Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MAKAMU
wa rais ,Samia Suluhu Hassan,amewataka kuwafichua watumishi mbalimbali
wa halmashauri na taasisi za serikali katika wilaya na mikoa
wanaodhaniwa kufuja fedha za serikali na kupoteza mapato lengo ikiwa ni
kuzikusanya fedha na kuzirudisha katika mikono ya wananchi waone faida
yake.
Amesema serikali ya awamu ya tano inaendelea na nguvu yake ya kukusanya mapato na kuziba mianya ya rushwa na kupotea kwa mapato.
Aidha
Samia ametoa rai kwa wananchi mkoani Pwani kuendelea kushirikiana na
vyombo vya ulinzi na usalama kulinda amani na usalama wa mkoa huo
kufuatia kujitokeza kwa mambo ambayo yameonekana kuhatarisha usalama wa
mkoa hivi karibuni.
Katika
hatua nyingine amewahakikishia wakazi wa mji wa Chalinze kutatua tatizo
la maji ambalo bado ni kero kubwa ambapo ameeleza kwamba mwishoni mwa
mwaka huu matunda yataanza kuonekana.
Akizungumza
na baadhi ya wananchi wa Mlandizi na Chalinze,mkoani Pwani wakati
aliposimama kuwasalimia akielekea mjini Dodoma kikazi,alisema wananchi
waiamini serikali yao kwani imeanza kuirejesha nchi katika nidhamu ya
mapato na matumizi na kazi ya maendeleo inaendelea.
“Watanzania
watajenga Tanzania yao wenyewe na serikali yake na Tanzania inaweza
kujiendesha yenyewe na kama itategemea misaada iwe sio kwa kiasi
kikubwa.”alisema.
Aliwasisitiza wananchi kulipa kodi pale inapohitajika ili kusaidia na serikali kuinua mapato yake.
Hata
hivyo Samia aliwataka wakulima na wafugaji kuishi kwa upendo na
mshikamano baina yao pasipo kutofautiana kwani kwa kufanya hivyo
kunasababisha migogoro isiyo na tija na wakati mwingine kuvunja amani.
Kufuatia
ombi la Mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete ,kumweelezea
kuhusu kero ya maji inayowakabili wakazi wa jimbo hilo,Samia alisema
serikali inatambua hilo na kwasasa ipo katika mpango mzuri wa kumaliza
tatizo la maji lililopo.
Alielezea
kuwa WAMI yapo maji ya kutosha lakini tatizo ni usambazaji ,hivyo
wanatarajia kuvuta maji kwa mabomba hadi eneo la Pera na kujenga matanki
makubwa yenye ujazo wa lita 300,000 ,Kibiki watajenga tanki lenye ujazo
wa lita 200,000 ili maji yakifungwa kuweze kuwa na maji ya kufikisha
kwa wananchi kirahisi.
Makamu
huyo wa rais alisema watajenga hifadhi nyingine ya maji pale Mazizi
yenye lita mil.2 ambayo itawezesha kutumia maji ndani ya wiki mbili bila
kukatika ambapo mpango huo upo njia na tayari mkandarasi yupo na
wametanguliza sh.bil 43 ili kazi ianze .
Samia
wakati anafanya kampeni ili kuomba kuchagulia kuingia madarakani
aliahidi kuwatua akinamama ndoo kichwani kwa kutatua tatizo la maji na
kusema anashughulikia suala hilo hadi hapo atakapowaondolea wananachi
adha ya kutembea umbali mrefu kusaka huduma hiyo muhimu.
“Nayachukua
mambo yote na nitaendelea kuyafanyia kazi ,natambua kilio chenu hasa
akinamama ambao huamka usiku ama kutembea umbali mrefu kutafuta
maji”alisema Samia.
Akizungumzia
suala la afya kuhusu vifaa tiba alisema atazungumza na wizara husika
kutatua kero ya vifaa tiba,madawa na watumishi katika kituo cha afya
Msoga ili kupunguza mzigo kwa hospitali za rufaa ikiwemo Tumbi.
Alisema
tatizo la watumishi karibu litamalizika,kulikuwa na idadi kubwa ya
watumishi hewa hivyo walikuwa wakiisafisha watumishi hao na hivi
karibuni watafungua ajira mpya baada ya zoezi hilo kukamilika.
Samia
aliipongeza Chalinze kumaliza tatizo la madawati ila kwenye mafanikio
kunajitokeza tatizo jingine hasa kutokana na idadi ya wanafunzi imekuwa
kubwa na kuzalisha tatizo la madarasa .
Aliwataka
viongozi wa wilaya na mkoa kuelekeza nguvu zao kujenga ,kuongeza na
kukarabati majengo ya madarasa ili watoto waweze kusoma .
Kuhusiana
na ahadi ya ujenzi wa soko na stend mjini Chalinze,amemuagiza mkuu wa
mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo kuhakikisha anasimamia hatua ya
tathmini ya eneo lililopatikana kwa ajili ya ujenzi huohadi ifikapo
mwezi novemba mwaka huu.
Viwanda
na uwekezaji,anasema serikali kwasasa inasuka nguvu za viwanda na
uwekezaji mkoani hapo kujenga kwa ajili ya kutengeneza ajira na kukuza
uchumi wa mkoa .
Alisema
viwanda vikubwa 10 vitajengwa ikiwemo cha chuma na nondo,cha
kutengeneza vigae na kusindika matunda hivyo wananchi wawe tayari
kupokea wawekezaji ili kupunguza tatizo la uhaba wa ajira.
Akiwa
Mlandizi ,Samia aliahidi kuweka uzio kama alivyoahidi wakati wa kampeni
kwenye uchaguzi uliopita katika kituo cha afya Mlandizi kwani ni moja
ya sifa ya kuandishwa kwa kituo cha afya kupanda hadhi ya wilaya na bado
wanania ya kupandisha hadhi ya kvituo mbalimbali ili kuzipunguzia mzigo
hospitali za rufaa .
Alisema
soko la mlandizi bado ni dogo ila ana taarifa kuwa kwenye eneo la
Kisabi A na B kuna maeneo yamepimwa kwa ajili ya masoko na Tamisemi
wameweka mkono kidogo na kuwahakikishia kuwa atakaa na Tamisemi
kuangalia uwezekeno wa kuachia maeneo hayo ili kuwepo na soko na stend
kubwa .
Alieleza
kupimwa kwa mji wa Mlandizi na kusema ataongea na wizara ya ardhi na
sasa bahati nzuri wizara hiyo wamekuwa wepesi kufanya zoezi hilo hivyo
ataweka msukumo kwa wizara ili waweze kupimiwa na barabara ya
Mlandizi-Mzenga ahadi ipo palepale itajengwa kwa kiwango cha lami .
0 Comments
on