MUANDISHI : EDDAZARIA
ILIPOISHIA
Mtu
huyo wa ajaba akaendelelea kutazama tazama kila kona ya sable hii,
akapiha hatua mbili mbele na kuzama ndani kabisa ya sable hii, na kuwapa
mgongo Rahab na Raisi Praygod walio simama nyuma yake. Akaendelea
kuvuta vuta pumzi, iliyo muashiria kwamba humu ndani kuna binadamu
waklio hai, akalikoki bunduli lake aina ya gobore na kulishika vizuri
huku kidole chake kimoja akiwa amekizamisha kwenye traiga, kwa haraka
akageuka nyuma na kuwaona Rahab na Raisi Praygod wakiwa nyuma yake
wanamtazama
ENDELEA
Kwa
haraka Rahab akaruka hewani na kuipiga teke bunduki ya mtu huyu mwenye
muonekano wa ajabu sana, bunduki yake ikaanguka chini na kumpa nafasi
nzuri Raisi Praygod kumrukia mtu huyo kwa kutumia bega lake lililo tua
begani kwa mtu huyo na wote wawili wakaanguka chini.
Rahab kwa haraka akaiokota bunduki ya mtu huto na kwakutymia kitako cha bunduki hiyo aina ya gobore akampiga nayo kichwani zaidi ya mara kumi mtu huyo, na kupelekea kichwa cha mtu huyo kupasuka kwa na kuvuja damu yenye rangi nyeusi ti.
Rahab kwa haraka akaiokota bunduki ya mtu huto na kwakutymia kitako cha bunduki hiyo aina ya gobore akampiga nayo kichwani zaidi ya mara kumi mtu huyo, na kupelekea kichwa cha mtu huyo kupasuka kwa na kuvuja damu yenye rangi nyeusi ti.
“Mtu gani huyu….?”
Rahabu
aliuliza huku akihema kwa nguvu akionekana kuchanganyikiwa kwa kumuona
mtu wa aina hii ambaye tangu azaliwe hajawahi kumuona.
“Tuondike hakuna haja ya kuendelea kukaa hapa”
Raisi
Pragod alizungumza huku akichungulia mlangoni kutazama kama wale watu
wengine wa kutisha wamesha ingia ndani walipo kua wakiingiza mizoga ya
watu walio waua. Wakatoka nje wakiwa katika tahadhari kubwa huku Rahab
aklwa ameishika bunduki ya mtu huyo.
Wakafanikiwa kutoka nje pasipo kuonekana na watu hao ambao wapo ndani ya kijumba chao wakiendelea kuwakata kata vipande marehemu walio wachukua na kuwafanya ndio chakula chao cha usiku. Wakaanza kutokomea porini huku wakimuomba Mungu waweze kutoka kwenye msitu huu ambao bado haujawapa matumaini ya kuweza kuziokoa nafsi zao zilizo kwenye matatizo makubwa
Wakafanikiwa kutoka nje pasipo kuonekana na watu hao ambao wapo ndani ya kijumba chao wakiendelea kuwakata kata vipande marehemu walio wachukua na kuwafanya ndio chakula chao cha usiku. Wakaanza kutokomea porini huku wakimuomba Mungu waweze kutoka kwenye msitu huu ambao bado haujawapa matumaini ya kuweza kuziokoa nafsi zao zilizo kwenye matatizo makubwa
Hasili
ya watu hawa wa kutisha wanajulikana kama Mazombi, walio anza
kujitokeza mwaka 1819 katika bara la ulaya. Inasemekana watu hawa ni
wale walio weza kupoteza maisha kwa sumu zenye kemikali kubwa na
waliweza kurudi katika ulimwengu huu wakiwa katika hali hiyo ya kutisha
na kuweza kuwafanya wanadamu halisi kama ndio vitoweo vyao vya kila
siku.
Rahab
na Raisi Praygod wakaendelea kukata mbuga pasipo kuchoka, japo
wanatamani kuweza kupata japo dakika waweze kupumzika, ila kila walipo
kumbuka maiti za watu walio waona wakishushwa na mazombi hayo
hawakutamani kamwe kuweza kusimama.
