.
ILIPOISHIA:
"edward sambo ana..",Yule mtu
alitaka kuendelea kuongea ila
alishindwa, mara ukasika mlio wa bunduki ulioambatana na
risasi iliyoishia kichwani mwa yule mtu na akapoteza uhai,
Jack na wenzake waliponyanyua
nyuso zao, wakawaona vijana wanne
waliobeba bunduki wakielekea
upande wao....
ENDELEA...
Wakakurupuka na kuanza kukimbia
kumfuata mwenyeji wao anapoelekea,
ukasikika mlio wa risasi tena, Jack
akashuhudia mwili wa Mapesa
ukienda chini kama gunia la pamba
lililotupwa kutoka juu ya roli, Jack
akajua anafuata yeye, maana yeye
alikuwa nyuma mwenyeji wao mbele,
akakunja kona ghafla na kuacha
kufuata njia, akawa anaelekea
vichakani huku risasi mfululizo
zikimsindikiza bila kumdhuru,
akazidi kukimbia tena na tena
mpaka alipotokezea sehemu ambapo
aliona kuna nyumba nyingi nyingi za
udongo, lakini alizidi kukimbia huku
akipiga kelele za kutaka msaada,
ndipo vijana wa pale kijijini
wakamshika na kumuweka chini,
"vipi, una tatizo gani?",Kijana mmoja
alimuuliza lkn Jack hakujibu, alikuwa
akihema haraka haraka sana,
"nyie huyu si Jack yule
muigizaji",Msichana aliekuwa
miongoni mwa watu waliojaa
kumzunguka Jack aliwaambia wenzie,
"ah kumbe mizinguo tu, usikute
ametujaza hapa kumbe
anaigiza",Teja mmoja aliekuwa
katikati ya kundi aliongea huku
akimalizia na tusi la nguoni.
"samahanini, hapa ni wapi?",Jack
aliamua kuongea baada ya kuvuta
pumzi muda mrefu,
"hapa dumila, morogoro. Nini
kimekusibu?",Kijana mmoja alimjibu
kisha akamtupia swali,
"nilikuwa napita hapo msituni,
nikakutana na vibaka",Jack aliongea
kwa sauti ya kawaida iliyosikika
vizuri,
"hapo mbona kawaida, ulikuwa peke
yako?",Wale vijana walimuuliza,
"ndio, kwani vipi?",Jack alijibu kwa
kubabaika,
"tulijua mlikuwa wengi, tulitaka
tukawatafute wenzio",Kijana mmoja
alitoa kauli iliyoungwa mkøno na
wenzake,
"mna silaha au?",Jack aliuliza,
"tuna mapanga na marungu",Vijana
walijibu kwa kujiamini,
"bunduki na rungu wapi na
wapi?",Jack aliongea kimoyo moyo
kisha akaulizia mahali ambapo
anaweza kupa usafiri wa kumfikisha
Dar ili akatoe taharifa, maana hata
simu yake aliidondosha katika
kuwakimbia wauaji kule porini.
Alifanikiwa kupata basi muda huo wa
saa moja jioni lilimpeleka mpaka
ubungo, kisha akatafuta gari
iliyompeleka nyumbani kwake.
"vipi wewe!?",Sangu alimshangaa
Jack baada ya kumfungulia,
"kwani vipi?",Jack nae aliuliza huku
akiingia ndani,
"hukuondoka hivyo wewe, au ulikua
unafanya shooting msituni?",Sangu
aliendelea kumuuliza maswali ya
mshangao,
"bwana niache",Jack aliongea kwa
ukali huku akiingia chumbani kwake.
Baada ya saa, Jack alikuwa
amemaliza kuoga na alikuwa
sebuleni akimuelezea yaliyowakuta,
"kwa hiyo mapesa amekufa?",Sangu
aliuliza kwa masikitiko,
"nani kasema kafa, mi nimekwambia
amepigwa risasi, so sijajua amekufa
au lah..",Jack alijibu huku akionesha
dhahiri hakufurahishwa na swali la
Sangu,
"polisi si umewapa taharifa?",Sangu
aliuliza,
"mi sijawapa, ila yule jamaa
tuliyekuwa nae msituni atakuwa
amewapa",Jack aliongea kwa
kujiamini,
"una uhakika gani, kama nae aliuliwa
je?",Sangu aliuliza huku akimshangaa
Jack,
"mh, ila kweli, ngoja tupate chakula
kisha twende tukatoe taharifa",Jack
alionesha kukubaliana na Sangu,
"ungeanza kuwapigia simu
kwanza",Sangu alimpa ushauri Jack,
"si nimekuambia hata simu
nimepoteza, nipe simu yako
niwapigie",Jack alimuambia Sangu,
"limeingia kwenye maji, hata kuwaka
haiwaki",Sangu alijibu kivivu.
