Tukio la msanii wa muziki wa Bongo Fleva, kuzimiwa kipaza sauti wakati aki perform jukwaani,hapa mjini Mombasa, limeusishwa na imani za kishirikina.

Akifanya mahojiano na kituo kimoja cha radio nchini Kenya, Mganga mashuhuri wa jadi kutoka nchini Tanzania, aitwaemuungu wa kabili, alinukuliwa akisema kuwa “ Suala la Ali Kiba ni suala la kichawi “, asisingiziwe Sallam meneja wa Diamond wala Diamond mwenyewe, wala waandaaji wa tamasha, wala walinzi wa Chris Brown.

Muungu wa Kabili ambae inadaiwa, alikuwa akiongoza kikosi cha jadi kinachoundwa na waganga mbalimbali kutoka nchini Tanzania na Kongo ya mashariki, alikuwepo jijini Mombasa, kuongoza kamati ya ufundi katika kuhakikisha tamasha hilo linafanyika bila kutokea kwa shari yoyote inayo weza kusababishwa na wachawi au maadui kama vile kunyesha kwa mvua ya kichawi, kutokea kwa stampede ( kiwewe kinachopelekea watu kukanyagana na kufa ), nakadhalika.

Lakini hata hivyo alipoulizwa kuhusu jambo hilo hakukubali wala kukataa ingawa anasema alikuwepo jijini Mombasa kwa kikazi na alikuwa mmoja wa watu walio hudhuria tamasha hilo.

Muungu wa Kabili aliongeza “ Wachawi na washirikina wanapenda sana kuhudhuria kwenye matukio yenye kuhusisha idadai kubwa ya watu kama vile matamasha ya muziki, mikutano ya kisiasa nakadhalika, kwa saabu katika maeneo hayo, kuna vitu vingi sana vya kichawi na kishirikina ambavyo wachawi huvichukua kwa ajili ya matumizi ya shughuli zao za kichawi “

“Mfano wa mambo ambayo wachawi huyafuata kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu ni pamoja na mchanga, udongo pamoja na mabaki ya vitu vilivyopo katika eneo la tukio.” Aliongeza muungu wa kabili.

Mchanga ama udongo wa kwenye eneo lenye mkusanyiko mkubwa wa watu ambao wamekesha hadi asubuhi huchanganywa na dawa zingine za kichawi kwa ajili ya kutengeneza ndumba za biashara na kufanyab biashara zitoke sana.

Ilhali uchafu uchafu na mabaki ya kwenye eneo lenye mkusanyiko mkubwa wa watu, hutumiwa na watu wa mazingaombwe kwa ajili ya kutengeneza viini macho. Alieleza muungu wa kabili.

Akizungumzia kuhusu tukio la Ali Kuzimiwa kipaza sauti na kushushwa jukwaani bila ridhaa yake, muungu wa kabili alisema.

“ Uzuri ni kwamba, nilikuwepo katika eneo la tukio na nilishuhudia kila kitu. Katika mikusanyiko mikubwa ya watu ambayo inakesha huwa kuna shughuli nyingi sana za kichawi na kishirikina. Kama hauna macho ya kiroho, hauwezi kuona kinacho endelea.”

Una jua katika uchawi huwa kuna vitu vinaitwa “ Mamlaka za kichawi”. Mamlaka za kichawi zinahusisha mambo mengi sana. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na mambo ambayo wachawi huyatumia kulogea watu. Unajua mchawi hawezi kuloga mtu bila kufananisha ulozi wake na kitu kingine.

Kwa mfano , katika uchawi wa kuwatenganisha watu kama vile wanandoa, ndugu au marafiki, na kuwa fanya wasionane tena hadi wanarudi kaburini, wachawi hufanya matambiko maalumu, kasha hutafuta nyayo za watu walio kusudia, nyayo hizo zinafanyiwa ulozi, halafui unyayo wa mtu mmoja utakwenda kuzikwa kwenye mlima mmoja, ambao labda upo Mombasa, na unyayo wa mtu mwingine utaenda kuzikwa kwenye mlima ambao labda upo, NAIROBI.

Sasa katika ulozi wao, wachawi watasema maneno kama vile “ FULANI BIN FULANI, SIKU YA LEO NIMEKUZIKA, KATIKA MLIMAA HUU ULIOPO HAPA MOMBASA, NA FULANI BIN FULANI YEYE AMEZIKWA KWENYE MLIMA FULANI ULIOPO HUKO NAIROBI. KAMA MLIMA HUU ULIOPO HAPA MOMBASA, UNAWEZA KUKUTANA NA MLIMA ULIOPO NAIROBI, BASI NA WEWE FULANI BIN FULANI AMBAE NIMEKUZIKA KATIKA MLIMA HUU, UTAWEZA KUKUTANA NA FULANI BIN FULANI AMBAYE YUPO NAIROBI.

