Rapper huyo ambaye ameshirikiana na muimbaji, Abela kuunda kundi hilo, ameiambia Djmwaki.com kuwa kabla ya kuunda kundi hilo walikaacha chini na kuangalia namna ambavyo wataweza kukabiliana na matatizo.
“Sisi tumejipanga kupambana na changamoto zote, mpaka kuja au kufikia maamuzi ya kuungana na kuanzisha kundi tayari tumeshasomana tabia, yaani sisi tuna mengi ambayo tuliyaangalia. Kwahiyo naweza sema tupo vizuri tunaomba Mungu atusimamie tu,”
Pia rapa huyo amesema muziki kwa sasa umebadilika na kuwafanya wasanii kuacha kutegemea show pekee.
“Kwa sasa ukifanya muziki mzuri utaona matunda ya muziki wako kwa sababu sasa hivi wasanii hatutegemei shows tu, watu wanapata deal kubwa za kupiga show za mkampuni, endorsement na mambo mengine. Kwahiyo mimi naona kuna mashavu mengi sana kwenye muziki kama ukiandaa kazi nzuri,”
0 Comments
on