imesimama nje ya geti, nikarudi ndani na kuwaamrisha wanipe funguo za gari lao,
“ipo kwenye hiyo suruali yangu”
Nikaiokota funguo ya askari aliyechapwa na dorecy, nikatoka nje na kumuomba mlizi aniungulie geti, nikaingia ndani ya gari lao walilo jia na kuliingiza ndani ya geti na kwenda kulisimamisha nyuma ya yumba yetu pembezoni mwa ‘swimming pool’.Nikamuita mlinzi na kumuomba asaidiane na mimi kuwabeba askari hawa
“tunawapeleka wapi bosi?”
“nyuma ya nyumba huko”
“ila kablwa hatujawapeleka, wavue viatu vyao”
Mlinzi akaanza kuwavua viatu kisha, tukamuanza yule niliye mchapa, kumbeba.Nikaingia kwenye nyumba ya nyuma, kwenye chumba ambacho chini kina handaki.Hata mlinzi mwenyewe akashangaa kwani hakuamini kama chumba hichi kina handaki, lenye ukumbi mkubwa.Tukamuingiza askari wa kwanza na kumfwata askari wa pili na kumuingiza, huku wote wakiwa wamefungwa miguu na mikono yao
“hakikisha, hawatoki.Pia hakikisha unawapatia chakula mchana na jioni”
“sawa bosi nimekuelewa”
“pia hakikisha haingii, mtu yoyote akidai kuwa yeye ni askari au mpelelezi”
“sawa”
Nikaachana na mlinzi yeye akarudi zake getini na mimi nikaingia ndani, nikamkuta dorecy akimwalizia kuyafuta maji yaliyo tapakaa chini kwa tambaa.
“eddy, uhisi njaa”
“kwa mbali ninajihisi njaa”
“kwenye friji, jikoni niliona nyama na soseji ngoja nipiki chakula”
“powa, upendavyo wewe, mimi ninaingia chumbani huku juu”
“sawa”
Nikaingia ndani kwangu, mazingira ya chumba changu kwa jinsi nilivyo yaacha, hapakuwa na tofauti sana.Nikaingia nikainama chini ya mvungu wa kitanda changu na kulikuta begi lenye madini, niliyo yatoa kwenye handaki.Nikakifungua na kukuta madini yapo kama yalivyo.Nikakirudisha kibegi chini ya mvungu, nikaingia bafuni na kuvua nguo zangu zote, nikasimama mbele ya kioo kikubwa kiichomo humu ndani ya bafu langu
Mwili wangu mzima umejaa, majeraha mengi, yaliyo tokana na mateso niliyo pitia siku chache za nyuma, nikajikuta machozi yakinimwagika kwani hata ule uzuri ambao mungu aliniumba nao umetoweka kwa kiasi fulani.
“kwa nini mimi?”
Nilijiuliza swali huki nikitokwa na machozi,
“nimekuwa, hivi na roho ya kinyama”
“gereza au kifo ndio mwisho wangu”
Nilizungumza huku nikiendea kumwagikwa na machozi mengi, malengo yangu yote niliyo jiwekea kuja kuwa daktari bingwa nchini tanzania yametoweka kabisa, hapa ndipo nikaanza kuamini kwamba pesa haitimizi malengo ya mtu, kwani tangu nimezaliwa sikuwahi kuishi maisha ya shida kwani baba anapesa na mama ndio tajiri kupindukia, ila kwa sasa ndio wamekuwa maadui sana.Sikujua baba yangu wa damu anaendeleaje, kwani sikupata hata muda wa kukaa na mama na kumuuliza kuhusiana na baba yangu aliyepo afrika kusini
Macho yangu, nikaendela kuyakaza kwenye kioo, nikiitazama sura yangu, iliyo jaa dhambi na ukatili ulio mkubwa.Sikupenda kuwa hivi, ila matatizo yakanibidi mimi kuwa hivi
“mungu, nisamehe, mimi ni mwenye dhambi tena dhambi nyingi.Ila ninaomba nimuue mzee godwin tuu.Ili nikifa nife kwa amani”
Nilijikuta nikizungumza maneno haya ambayo sikujua ni kwanini nimeyazungumza, tena kwa sauti ya juu.Nikafungua bomba la maji ya mvua na kuasimama kwa muda chini ya maji haya yanayoendelea kutiririka mwilini mwangu.Mwili wangu umejawa na nongo nyingi sana kwani hata maji ambayo yanaingia kwenye kishimo kidogo cha hapa bafuni yanaonyesha jinsi mwili wangu ulivyo jaa uchafu.Nikaoga na kurudia kupiga mapovu manne ndipo, hali ya uchafu ikaondoka mwilini mwangu.Hata rangi halisi ya mwili wangu ikarejea.
