Mti wa ukwaju. Majani yake hutumika katika tiba ya kuongeza maziwa kwa mama anaye nyonyesha. |
1.
Chukua majani
ya mti wa
Mvumbasi, unguza pamoja na majani ya
mti wa mnungunungu, halafu changanya na mafuta
ya taa lita
moja. Matumizi: Utakuwa unatumia kujichua kwenye miguu
kutwa mara tatu
kwa muda wa
siku thelathini. Utapata nafuu
kubwa sana.
Tunda la topetope;Mizizi ya mtopetope hutumika katika tiba ya kuondoa uvimbe kwenye kizazi. |
2.
TIBA YA KIKOHOZI: Tafuna majani
ya mti wa mbaazi. Mbali na
kutibu kikohozi, mti wa mbaazi, unatibu magonjwa mengine mengi.
Mfano, mizizi ya mti wa mmbaazi, husaidia kutibu
chango la kiume na
kusafisha kibofu cha mkojo.
3.
KUVIMBA
KWA TEZI LA SHINGO: Kama una sumbuliwa
na tatizo la
tezi kuvimba, chukua unga wa
Kamun Nyeusi, kisha
changanya na sega la
nyuki, halafu tumia kukanda kwenye tezi, kila
siku kwa muda wa mwezi
mmoja. Utapata mafanikio
makubwa sana.
4.
TIBA YA
MAUMIVU YA MGONGO, MIGUU, NYONGA NA KIFUA
KUPASUA:
Kama
una sumbuliwa na
maumivu ya mgongo, miguu, nyonga na
kifua kupasuka, fuata maelekezo
yafuatayo:
Chukua
mafuta ya nyonyo robo lita, mafuta ya Kamun
Nyeusi kiasi cha robo lita pamoja
na mafuta ya karafuu robo
lita , changanya pamoja halafu
uwe unatumia kujichua
sehemu yenye maumivu, kutwa mara tatu
kwa siku thelathini. Utapata nafuu
kubwa sana.
5.
TIBA YA KWIKWI : Kama
unasumbuliwa na kwikwi, fuata
maelekezo yafuatayo : Chukua majani ya
mwembe mkavu, pekecha kisha
mpe mgonjwa atumie
kuvuta kama sigara
halafu awe anameza moshi. Tatizo
la kwikwi litaisha.
6.
Tatizo La
Kukojoa Kitandani ; Kama una
tatizo la kukojoa
kitandani, tumia mizizi ya
mbaazi kwa kuchemsha, na
kunywa maji yake
kutwa mara mbili kwa
siku, kwa muda wa siku kumi na
nne.
7.
Tatizo la
uvimbe kwenye kizazi :
Kama una tatizo
la uvimbe kwenye
kizazi, chukua mizizi ya
mtopetope, tumia kwa kuchemsha
na kisha kunywa maji
yake, mara tatu kutwa
kwa siku thelathini.
8.
Vidonda vya
koo : Kama una tatizo la vidonda vya
koo, chukua maji ya uvuguvugu kiasi cha nusu
lita, kisha kamulia ndimu
tatu fresh, halafu tumia kusukutulia. Utafanya hivyo
mpaka, utakapo pata nafuu.
9.
Malaria sugu : Kama
una malaria sugu, chukua maji
ya dafu moja, weka
kwenye chombo kisafi, kisha kamulia
ndimu saba, halafu tumia
kunywa. Fanya hivyo mara
mbili kwa siku, asubuhi
na jioni kwa
siku tatu hadi saba. Hakika
utapata matokeo mazuri
sana.
10.
Tiba ya tatizo
la kutoa harufu mbaya kinywani, sehemu za
siri, kikwapa na jasho lenye
harufu mbaya : Chukua maji
yaliyo lowekewa mchele
kiasi cha lita
moja, kisha tumia kunawia
sehemu husika na
kusukutulia mdomo. Utafanya hivyo mara
tatu kwa siku
hadi utakapo ridhika
na matokeo unayo
yahitaji.
11.
Kwa
wakina mama; Jinsi yakuzuia
uchungu wamimba,maumivu yakiuno, maumivu wakati wahedhi, na damu itokayo bila
mpangilio wasiku maalumu,Chukua majani ya mbigili yatwange halafu changanya
navijiko vitatu vikubwa vya unga wa mti unaitwa msonobali kisha tumia kunywa glasi 1 yenye ujazo
wa milimita mia
mbili na hamsini,
kutwa mara tatu hadi hali yako itakapokua nzuri
12.
Tiba Ya Vidonda Vya
Tumbo,Kisukari pamoja na
Typhoid:
Chukua mizizi ya mti wa msongati pamoja
na majani ya mkalatusi vitwange kwa pamoja kisha
chemsha kwenye maji
lita moja, halafu tumia kunywa glasi moja ya robo
lita, mara tatu kwa siku
kwa siku thelathini.