Hali
ya majonzi ikawatawala mazombi walio mshuhudia mwenzoa aliye pasuliwa
kichwa na kusababisha ubongo wote kumwagika nje. Hawakua na hamu hata ya
kuendelea kupata vitoweo walivyo kuja navyo na ziadi kila mmoja
akachukua silaha yake na kuingia msituni kufwatilia watu hao walio
sababisha mauaji ya mmoja wao. Kutokana na kuufahamu vizuri msitu wao,
wakajigawa kwenye makundi ya mazombi wawili wawili na kupelekea kuwa na
vikundi vinne. Kila mmoaja akajiapiza kuweza kufanya mauaji ya kikatili
kwa watu walio sababisha mauji ya mpendwa wao
***
Samson
na wezake wakafanikiwa kufika katika kiswa cha Kunashir nchini Russia,
kwa bahati nzuri wakafanikiwa kupokelewa na mkuu wa kikiso kilicho asi
nchi ya Russia bwana Rusev, Wakapelekwa moja moja kwa moja kwenye jengo
lenye ofisi za kikundi hichi kinacho endelea kufanya mapinduzi kwenye
nchi yake ikiitaka serikali kuweza kuunda serikali mbili, ili wao
wajipatie mamlaka ya kuweza kutengeneza silaha hatari za nyuklia.
Kila
mmoja akakabidhiwa kinywaji alicho kihitaji yeye, ili kuweza kujipozwa
kwa uchovu mwingi wa safari yao ndani ya maji, tangu pale walipo kamtwa
na jeshi la polisi nchini Tanzania. Fetty na wezake hawakuwa na uwezo wa
kuielewa lugha ya kirusi, ambayo Samson yeye aliweza kuizungumza vizuri
pasipo matatizo ya aina yoyote. Alicho kua akikifanya Samson ni
kuwatafsiria kila kitu ambacho alicho kua akikizungumza na bwana Rusev.
“Jamaa anauliza eti, tunaweza kujiunga na kundi lake?”
“Mmmm……!!” Anna aliguna
“Hatuwezi sisi tupo hapa kwa ajili ya biashara”
Samson
akamjibu bwana Rusev kitu alicho kizungumza Fetty anaye onekana kuto
kubaliana na swala zima la wao kujiunga na kundi la bwana Rusev
“Je anauliza tunahitaji kiasi gani cha pesa ili tuweze kumkabidhi hii manohari?”
“Sasa hapo ndio umenena la maana” Halima alizungumza huku akitabasamu
“Anatulipa kwa dola au shilingi?” Agnes aliulza
“Hembu na wewe acha ushamba wako, huku shilingi aitolee wapi?” Fetty alimkosoa mwenzake
“Haya yaishe kiongozi Fetty”
“Muambia sisi tunataka dola milioni mia zinatutosha”
Samson
akamgeukia bwana Rusev na kumueleza kiasi walicho kitaja wezake na
bwana Rusev hakuwa na hiyana zaidi ya kukubali kuwalipa kiasi hicho.
“Anauliza tunataka cashe au hadi benki?”
Anna akashusha pumzi na kubugia fumba moja la juisi anayo kunywa
“Hapa cha msingi kila mmoja apewe kiasi chake mkononi, tusepe” Halima alizungumza huku akiwatazama wezake machoni
“Ujue hizo pesa ni nyingi sana, na kama kuzibeba itakua ngumu?” Fetty alishauri
“Sawa
Fetty, haya tukisema tupewe kwenye, akaunti namba tutazitolea wapi,
hiyo moja, mbili sisi site hapa tunatafutwa karibia dunia nzima, ni
benki ipi tutazipeleka sura zetu na kwenda kuitoa hiyo pesa?”
“Kumbe
siku moja moja na wewe. Anna unazungumzaga poiti. Kikubwa hapo Samso
muambie huyo mtui wako tunahitaji cashe hapa hapa, kam ni kwenye mabegi
tutabeba, cha msingi ni kupewa pesa na kwenda kuanza maisha mapya mbele
ya safari”
Agnes
alizungumza na wote wakakubaliana waweze kukabidhiwa pesa zao mkononi,
Samson akamueleza bwana Rusev maamuzi waliyo yafanya wezake. Bwana Rusev
akanyanyua mkonga wa simu yake ya mezani, akaminya namba kadhaa na
kumpa maelekezo mlinzi wake, pamoja na muhasibu wake.
“Jamaa anasema pesa inakuja”
Kila
mmoja akajiweka mkao wa kupokea kitita chake, ili aweze kuendelea na
maisha yake mbele ya safairi. Baada ya dakika kumi na tano kukatika
kundi kubwa la watu wapatao kumi, wenye bunduki wakaingia ndani ya ofisi
ya bwana Rusev, jambo lililo anza kuwapa wasiwasi Fetty na wezake ambao
hawakueelewa ni kitu gani kinacho endelea kwani, watu hao wameingi
gafla na moja kwa moja wakamzingira bwana Rusev.
***
Kitendo cha Rahab kujikwaa na kuanguka chini, ikawa ni bahati nzuri
kwake, kwani mshale ulio kuwa umelengwa na zombi mmoja ulipita juu yake
na kugonga kwenye mti uliopo mbele yake.
“Haaa……!!!”