Nikamaliza na kurudi chumbani kwangu, nikiwa ninatafuta ni wapi lilipo taulo langu lipo, mlango wa chumbani kwangu ukafunguliwa na dorecy
“ahaaa sory eddy...!!”
“ahaaa bila samahani”
Nilizungumza huku mikono yangu nikiwa nimeiziba kweye sehemu zangu za siri
“ahaaa sory eddy...!!”
“ahaaa bila samahani”
Nilizungumza huku mikono yangu nikiwa nimeiziba kweye sehemu zangu za siri
“chakula tayari kule”
“sawa, ninakuja”
Dorecy akatoka, nikavaa pensi, nikaelekea sebleni na kumkuta akiwa ananisubiria kwenye meza ya chakula
“mbona, hukula chakula?”
“nilikuwa ninakusubiria”
“ohoo, ungeanza tuu”
“hapana, itakuwa sio tabia nzuri sana kwa yule umpendaye”
“kweli”
“ehee, sisi kwetu hatujafundishwa hivyo”
“sawa”
Nikakaa kwenye kiti, dorecy akanitengea chakula changu na taratibu tukaanza kula,
“kipindi nikiwa, sunday school tulikuwa tunafundishwaga kusali kabla ya kula”
Nilizungumza
“mulikuwa munafundishwaje?”
“tulikuwa tunaomba, ohh loard our father, bleas this food for this day, welcome dorecy”(.....Baba yetu wa mbinguni, bariki hiki chakula cha leo, karibu dorecy)
“hahaaa, eddy.Sasa mbona leo hujasali?”
“ahaa weee acha tuu”
Tukaendelea kula huku nikitazamana mara kwa mara na dorecy, nikanyanyuka na kuzunguka meza hadi alipo kaa dorecy, nikasimama nyuma yake, mikono yangu nikaiweka mabegani mwake.Nikainama taratibu na kumbusu shavuni
“dorecy”
“mmmm”
“ninakupenda”
Dorecy hakunijibu chochote, taratibu nikaanya kuinyonya shingo yake na kumfanya aanze kujichezesha chezesha kwa hisia.Nikamnyanyua kwenye kiti na kuanza kuinyonya midomo yake, huku nikaanza kumvua nguo moja baada ya nyingine.Tukajikuta tunazama kwenye dimbwi kubwa la mapenzi huku kila mmoja akijitahidi kumpa mwenzake raha ambayo anastahili kuipata kwenye dimbwi la mapenzi.
Tukatumia kama dakika thelathini na nano kuburudishana hadi tunamaliza, tukavikuta vyombo vyote vipo chini huku sisi tukiwa juu ya meza tukitoa pumzi nyingi
Nikambeba dorecy hadi chumbani kwangu, sote tukaingia bafuni, tukaoga na kurudi chumbani na kujitupa kitandani
“eddy, unampango gani juu ya mama”
“nataka nikamkomboe, siamini kama amekufa?”
Nikambeba dorecy hadi chumbani kwangu, sote tukaingia bafuni, tukaoga na kurudi chumbani na kujitupa kitandani
“eddy, unampango gani juu ya mama”
“nataka nikamkomboe, siamini kama amekufa?”
“japo sipendi kujua kilicho tokea kwenye familia yako hadi kukafikia huku, ila nakuhaidi tutashirikiana kudfa na kupona”
“nitashukuru kwa hilo”
“kingine, itabidi unyoe nywele zako....”
“ili”
“uvae zile nguo za askari, la sivyo utakamatwa kirahisi”
“etii ehee?”
“hapo hakuna cha etii, inabidi iwe hivyo”
“sawa, tutafanya asubuhi”
Kutokana na kuchoka kila mmoja akajilaza na usingizi mwingi ukanipitia,nikawa wa kwanza kuamka nikaingia bafuni na kuoga, nikamuamsha dorecy naye akaingia bafuni na kuoga.Nikachukua mashine ya umeme ya kunyolea na kumkabidhi dorecy, akaanza kuninyoa nywele zangu zote na kunifanya nibadilike sana.
“dory, nataka twende bank mara moja”
“tukafanyaje?’
“kuna ishu nakwenda kuiuzia benki”
“benki gani?”
“cnb”
“sawa, ila tumia hizo nguo za polisi”
“powa”
Nikavaa, nguo za polisi,aliye chapwa na dorecy, zikanitosha vizuri, nikazunguka lilipo gari la polisi nilipo liacha na kuchukua kofia moja ambayo ipo ndani ya gari, nikarudi sebleni na kuvaa viatu vya kiaskari
“kama polisi kweli vile”
“umeona eheee”
“eddy una picha ndogo”
“ya nini?”