13.
Tiba Ya Tatizo
La Kukosa Hamu
Ya Tendo La Ndoa
Kwa Wanawake : Kama wewe
ni mwanamke unaye
sumbuliwa na tatizo
la kukosa hamu ya
tendo la ndoa,
unaweza kutibu tatizo
lako kwa kutumia
vyakula mbalimbali kama
ifuatavyo :
i.
JUISI YA
MIWA : Tumia kunywa
nusu lita hadi lita
moja ya juisi
ya miwa, mara tatu
kwa siku asubuhi, mchana na
jioni kwa siku
thelathini. Utapata matokeo mazuri. Mbali
na kuwasaidia akina
mama wenye tatizo
la kukosa hamu
ya tendo la
ndoa, juisi ya miwa
ina faida nyingine
nyingi kitabibu. Moja kati ya
faida kubwa za
juisi ya miwa, ni
uwezo wake mkubwa
wa kusafisha figo. Hivyo
hata wanaume wanashauriwa
kutumia juisi ya
miwa au miwa
kwa wingi,kwa sababu
inasaidia kusafisha figo, na
figo ni moja
kati ya ogani
muhimu sana katika
mfumo wa nguvu za
kiume.
ii.
MBEGU ZA FENESI :
Chukua mbegu za fenesi
kiasi cha robo kilo,
kisha chemsha na
maji lita mbili, halafu tumia
kula pamoja na
supu yake. Utafanya hivyo mara
tatu kwa siku kwa
muda wa siku
thelathini. Hakika utapata matokeo
mazuri sana. Unaweza
pia kuzisaga na
kutumia unga wake, kwa
kuchemsha na kunywa, kwa kufuata
utaratibu huo hapo
juu.
iii.
KOROSHO : Tumia kula
korosho pakti moja
yenye ujazo wa robo
kilo, mara tatu kwa siku, asubuhi, mchana na
jioni kwa siku
thelathini. Yaani asubuhi,
tumia robo kilo, mchana robo
kilo na jioni
robo kilo kwa siku thelathini. Utapata matokeo
mazuri.
iv.
MIHOGO MIBICHI : Tumia kutafuna
walau vipande vitatu
vya mihogo mibichi
kwa siku, kwa muda wa
siku thelathini. Yaani asubuhi
utumie kipande kimoja
kikubwa,mchana kipande
kimoja kikubwa na
usiku, utumie kipande kimoja
kikubwa.
14.
TIBA ASILIA YA TATIZO
KIFUA KISICHO PONA KWA WATOTO WADOGO
WALIO KUNYWA UCHAFU WAKATI WA KUZALIWA, PUMU, KIFUA KISICHO PONA KWA WATU
WAZIMA,KICHOMI,KUWASHWA MWILI NA KUPALIWA WAKATI UMELALA USINGIZINI
Tiba Yake, chukua majani ya
mpera kiasi cha kama viganja
vinne, yaponde pamoja na magome
ya muembe kiasi cha viganja
vinne, na tunda la
koma manga, twanga vyote kwa
pamoja ( Yani majani ya
mpera, magome ya muembe na tunda moja
la komamanga ).
Ukisha maliza
kutwanga, changanya na maji
lita mbili halafu chemsha
pamoja na lita moja ya
asali mbichi ya nyuki
wadogo.
Chemsha hadi
itokote, halafu ipua dawa
yako.
Matumizi
: Kwa mtoto mdogo mwenye
umri wa kati ya mwaka
mmoja na miaka mitano, tumia
kumpa kijiko kimoja kikubwa
mara mbili kwa siku, asubuhi
na jioni n kwa
siku saba.
Na kwa mtu mzima, tumia kunywa
vijiko vikubwa viwili mara
mbili kwa siku asubuhi na
jioni, kwa siku ishirini na
moja
15.
KUJITIBU TATIZO LA MTOTO
WA JICHO : Kujitibu mtoto
wa jicho, tumia kunyunyizia
jichoni matone mawili ya utomvu
wa toto la ndizi. Fanya hivyo
mara tatu kwa
siku, asubuhi, mchana na jioni kwa
siku thelathini. Utapata matokeo mazuri.
Mbali na
kutibu tatizo la mtoto
wa jicho, toto la ndizi,
likichanganywa kitaalamu na
wine ya mnazi ( Palm wine ) au mnazi, husaidia
kutibu tatizo la
kidole tumbo au
appendix.
16.