Rahab
alijikuta akiduwaa na kutazama nyuma, kwa mbali akamuona mtu huyo aliye
fura hasira akija kwa kasi ya ajabu, kwa haraka Rahab akaikota bunduki
yake, kwa bahati nzuri akakuta kuna risasi moja, akaikoki kwa haraka na
kumlenga zombi huyo anaye mfwata kwa kasi. Kama kawaida yake Rahab,
hakukusoea kuifyatua risasi hiyo iliyo tua kichwani mwa zombie huyo na
kumpua kchwa na kugawanyika vipande vipande. Raisi Praygod akaendelea
kushangazwa na uwezo mkubwa wa upambanaji alio kua nao Rahab ambaye
hakumdhania kwamba anweza kuja kuwa msaada mkubwa sana kwenye maisha ya
kuiokoa roho yake. Rais Praygod akampa mkono Rahab na kumnyanyua kutoka
chini alipo kua ameanguka. Wakaendelea na kukimbia.
Mlio
wa bunduki, ukawastua mazombi wote walio kua kwenye msitu huu,
wakafahamu ni wapi mlio huo wa bunduki ulitokea, walicho kifanya ni
kubadili mielekeao yao na kwenda sehemu ya tukio huku akijifariji kwamba
watu wanao wawinda watakua wamekamatwa na mmoja wao. Wote wakajikuta
wakishikwa na butwaa baada ya kumkuta kiongozi wao akiwa amechanguliwa
kichwa chake kama ilivyo kua kwa mwenzao waliye mkuta ndani ya kijumba
akiwa amekufa, Baadhi yao hawakuweza kuyazuia machozi yao kuweza
kumwagika kwani kiongozi wao huyo ndio kila kitu katika maisha yao.
Rahab
na Raisi Praygod wakaendelea kutokomea msituni, huku mwanga wa
mbalamwezi ukizidi kuwapia uwezo wa kuweza kuona ni wapi wanapo kwenda
na niwapi wanapo tokea. Wakafanikiwa kufika barabarani ambapo wakalikuta
gari la watu hao wa ajabu, likiwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara.
Wakaanza kulinyatia taratibu, huku kila mmoja akiwa amepita upande wake.
Wakafanikiwa kufika mbele, kwenye kichwa cha dereva, wakachungulia ila
hapakuwa na mtu wa aina yoyote zaidi funguo inayo ning’inia pembeni ya
mskani
“Panda”
Raisi
Praygod alimsisitiza Rahab ambaye alikua akiendelea kulichunguza gari
hilo linalo toa harufu kali ya mizoga iliyo kufa. Rahab akafungua mlango
na kuingia, Raisi Praygod akawash gari, taratibu wakaanza kuondoka
katika eneo hilo huku, raisi akijitahjidi kuongeza mwendo wa gari hilo
linalo toa mgurumo mbaya, kama mabati yanayo gonganga kwa nguvu
Mlio
wa gari, ukawastuaa mazombi hao walio kua wakiendelea kusononeka na
kuomboleza kifo cha kiongozi wao. Wanne kati yao, wakakimbilia sehemu
mlio wa gari unapo tokea huku wengine wakiubeba mwili wa mkuu wao
kuurudisha kwenye makazi yao.
Gafla
raisi Praygod akajikuta akifunga breki kali, baada ya kuwaona mazombi
wanne wakiwa wamesimama katikati ya barabara huku kila mmoja akiwa
ameshika bunduki aina ya gobore, wakiwa wamezielekezea kwao, wakiwa
tayari kwa kuwalenga Raisi Praygod na Rahab.
***
Wanajeshi
wa bwana Rusev walio mzingira, wakamnyanyua kiongozi wao, huku
wakimuhitaji aweze kukumbia kwani kuna mashambulizi ya ndege za kijeshi
la Russia yanaweza kufanyika ndani ya dakika kadhaa zinazo kuja.
Wakatoka kw mwendo wa kukimbia huku wakiwa wamemzingira kiongozi wao
huyo wanaye mtukuza kama muumba wao.
“Jamani inakuwaje, mbona tumeachwa peke yetu?”
Anna
aliuliza huku akiwa amesimama wima akichungulia mlangoni na kumuona
kiongozi huyo akiingia kwenye lifti yeye na wanajeshi wake na kushuka
chini.
“Tuondokeni”
Samson
alizungumza huku akiongoza msafara wa kuelekea walio elekea bwana Rusev
na wanajeshi wake, kwa mwendo wa haraka wakafanikiwa kufika kwenye
lifti, ikawalazimu kuweza kusubiri baada kwa muda kidogo kwani bwana
Rusev na watu wake walikua wanaelekea chini wakitokea gorofa ya tano.