Wakati wanaendelea kula usiku huo
huku wakitazama TV ya taifa, macho
yalivutwa zaidi walipoona tangazo la
TV linaloonesha habari muhimu
zilizofika punde,
"msanii maarufu nchini, Jackson Mtei
almaarufu Jack, anatafutwa na polisi
kwa tuhuma za mauaji aliyofanya leo
jioni katika kijiji cha matombo jirani
na dumila, inadaiwa Jack amemuua
meneja wake bwana Juma Mapesa na
mpelelezi maarufu bwana Sadick
Jomo. Maaskari wanne waliokuwa
jirani wamemkamata mtu mmoja
ambae alikuwa na Jackson kipindi
anafanya mauaji hayo na huyo
bwana amekiri kuwa alishirikiana na
Jack kufanya uuaji huo. Jeshi la polisi
linaendelea kumtafuta Jack ambae
hajulikani halipo",Mtangazaji
alimaliza kutoa taharifa,
"mama yangu, nini hiki, au
nachezewa?",Jack aliongea huku
akishangaa,
"huyo mtu alioneshwa na kudai
kushirikiana na wewe kufanya mauaji
unamjua?",Sangu alimuuliza Jack,
"yule ndo alikuwa mwenyeji wetu
kule msituni",Jack alijibu huku
kakata tamaa,
"na hao polisi wanne waliooneshwa
unawajua? ",Sangu hakuchoka
kuuliza,
"wale ndo wamemuua huyo jamaa
alienipa memory card, na
Mapesa",Jack alijibu..
Wakiwa wanashauriana ni namna
gani watawaelewesha polisi, ilisikika
sauti ya mtu akibisha hodi mlango
wa mbele, Sangu akaenda kufungua,
"karibuni, niwasaidie nini?",Sangu
aliongea baada ya kufungua mlango,
kisha akatoa kichwa nje,
"sisi ni maafisa wa polisi, tunamtaka
Jack",Mmoja kati ya wale wapiga hodi
alijitambulisha,
"hayupo",Sangu alijibu huku akitaka
kufunga mlango, wale polisi
wakamsukuma, kisha wakaingia
ndani kwa fujo..
***ITAENDELEA***
ILIPOISHIA:
"edward sambo ana..",Yule mtu
alitaka kuendelea kuongea ila
alishindwa, mara ukasika mlio wa bunduki ulioambatana na
risasi iliyoishia kichwani mwa yule mtu na akapoteza uhai,
Jack na wenzake waliponyanyua
nyuso zao, wakawaona vijana wanne
waliobeba bunduki wakielekea
upande wao....
ENDELEA...
Wakakurupuka na kuanza kukimbia
kumfuata mwenyeji wao anapoelekea,
ukasikika mlio wa risasi tena, Jack
akashuhudia mwili wa Mapesa
ukienda chini kama gunia la pamba
lililotupwa kutoka juu ya roli, Jack
akajua anafuata yeye, maana yeye
alikuwa nyuma mwenyeji wao mbele,
akakunja kona ghafla na kuacha
kufuata njia, akawa anaelekea
vichakani huku risasi mfululizo
zikimsindikiza bila kumdhuru,
akazidi kukimbia tena na tena
mpaka alipotokezea sehemu ambapo
aliona kuna nyumba nyingi nyingi za
udongo, lakini alizidi kukimbia huku
akipiga kelele za kutaka msaada,
ndipo vijana wa pale kijijini
wakamshika na kumuweka chini,
"vipi, una tatizo gani?",Kijana mmoja
alimuuliza lkn Jack hakujibu, alikuwa
akihema haraka haraka sana,
"nyie huyu si Jack yule
muigizaji",Msichana aliekuwa
miongoni mwa watu waliojaa
kumzunguka Jack aliwaambia wenzie,
"ah kumbe mizinguo tu, usikute
ametujaza hapa kumbe
anaigiza",Teja mmoja aliekuwa
katikati ya kundi aliongea huku
akimalizia na tusi la nguoni.
