Kitendo
cha askari polisi kumpigia saluti Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi
(CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa, Profesa
Ibrahim Lipumba imezua gumzo la kuhoji uhalali wake.
Askari
huyo alionekana juzi akimpigia saluti Profesa Lipumba katika eneo la
Buguruni ambapo mwanasiasa huyo alienda kushiriki zoezi la usafi.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alipoulizwa kuhusu usahihi wa
askari polisi kuwapigia saluti viongozi wa vyama vya siasa wasio wabunge
alijibu kwa ufupi, “sio sawa.”
Kwa
mujibu wa Kanuni za Jeshi la Polisi (PGO) namba 102, haiwataji viongozi
wa vyama vya siasa wasio wabunge kati ya watu wanaopaswa kupewa salamu
hiyo ya jeshi yenye kuonesha heshima.
Aliyekuwa
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Kapteni
John Chiligati aliwahi kueleza Bungeni kuwa saluti ni ishara ya kuonesha
heshima kwa kiongozi mkuu kwenye asasi za kijeshi.
Kapteni
Chiligati alisema kuwa mbali na viongozi wa kijeshi, viongozi wengine
wanaopaswa kupewa saluti ni wa mihimili ya Serikali, Bunge na Mahakama.
Wengine ni majaji wote, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na mahakimu wa mikoa na wilaya wakiwa kwenye mahakama zao.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha CCK, Renatus Muabhi alisema kuwa huenda askari huyo
alipiga saluti kwa kupaniki kutokana na maagizo aliyopewa ya kumlinda
Profesa Lipumba katika zoezi hilo.
0 Comments
on