Baada ya muda lifti ikafunguka na wote watano wakaingia ndani na Samson
akaminya kitufe cha kuelekea chini. Wakiwa katika gorofa ya tatu,
mtikisiko mkubwa, wa bomu ukatokea na kuisababisha gorofa hilo kuyumba
na umeme ukakatika na kuipekea lifti hiyo kusimama na kumfanya Agnes
kupiga ukelele mkali, kwani gorofa lilianza kuteguka vipande vidogo
vidogo likielekea kuanguka chini.
SHE IS MY WIFE(30)
Mtikisiko ukaendelea kulitetemesha jengo lihi ambalo lilipigwa kombora
na ndege ya jeshi la Russia, ikiwa ni shambulizi la kustukiza kwenye
kikosi hichi kinacho itesa serikali kwa kipindi kirefu. Kwa bahati nzuri
mlango wa lifti ukaweza kuachia upenyo mdogo, kwa kutumia nguvu Samson
akaanza kuufungua hadi ukafunguka, kwa bahati nzuri sehemu lifti ilipo
kwamba ni gorofa ya pili, wakatoka wote kwa pamoja na kutafuta eneo
lenye ngazi za kushukia. Kwa bahati nzuri eneo la ngazi halikua mbali
sana na eneo zilipo lifti.
Milio
ya risasi, ikaanza kusikika vizuri masikioni mwao, ikitokea nje, hhuku
kindi la Mr Rusev likipambana na wanajeshi walio kuja kuvamia katika
kisiwa hicho, wakafanikiwa kutoka nje huku gorofa hilo wakiliacha
likendelea kumeguka vipande vidogo vidogo.
“Twendeni huku”
Samson
alikua kiongozi wa wengine, na hapakuwa na wakumuuliza kwamba ni wapi
wanapo elekea kwani kila mmoja alihitaji kuyaokoa maisha yake au kuuokoa
usalama wake kutoka mikononi mwa jeshi la serikali hiyo inayo linalo
sifika kwa maamuzi magumu pale wanapo mkamata mtu anaiye jihusisha na
ugaidi, na mara nyingi wa wa namna hiyo wameweza kuambulia kifo kwa
kupigwa risasi nyini zisizo na idadi mwilini mwaoa kama alivyo fanyiwa
kiongozi Saddam Hussein.
Wakafanikiwa kufika kwenye moja ya jengo, ambalo milango yake yote imefungwa kwa makufuli makubwa
“Samson tunafanyaje sasa?”
Halima
aliuliza huku macho yakimlenga lenga. Samson hakumjibu chohote Halima
zaidi ya kuziangalia ndege za jeshi, aina ya Jet zikipita kwa kasi
katika eneo mbali kidogo na sehemu walipo, huku zikimwaga risasi nyingi
kwa wanajeshi wa Bwana Rusev. Hapa ujambazi wao wakauona haufui dafu
mbele ya shambulizi hili lililo wapagawisha akili zao huku kila mmoja
asijue ni wapi kwa kwenda.
Kwa
bahati nzuri bwana Rusev akafanikiwa kuingia kwenye manohari walio kuja
nayo Samson na rafiki zake, akiwa na kundi la wanajeshi wake walio kuja
kumchukua ofsini kwake. Hapakupoteza muda zaidi ya kuondoka katika eneo
la kisiwa ambacho kwa sasa hali yake imekua mbaya zaidi ya kuzimu. Ila
nafsini mwake bwana Rusev akatokea kuwaonea huruma sana Samson na
mabainti wadogo alio kuja nao, ambao Samson aliwaeleza walikuwa ni
magaidi wanao anza kuchipukia katika swala zima la kigaidi.
Kazi
ikawa ni ngumu kwa Samson na wezake ambao hadi sasa hivi hali inazidi
kuwa tete kwao, hawakujua ni wapi waende kukweukwepa mkono wa serikali,
mfano mzuri wanaouona kwa askari wa bwana Rusev wanavyo angushwa chini
kama kuku wenye videri kwani, risasi kutoka kwenye ndege hizo za jeshi
hazikukosea wapi kwa kupiga.
“Jamani hapa hatuna la kufanya, kila mmoja atawanyike kivyake akaokoe maisha yake mbele ya safari”
Samson alizungumza huku akihema kwa nguvu
“Nyoo atawanyiki mtu hapa, wewe ndio umetuleta na wewe ndio utatuokoa”
Agnes alizungumza kwa hasira akionekana kumpiga Samson vikali, kwa wazo lake alilo liropoka
“Sikia SAMSOM. Nahisi hutujui vizuri wewe eheee?”
Fetty
alizungumza huku sura yake ikiwa imebadilika kabisa, akionekana anaweza
kufamfanya Samson kitu chochote muda wowote kuanzia sasa. Samson
ikambidi awe mpole kana ni uwezo wa kupigana na Fetty na wezaka anao,
ila hajui ni watu wa aina gani hadi wanajiamini kiasi hichi na kuwa
magaidi wanao sakwa na jeshi la polisi Tanzania.
