Header Ads Widget

Justin Bieber Ataka muziki wake ukubalike kuliko yeye.



Pop staa Justin Bieber kutoka Canada amesema anataka muziki wake upewe heshima kama unavyopewa heshima muziki wa Adele na kwamba akiwa jukwaani mashabiki zake wanyamaze na kusikiliza muziki wake sio kumpigia kelele yeye.
Justin alishuka kwenye jukwa la show yake jumapili iliyopita baada ya kuzomewa na watu huko Manchester, Uingereza ila baadae alirudi tena.
Justin anasema atafundisha mashabiki wake kuwa na shauku ya muziki wake na sio kumuona yeye tu, baadhi ya watu kwenye show hio wamekuwa na hisia tofauti wengine wakisema anaelekea kuwa na msongo wa mawazo.
Hii sio mara ya kwanza JB anasisitiza mabailiko, awali alikata kabisa mashabiki kupiga picha na yeye bila kuomba.

Post a Comment

0 Comments