"samahanini, hapa ni wapi?",Jack
aliamua kuongea baada ya kuvuta
pumzi muda mrefu,
"hapa dumila, morogoro. Nini
kimekusibu?",Kijana mmoja alimjibu
kisha akamtupia swali,
"nilikuwa napita hapo msituni,
nikakutana na vibaka",Jack aliongea
kwa sauti ya kawaida iliyosikika
vizuri,
"hapo mbona kawaida, ulikuwa peke
yako?",Wale vijana walimuuliza,
"ndio, kwani vipi?",Jack alijibu kwa
kubabaika,
"tulijua mlikuwa wengi, tulitaka
tukawatafute wenzio",Kijana mmoja
alitoa kauli iliyoungwa mkøno na
wenzake,
"mna silaha au?",Jack aliuliza,
"tuna mapanga na marungu",Vijana
walijibu kwa kujiamini,
"bunduki na rungu wapi na
wapi?",Jack aliongea kimoyo moyo
kisha akaulizia mahali ambapo
anaweza kupa usafiri wa kumfikisha
Dar ili akatoe taharifa, maana hata
simu yake aliidondosha katika
kuwakimbia wauaji kule porini.
Alifanikiwa kupata basi muda huo wa
saa moja jioni lilimpeleka mpaka
ubungo, kisha akatafuta gari
iliyompeleka nyumbani kwake.
"vipi wewe!?",Sangu alimshangaa
Jack baada ya kumfungulia,
"kwani vipi?",Jack nae aliuliza huku
akiingia ndani,
"hukuondoka hivyo wewe, au ulikua
unafanya shooting msituni?",Sangu
aliendelea kumuuliza maswali ya
mshangao,
"bwana niache",Jack aliongea kwa
ukali huku akiingia chumbani kwake.
Baada ya saa, Jack alikuwa
amemaliza kuoga na alikuwa
sebuleni akimuelezea yaliyowakuta,
"kwa hiyo mapesa amekufa?",Sangu
aliuliza kwa masikitiko,
"nani kasema kafa, mi nimekwambia
amepigwa risasi, so sijajua amekufa
au lah..",Jack alijibu huku akionesha
dhahiri hakufurahishwa na swali la
Sangu,
"polisi si umewapa taharifa?",Sangu
aliuliza,
"mi sijawapa, ila yule jamaa
tuliyekuwa nae msituni atakuwa
amewapa",Jack aliongea kwa
kujiamini,
"una uhakika gani, kama nae aliuliwa
je?",Sangu aliuliza huku akimshangaa
Jack,
"mh, ila kweli, ngoja tupate chakula
kisha twende tukatoe taharifa",Jack
alionesha kukubaliana na Sangu,
"ungeanza kuwapigia simu
kwanza",Sangu alimpa ushauri Jack,
"si nimekuambia hata simu
nimepoteza, nipe simu yako
niwapigie",Jack alimuambia Sangu,
"limeingia kwenye maji, hata kuwaka
haiwaki",Sangu alijibu kivivu.
Wakati wanaendelea kula usiku huo
huku wakitazama TV ya taifa, macho
yalivutwa zaidi walipoona tangazo la
TV linaloonesha habari muhimu
zilizofika punde,
"msanii maarufu nchini, Jackson Mtei
almaarufu Jack, anatafutwa na polisi
kwa tuhuma za mauaji aliyofanya leo
jioni katika kijiji cha matombo jirani
na dumila, inadaiwa Jack amemuua
meneja wake bwana Juma Mapesa na
mpelelezi maarufu bwana Sadick
Jomo. Maaskari wanne waliokuwa
jirani wamemkamata mtu mmoja
ambae alikuwa na Jackson kipindi
anafanya mauaji hayo na huyo
bwana amekiri kuwa alishirikiana na
Jack kufanya uuaji huo. Jeshi la polisi
linaendelea kumtafuta Jack ambae
hajulikani halipo",Mtangazaji
alimaliza kutoa taharifa,
"mama yangu, nini hiki, au
nachezewa?",Jack aliongea huku
akishangaa,
"huyo mtu alioneshwa na kudai
kushirikiana na wewe kufanya mauaji
unamjua?",Sangu alimuuliza Jack,
"yule ndo alikuwa mwenyeji wetu
kule msituni",Jack alijibu huku
kakata tamaa,
"na hao polisi wanne waliooneshwa
unawajua? ",Sangu hakuchoka
kuuliza,
"wale ndo wamemuua huyo jamaa
alienipa memory card, na
Mapesa",Jack alijibu..
Wakiwa wanashauriana ni namna
gani watawaelewesha polisi, ilisikika
sauti ya mtu akibisha hodi mlango
wa mbele, Sangu akaenda kufungua,
"karibuni, niwasaidie nini?",Sangu
aliongea baada ya kufungua mlango,
kisha akatoa kichwa nje,
"sisi ni maafisa wa polisi, tunamtaka
Jack",Mmoja kati ya wale wapiga hodi
alijitambulisha,
"hayupo",Sangu alijibu huku akitaka
kufunga mlango, wale polisi
wakamsukuma, kisha wakaingia
ndani kwa fujo..
***ITAENDELEA***