“Twendeni huku”
Ikamlazimu
Samson kuwa kuanza kukimbia kuelekea asipo pajua, ila alihitaji
kuepukana na varangati la Fetty na wezake, kwani anafahamu varangati la
Rahab, alilo anzishiwa siku alipo kua naye chumbani, na hawa ni rafiki
wa Rahab, ina maana wote varangati lao si lakitoto. Wakazidi kukimbia
huku wakimfata Samson kwa nyuma. Kila walio ona mwili wa askari aliye
fariki hawakusita kuiokota bunduki ya askari huyo, Wakaingia kwenye
msitu uliopo kwenye kisiwa hicho, Kila mmoja akajitahidi kufyatua risasi
pale walipo weza kupata nafasi ya kufanya hivyo kwa wanejeshi wa
serilali walio anza kuingia kisiwani wakitokea kwenye boti zao walizo
kuja nazo kupitia baharini.
Hapakuwa
na muda wa masihara tena zaidi ya wao kufanya kazi moja tu ya kuua kila
mwanajeshi aliye jitokeza kwenye macho yao. Mashambulizi ya ndege za
kivita yalisitishwa kutokana na wanajeshi kuingia ndani ya kisiwa,
kwahiyo ingewawia ngumu marubani wa ndege hizo aina ya Jeti kuendelea
kufanya mashambulizi ambayo yangeweza kuwadhuru hadi wezao. Hiyo ikawa
ni nafuu kubwa sana kwa Samson na wezake.
Wakafanikiwa
kufika ufukweni ambapo, wakaweza kukuta nguo maalumu za kuogelea,
zilizo vuliwa na wajeshi baadhi walio tumia njia ya kuogelea kuingia
ndani ya kisiwa hicho na kuanza kufanya mashambulizi ya kimya kimya.
Wakayavua mavazi yao waliyo yavaa, wakavaa mavazi hayo ya kuogelea
ambayo yana mitungi midgo ya gesi inayo valiwa mgongoni, huku ikiwa na
shivikizo vidogo. Kisha wakakimbilia ndani ya maji na kuanza kuogelea
kwa kasi kila mmoja anayo imudu yeye.
***
“Usipunguze mwendo muheshimiwaaaaa”
Rahab
alizungumza kwa sauti kali, iliyo mbadilisha mawazo Raisi Praygod, na
kumfanya ausogeze mguu wake kwenye brake na kuongeza mwendo huku
wakiinama chini. Mazombi hawa kwa hasira wakaanza kufyatua risasi kwenye
kioo cha gari pasipo kulipisha, Raisi Praygod akazidi kuongeza mwendo,
hadi misuli ya mwili wake ikakaza kabisa, huku akiwa amayang’ata meno
yake kwa nguvu akihakikisha anawafikia mazombi hao walio endelea kupiga
risasi.
Kwa bahati nzuri gari hilo likawaponda ponda vibaya mazombi hao walioweka mgomo wa kulipisha gari hilo na kupelekea kuwaponda ponda vibaya na kufafa. Kwa haraka Raisi Praygod akajiweka sawa kuendelea kuliendesha gari hili linalo kwenda kwa kasi, wakaendelea kuifwatisha barabara hiyo ya lami ambayo ni ndefu sana na haina kona nyingi sana, na ipo katikati ya msitu huu mnene na wakutisha.
Kwa bahati nzuri gari hilo likawaponda ponda vibaya mazombi hao walioweka mgomo wa kulipisha gari hilo na kupelekea kuwaponda ponda vibaya na kufafa. Kwa haraka Raisi Praygod akajiweka sawa kuendelea kuliendesha gari hili linalo kwenda kwa kasi, wakaendelea kuifwatisha barabara hiyo ya lami ambayo ni ndefu sana na haina kona nyingi sana, na ipo katikati ya msitu huu mnene na wakutisha.
Wakafanikiwa
kukuta kibao kilicho andikwa kwa herufi kubwa za kushongesha ‘GOOD BYE
BLACK FOREST’ Ikiamaanisha kwamba msitu huo ndio jina lake, kabdi
walivyo zidi kwenda ndivyo walivyo zidi kuoata matumaini ya kuingia
kuokoka kwani, waliweza kukutana na barabara nyingine, ambazo zina
magari ya watu wa kawaida.
“Asante Mungu”
Rahab
alizungumza huku akionekana kuto kuoamini kwamba wapo salama wakitokea
kwenye mikono ya watu ambao walihitaji kuzitoa roho zao. Taratibu gari
hilo likaanza kupunguza mwendo kasi wake, likiashiria kuishiwa na mafuta
“Vipi….?”