“kuna kitambulisho nataka nifoji hapa”
Nikaingia chumbani kwangu na kutoa picha ndogo ya na kukabidhi dorecy, akaanza kazi ya kufoji kitambulisho kimoja cha polisi.Nikachukua bastola moja na kuichomeka kwenye viatu na kuifunika na sruali, nikachukua bastola nyingine na kuichomeka kiunoni.Nikavaa jaketi la kuzuia risasi, dorecy naye akawa amemaliza kuvaa nguo zake, nikaingia ndani kwangu na kuchukua begi lenye madini, nikaingia chumbani kwa mama na kuchukua funguo ya gari lake aina ya vx v8 na kutoka navyo nje.
“una endesha, niendeshe”
Nilimuuliza dorecy
“wewe endesha, huu mji wenu mimi siuelewi kabisa”
Tukaingia ndani ya gari na kuondoka nimasisitizia mlinzi asiruhusu mtu kuingia ndani ya nyumba yetu.
“nimemaliza kukitengeneza kitambulisho chako”
Dorecy akanikabidhi kitambulisho changu, chenye jina la edward kilonzo, ni jina la askari aliye tandikwa bakora na dorecy.Tukafika benk, kabla sijashuka dorecy akanibusu shavuni.
“ninakupenda eddy wangu”
“na mimi pia”
“kwani humo ndani ya begi kuna nini?”
“nitakuambia nikirudi”
Nikatazama mazingira yote ya benki na kuona yapo salama, nikashuka kwenye gari huku nikiwa na kibegi na kuanza kupiga hatua za kuelekea ulipo mlango wa benki, huku amcho yangu yakiwa makini sana.Nikafika hadi kwa muhudumu pasipo askari wa mlangoni kunigundua
“dada habari yako?”
“salama”
“meneja nitamuona wapi?”
“una mawasiliano naye?’
“hapana ila, ninaujumbe kutoka kwa bosi wangu.Kuna huu mzigo nimeagizwa nimkabidhi yeye”
“unalijua jina la meneja?”
“ndio, anaitwa bwana turma”
“basi twende, nikupeleke ofisini kwake”
“asante”
Tukaingia kwenye lifti na kupandisha gorofa ya kwanza, nikaingia ofisini mwa bwana turma ambaye ni rafiki mkubwa wa mama, na mimi ananifahamu vizuri sana.Kwa bahati nzuri nikamkuta hana mtu anaye zungumza naye
“meneja unamgeni”
“muambie aingie”
Muhudumu akaniruhusu kuingia ndani ya ofisi, kisha yeye akaondoka, nikaivua kofia yangu na kumfanya bwana turma kutabasamu baada ya kuniona
“eddy, umekuwa askari?”
Aliniuliza huku akicheka
“hapana mjomba”
“ila?”
“ahaa vijimambo tu,”
“ila ninasikia unatafutwa na polisi”
“ndio, ila mjomba ninaomba msaada wako”
“msaada gani?”
“kuna haya madini, yanadhamani kubwa sana.Ninaomba niwauzie nyinyi kama benki na pesa yangu muiweke humu ndani, ipo siku mungu akibariki, mimi au mwangu anaweza akasaidiwa na hiyo pesa”
Bwana turma akaniangalia kwa macho ya umakini, akaniomba nimuonyeshe hayo madini.Nikamfungulia begi na kumuwekea, kibegi juu ya meza.Akabaki akishangaa
“umeyatoa wapi?”
“hii ni mali ya mama, ninakuomba sana uniwekee”
“wewe ulikuwa unayauza kwa kiasi gani?”
“bilioni moja na nusu shilingi”
“mbona nyingi sana”
“hata haya madini, yanadhamani kubwa sana.Nikisema niuze kwa masonara si chini ya bilioni tano”
“sawa mjomba nimekuelewa, ngoja nikawaite wahasibu na wanasheria wa benki tuwez kufanya biashara”
“sawa mjomba”
Bwana turma akatoka nje ya ofisi yake na kuniacha nikiwa ndani, nikakaa zaidi ya dakika kumi na tano, sikumuona bwana turma kutokea, nikaanza kupata wasiwasi, labda amekwenda kuwaita askari.Nikanyanyuka na kukifunga kibegi changu, nikatizama kwenye kioo cha computer yake, iliyopo juu ya meza yake, kilicho gawanyika katika vipande sita vya picha za video za kamera za ulinzi na kuona gari aina ya rangerover ikisimama kwa kasi nje ya benki na wakashuka wasichana watano walio valia mavazi meusi huku wakiwa na bunduki mikonini mwao.Wakanza kuwashambulia askari huku walili wakiingia ndani ya benki na kuanza kuwashambulia askari na kuwaamrisha watu wote kulala chini.Nikamuona wakimuamrisha bwana turma kuingia kwenye chumba ambacho ndicho wanahifadhia pesa...
Itaendelea....