LAKINI KWA KUWA WEWE FULANI BIN FULANI AMBAE UMEZIKWA KWENYE HUU MLIMA ULIOPO HAPA MOMBASA, HAUWEZI KAMWE KUKUTANA NA FULANI BIN FULANI, AMBAE AMEZIKWA HUKO NAIROBI.BASI HATA W EWE FULANI BIN FULANI HAUTAKUTANA NA FULANI BIN FULANI MPAKA SIKU UNAINGIA KABURINI “

Mifano ipo mingi sana. Haya mambo ya kulinganisha katika ulozi yapo ya aina mbili, Yapo ya asili na yapo ya kutengeneza.

Turudi kwa Alikiba na kuzimiwa kipaza sauti Mombasa. Kwenye mikusanyiko ya watu wengi, wachawi hutuma majini kwa ajili ya kuwaangusha au kuwaua watu, na kisha baada ya hapo, kutumia udongo , au mabaki yaliyopo katika eneo husika, katika kutengeneza uchawi wa aina mbalimbali kama vile kifafa cha kichawi, au kushusha nyota.

Uchawi huu hutumwa katika eneo husika, na hunuizwa watu kuanguka,kuzimia au hata kufa. Walengwa wakuu wa uchawi huu ni watu maarufu.

Tukio la Ali Kiba, katika ulimwengu wa kiroho lina ashiria, kuzimwa na kushushwa nyota yake kwa nguvu.
Kuzimiwa kipaza sauti kunaashiria kuzimwa kwa nyota yake na kushushwa jukwaani kuna ashiria kushushwa nyota yake.

Tukio hili halikukusudiwa kwa Ali Kiba, ni uchawi ulionuiziwa kwa watu wote katika eneo hilo, sema Ali Kiba amekuwa mhanga tu.
Hii maana yake ni kwamba, wachawi wataenda kuchukua mchanga katika eneo hilo, na watautumia kutengeneza uchawi wa kushusha na kuzima nyota za watu.

Siku ya tukio, sio Ali Kiba pekee, wapo watu wengi tu walio anguka tena wenyewe, lakini kwa sababu sio maarufu, Ali Kiba ndio alionekana.

Hii haimaanishi kuwa Ali Kiba ameshushwa nyota yake la hasha. Nyota yake itaendelea kuwa juu na ataendelea kufanya vizuri katika shughuli zake za muziki.

Wachawi watatumia tukio la kushushwa na kuzimiwa kipaza sauti. Kwa mfano “ Kama fulani bin Fulani, pamoja na kwamba yupo juu , lakini alizimiwa kipaza sauti na akashushwa chini, basi hata Fulani bini Fulani nae pia nyota yake itazimwa na kushushwa.

Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa taarifa kwamba meneja wa Salam ndio alifanya fitna ili Ali Kiba azimiwe microphone pamoja na madai kwamba, walinzi wa Chris Brown ndio walishinikiza Ali Kiba ashushwe,muungu wa akili alisema.

“ uchawi ni unafiki. Hizo sababu unazo zitaja ni unafiki na sio kweli. Wachawi hutumia busara sana wanapo fanya mambo yao, siku zote huwa hawataki kujulikana ndio maana huwa wanatengeneza sababu mbadala, ili watu wasiwastukie.

Mfano wakitaka kukuchukua msukule, watakutengenezea sababu kama vile ajali au ugonjwa wa ghafla nakadhalika.

Mfano mzuri ni ule wa kwenye maandiko matakatifu, Ndugu zake Yusufu mwana wa Yakobo, walipo muuza ndugu yao utumwani, walitengeneza uongo wa kupeleka kwa baba yao kwamba, Yusufu ameuwawa na Simba.

Katika kusapoti uongo wao, wakararua nguo za Yusufu, wakachinja damu ya kondoo na kupaka kwenye nguo za Yusufu.

Baba ya Yusufu alivyo tazama nguo za mwanae zilizo tapakaa damu, akaamini kabisa motto wake amekufa, kumbe ameuzwa utumwani. Hiyo ndio hekima ya kishetani inayo tumiwa na wachawi.

NINI SULUHISHO KWA ALIKIBA : muungu wa kabili anasema “ Katika ulimwengu wa kiroho, Ali Kiba haja athiriwa chochote na tukio la Mombasa, lakini ni muhimu awatafute masheikh, wamfanyie kisomo maalumu na ibada..

Miezi kadhaa iliyo pita, mwanadada mmoja alitoa ushuhuda wake kupitia vyombo mbalimbali vya habari, akimlaumu muungu wa kabili kwa kumfanyia madawa ya kichawi ambayo yalimletea matatizo makubwa katika maisha yake.

Maelezo ya mwanadada huyo yalibeba kichwa “ NILIMLISHA MUME WA MTU LIMBWATA LA NYAMA YA BUNDI “ na yanapatikana mtandaoni.


Chanzo cha Makala :  JAMII  FORUMS   <<Hapa>>


==