Rahab aliuliza huku akimtazama Raisi Pragod usoni
“Yatakua ni mafuta yamekwisha”
“Ohooo itakuaje sasa”
“Kwa hapa hakuna tatizo kutokana kuna magari yanayo pita tunaweza tukaomba msaada na kuchukuliwa”
“Mmmmm”
Raisi
Praygod akalisogeza gari hadi kando kando ya barabara na kuliegesha,
kisha wao wakashuka huku wakiwa wamevalia magauni, waliyo weza kuyapata
usiku ulio pita. Magari yakazidi kukatiza kwenye barabara waliyo kuwepo,
hii ni kutokana na kupambazuka, na mwanga wa juu kuchukua nafasi yake
katika dunia. Mwanga wa juu la asubuhi, likaendelea kupiga kwenye miili
yao, na kuwafanya wajihisi vizuri kwenye miili yao, ila njaa kwa mbali
zikaanza kuyasumbua matumbo yao yaliyo kosa chakula kwa masaa mengi.
“Muheshimiwa hapa tunaelekea wapi kwa maana sielewi elewi”
“Tusimamishe simamishe magari tutajua pa kwenda, kikubwa tumetoka kwenye hatari”
Wakaanza
kazi ya kuyasimamisha magari yanayo katiza kwenye barabara waliyopo,
kila mmoja aljitahidi kupunga mkono kwa kila gari lililo kua likikatiza
ila madereva wa magari hayo hawakuweza kusimamisha magari yao kuhofia
jinsi watu hao walivyo vyaa, wakihisi ni wendawazimu.
“Tutembee tembee mbele”
Raisi Praygod alishauri na wote wakaanza kutembea, huku wakiendelea kuyasimamisha magari hayo pasipo kufanikiwa.
“Muheshimiwa nikuulize kitu?”
“Uliza tu”
“Unavyo hisi kwa sasa, Tanzania, itakua inaongozwa na nani?”
“Aisee,
hata mimi sijui ila kisheria makamu wangu, ndio anaweza kukaimu kiti
changu cha uraisi hadi zipite siku tisini ndio wanaweza kufanya uchaguzi
wa kumchagua raisi mwengine, kama mimi sinto jitokeza”
“Ila inabidi uwahi kurudi nchini, ninaimani kwamba watu watakua wanahisi umefariki”
“Ni kweli, ila kwa sasa inanilazimu kuweza kupumzisha akili yangu, kabla ya siku tisini ninaweza kurudi nchini Tanzania”
“Sawa, je familia yako nayo si itakua na majonzi makubwa?”
“Yaaa, ila mke wangu alishafariki mwaka sasa umepita”
“Alaa, sijawahi kuisikia hiyo?”
“Ulikuwa wapi?”
“Aisee kipindi hicho mimi wala sikuwa ninajihusisha na maswala ya serikali, nilikua nikitafuta pesa kwa shida kubwa sana”
“Kwani ulikua unafanya kazi gani?”
Rahab
akakaa kimya kuweza kutafakari ni nini amjibu Raisi Praygod, ambaye
bado ni kijana mdogo wa miaka thelathini na tano. Rahab aliwaza endapo
atamuambia kwamba alikua akifanya kazi ya kuuza mwili wake, atajishusha
thamani. Pia akahisi akimueleza kwamba alikua ni jambazi inaweza kuleta
picha tofauti
“Vipi mbona kimya, haujibu swali langu?”
“Ahaaa,
kusema kweli muheshimiwa mimi, nilikua ni miongoni mwa wale wasichana
watano majambazi walio isumbua serikali kwa matukio ya uvamizi wa benki”
Raisi
Praygod akastuka kidogo, ila akajitahidi kuuficha mstuko wake, akaachia
tabasamu pana kiasi usoni mwake na kumfanya Rahab, asihisi kitu
chochote kinacho endelea kwa Raisi huyo
“Sasa kwa nini muliamua kufanya ujambazi?”
“Kusema
kweli sisi tulichukuliwa na mzungu mmoja, aliye kua akifanya kazi
kwenye hospitali ya jeshi kama daktari mwalimu wa kuwafundisha madaktari
wa jeshi kutengeneza sura bandia. Ambao yeye alikua akitufundisha kisha
na kutupa kazi ya kuweza kuua baadhi ya watu maarufu”
Hadi
kufika hapa Raisi Praygod akawa amemuelewa Rahab, nini anacho
kizungumza kwani kazi hiyo yeye ndio alipanga ianyike, akishirikiana na
rafiki yake Dokta William, kutokea Israel, kwa lengo la kuweza
kuwaangamiza watu wote wanao enda kinyume na serikali kwa kipindi hicho.
Ila hadi wasichana hao kuigeuka serikali hakufahamu kuna kitu gani
kilicho kua kikiendelea katikati.
“Ahaaa, ila kwa sasa si umeuacha?”