TIBA ASILIA YA
KUPUNGUZA GESI TUMBONI
Kuondoa gesi tumboni, kwa kutumia
tiba asilia, chukua juisi ya
kitunguu maji kiasi cha glasi moja yenye
ujazo wa milimita
mia mbili na hamsini,kisha
changanya na asali mbichi kijiko
kimoja koroga halafu tumia
kunywa .
Utafanya hivyo mara tatu kwa siku kwa muda
wa siku kumi
na nne.
AU chukua
kipande kimoja cha
tangawizi,kiponde ponde
kisha chemsha kwenye nusu lita ya maji pamoja
na kijiko kimoja kikubwa cha
asali mbichi ya
nyuki wadogo, halafu tumia
kunywa kutwa mara
mbili kwa siku
ishirini na moja.
AU ; Chukua asali mbichi
ya nyuki wadogo
kiasi cha robo
lita, changanya na vijiko
vitatu vikubwa vya
unga wa Kamun nyeusi,kisha chemsha pamoja
kwenye maji lita
moja.Halafu tumia kula
vijiko vikubwa vitatu
kutwa mara tatu kwa
siku ishirini na
moja.
17.
TIBA YA PUMU : Chukua magadi vijiko vikubwa vitatu, saga
upate unga wake, kisha changanya
na samli ya n’gombe vijiko 21
vikubwa na asali vijiko 30 vikubwa. Matumizi : Tumia kula
vijiko vikubwa vitatu
asubuhi, vitatu jioni na vitatu
usiku kwa muda wa
siku thelathini. Utapata
nafuu kubwa sana.
18.
TIBA ASILIA YA
KIHARUSI NA KIFAFA :
Chukua mizizi mitatu
ya mti wa
ukwaju, mizizi mitatu ya
mti wa mkungu, mizizi mitatu
ya mpapai, pamoja na mizizi
mitatu ya mti wa
ufwambo. Iponde ponde
yote kisha chemsha
kwa pamoja kwenye
maji ya lita tatu
hadi yachemke. Tumia kumpa
mgonjwa glasi moja, kutwa
mara tatu kwa siku
thelathini. Mgonjwa wako atapata
nafuu kubwa sana.
19.
TIBA ASILIA YA FANGASI ZA
KWENYE DAMU, UKURUTU, UPELE, MCHAFUKO
WA DAMU, PAMOJA NA KUWASHWA KWA MWILI.
Chemsha robo
kilo ya majani
ya mti wa
mdimu kwenye maji kiasi cha lita
mbili. Maji yakisha tokota,
ipua chuja, halafu tumia
kunywa glasi mbili asubuhi, mbili mchana, mbili
jioni. Utafanya hivyo kwa
muda wa siku thelathini. Hakika
utapata nafuu kubwa
sana.
20.
TIBA ASILIA YA MARADHI YA FANGASI ZA MIGUU NA KUNUKA
MIGUU.
Twanga majani ya
mwarobaini robo kilo,
chemsha na maji lita
tano, kisha weka kwenye beseni
halafu loweka miguu
yako ndani ya beseni
kwa muda wa
lisaa limoja. Utafanya hivyo
kutwa mara mbili kwa muda siku
kumi na nne. Utapata
matokeo mazuri sana.
AU chukua majivu kiasi cha
robo kilo,changanya na robo lita ya
juisi ya ndimu, kisha
nyunyizia kwenye miguu, na ukae kwa lisaa
limoja. Utafanya hivyo mara mbili
kwa siku kwa siku
thelathini. Japo inauma
lakini ni tiba nzuri sana.
21. KUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAE NYONYESHA : Chukua majani ya mti wa ukwaju, kiasi cha nusu kilo, kisha
chemsha na maji lita tano. Tumia kunywa glasi tatu asubuhi, tatu
mchana, tatu jioni kwa muda wa siku saba. Hakika utapata matokeo
mazuri sana. Utakuwa unafanya hivyo kila mara utakapo hitaji
kuongeza maziwa.
MAKALA HAYA
YAMELETWA KWENU KWA
HISANI YA NEEMA HERBALIST & NUTRITIONAL FOODS
CLINIC. DUKA LA KUUZA
DAWA MBALIMBALI ZA
ASILI.
TUNAPATIKANA
UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM, JIRANI NA
SHULE YA MSINGI,UBUNGO
NATIONA HOUSING NYUMA YA
JENGO LA UBUNGO
PLAZA.
KWA MAHITAJI YAKO
YA DAWA MBALIMBALI ZA ASILI
ZINAZO TIBU MAGONJWA
NA MATATIZO MBALIMBALI
YA KIAFYA, WASILIANA NASI
KWA SIMU NAMBA 0766 53 83 84.
NA KWA
TAARIFA ZAIDI KUHUSU HUDUMA
ZETU, TEMBELEA KILA SIKU KATIKA
BLOGU YETU.
0 Comments
on