Msanii na mtayarishaji wa muziki kutoka nchini Afrika Kusini, Dj Maphorisa amefunguka urahisi anaoupata wakati anapofanya kazi na wasanii wa Tanzania.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Clouds E kupitia Clouds TV kuwa anapofanya kazi na wasanii wa Bongo kwake inamrahisishia kazi kwakuwa wamekuwa wakijituma lakini pia anakuwa anaufahamu zaidi muziki huo.

Mpaka sasa wasanii aliofanya nao ni pamoja na Lady Jaydee, Chege na Temba, Madee, Vanessa Mdee na Diamond.
Muimbaji huyo alifanikiwa kupata tuzo ya ‘Best Collaboration’ kwenye tozo za MTV MAMA zilizofanyika Jumamosi iliyopita kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome, Afrika Kusini.