“Sina
haja tena inabidi, nifanye kazi halali, kwani hata yule daktari hatujui
ni wapi alipo. Wezangu nao ndio hivyo wamekamatwa, nahisi watakua
wemesha nyingwa. Kwani kwa makoso tuliyo yafanya sidhani kama wataacha
hai”
Raisi
Praygod hakuzungumza chochote zaidi ya kuangaza angaza tena macho yake
barabarani, akaona gari kubwa aina ya scania, likija kwa mwendo wa
kawaida, akalipungia mkono, ila likawapita pasipo kusimama. Kufika mbele
kidogo dereva huyo akalisimamisha gari hilo, na kuwapigia honi Rahab na
Raisi Praygod, waende wakapande.
Raisi
na Rahab wakalikimbilia gari hilo hadi sehemu lilipo simama, ambapo
dereva wa gari hilo wakakuta ni mtu mwenye asili ya Afrika. Mtu huyu
akaonekana kumtazama Raisi Praygod kwa muda kisha, huku akiwa haamini
macho yake
“Wewe si raisi wa Tanzania, bwana Praygod Makuya……!!?”
Mtu
huyo alizungumza kiswahili, sahihi akiashiria kwamba yeye ni mtanzania,
Rahab akamtazama Raisi aliye pata kigugumizi cha gafla, ila akajikaza
hivyo hiyo kumjibu mtu huyo
“Ndio, ndio mimi”
“Ingieni ndani”
Mtu
huyo alizungumza kwa furaha, na kuwafanya Rahab na Raisi Praygod
kuingia ndani ya gari na kukaa kwenye siti mbili zilizo kua wazi.
“Mimi ninaitwa Azaria, ni mtazania”
“Tunashukuru kukufahamu, hivi hapa ni wapi?”
“Huku
ni Mexco, kidogo nimekuja kutafuta tafuta maisha, nimepata kazi kwenye
kampuni hii ya kusafirisha mafuta. Vipi tena mbona huku?”
“Tulipata ajali ya ndege, mimi na huyu binti ndio tumefanikiwa kupona”
“Aisee
poleni sana wapendwa, unajua mara yangu ya mwisho kuondoka Tanzania
ndio kilikua kipindi cha kupiga kura. Nilikupa kura yangu muheshimiwa”
“Asante sana, pia asante kwa kuweza kutusaidia”
“Aisee poleni sana, pia muna bahati hapa ninaelekea mjini, ninapo ishi. Ninatoka mikoa ya chini huko kupeleka mafuta”
“Ahaaa asante sana, huyu ni msaidizi wangu anaitwa Rahab”
“Nashukuru kukufahamu dada Rahab”
“Asante na wewe pia kaka Azaria”
Wakafika
kwenye mmoja wa mgahawa ambapo Azaria akashuka na kwenda kuwanunulia
chakula pamoja na vichwaji, kisha akarudi navyo kwenya gari na
kuwakabidhi Raisi Praygod na Rahab ambao wanaonekana kuchoka sana, kwani
tangu walipande gari hilo yamekatika masaa sita wakiwa barabarani.
Wakaanza kukila chakula hicho taratibu huku wakionekana kuwa na hamu
kubwa ya kula chakula kizuri kama hicho.
“Hii safari itachukua muda gani kufika jijini Mexco City?”
Raisi Praygod alizungumza huku akiwa amefundia kipande cha paja la kuku, lililo nona sana
“Hapa
bado sana itatuchukua masaa mengine kama saba, hivi. Tuombe Mungu
tusisimamishwe na askari kwa maana huku wanajali sana kukagua passport”
“Aisee kumbe ni kurefu sana?”
“Sana tu, kwa dereva ambaye si mzoefu anaweza kulitupa gari, nje ya barabara. Ila kwa sisi wazoefu tunaona ni jambo la kawaida.”
Kutokana
na kushiba, uchovu mwingi ukamtawala Rahab na kujikuta akilala fofofo
huku, akiwaacha Raisi Praygod na Azaria wakiendelea kubadilishana mawazo
ya hapa na pale.
“Muheshimiwa
inatubidi kuweza kulala kwenye Motel moja hapo, mbele, kwani hapo mbele
kuna kizuizi cha ukaguzi, na jinsi ninyi mulivyo watatupa shida na giza
limesha ingia muda huu”
“Sawa
hakuna shida, tena umefanya la maana, kwani kuna rafiki yangu yupo hapa
Mexco ninaweza wasiliana naye akanipa hifadhi kwa muda”
“Kwa nini usiupigie ubalozi wa Tanzania ukakuletea msaada?”
“Kwa sasa sihitaji msaada wa kiserikali kuna mambo inanilazimu niyakamilishe kabla sijarudi nchini kwangu”
“Sawa muheshimiwa Raisi”
Wakafika
kwenye moja ya Motel iliyopo mbembezoni mwa barabara, na kuna magari
mengi makubwa, ikiashiria hapo ni sehemu ya madereva wengi kuweka vituo
vyao, ili kuendelea na safari zao muda walio upanga wao wenyewe. Azaria
akamuomba Raisi abaki ndani ya gari, kisha yeye akashuka kwenda kukata
vyumba vitatu, kisha akarudi akiwa na funguo mkononi
“Tunaweza kwenda”
Raisi Praygod akamuamsha Rahab ambaye muda wote alikuwa amelala fofofo, hii ni kutokana na kukesha siku nyingi pasipo kulala.
“Ehehee….”
Rahab aliweweseka kwa wenge la usingizi, huku akijitahidi kuyafumbua macho yake kuweza kutazama ni wapi walipo.
“Tumefika, shuka twende”
Raisi
Praygod akamsaidia Rahab kushuka ndani ya gari na wote wakaongozana na
Azaria hadi kwenye vyumba vyoa, huku kila walipo pita baadhi ya watu
waliwatazama RaisI Praygod na Rahab kwani wemechafuka sana, huku miili
yao wakiwa wameisitiri kwa magauni yaliyo chafuka.
Wote wakaingia kwenye chumba kimoja cha Raisi, ambapo kuna simu maalumu, yenye uwezo wa kupiga sehemu mbalimbali.
“Muheshimiwa niwaletee vyakula tena?”
“Hapana kwa mimi nipo sawa, labda kwa huyo bibie”
“Mimi ninausingizi mwaya, asanteee”
Rahab
alizungumza huku akipiga miyayo na kujirusha kitandani, hakujua kwamba
hichi chumba si chake. Azaria akataka kumuamsha ila Raisi Pragod
akamzuia.
“Wee muache tuu hakuna shida, akilala hapa”
“Sawa muheshimiwa ngoja mimi niende chumbani kwangu”
“Sawa na uwe na usiku mwema”
“Sawa muheshimiwa”
Azaria
akatoka na kumuacha Raisi Praygod akiendelea kuminya minya baadhi ya
batani za simu akijaribu kukumbuka namba za rafiki yake huyo aliye soma
naye kipindi cha nyuma nchini Canada. Kwa bahati nzuri akakuta namba ya
rafikia yake huyo ipo hewani, ikaita kwa muda, kisha ikapokelewa.
“Who?”(Nani?)
Sauti nzito ya kiume ilisikika upande wa pili wa simu
“Praygod Makuya hapa vipi wewe”
“Ahaaaa kaka, upo Mexco nini?”
“Ndio mskaji wangu, nipo kwenye motel moja hivi nimechili”
“Raisi unakaa kwenye Motel, vipi bwana mbona kuna mijihoteli mingi mikubwa kwa hadhi yako”
“Kaka yaliyo nikuta wewe acha tu?”
“Vipi kuna tatizo?”
“Yaaa tena si dogo, ila kukipambazuka tu nitakupigia ujue ni wapi nilipo uje kunifwata”
“Ahaaa
kaka kwanini usiniambie sasa hivi nije kukuchukua. Kwa maana usakama
wako wewe unahitajika na mimi ninavijana wengi tu wa kukulinda”
“Hapana Frednando, tusubiri kupambazuke nitakupigia au wewe unaweza kupiga kwa namba hii, nitakuambia ni wapi nilipo”
“Sawa kaka, haina shida, ngoja niweke mazingira vizuri”
“Sawa”
Raisi
Praygod akakata simu na kuanza kushangilia kwani matumaini ya usalama
wake kwa ujumla yamesha rudi, kwani rafiki yake ni miongoni mwa
matajairi wakubwa ndani na nchi ya Mexco. Macho ya Raisi Praygod yakatua
kwenye mapaja ya Rahab, aliye lala kifudi fudi, na kuacha makalio yake
makubwa kiasi kuonekana vizuri. Taratibu Rais Praygod akamsogelea Rahab,
akachuhuka shuka kubwa na kumfunika. Rahab taratibu akajigeucha na
kumtazama Raisi Praygod.
“Wewe hulali?”
Rahab aliuliza kwa sauti ya unyonge, huku akimtazama Raisi Praygod kwa macho yaliyo jaa usingizi, hadi akajikuta akirembua.
“Nataka nikaoge”
Rais
Praygod akapiga hatua moja, ila Rahab akamshika mkono na kumvuta kwa
nguvu na kuangukia kitandani. Rahab kwa haraka akausogeza karibu mdomo
wake kwa Raisi Praygod na wakaanza kunyonyana, huku wakionekana kuwa
katika hisia kali. Raisi Praygod akalivua gauni lake na kulitupa
pembeni. Akalishika la Rahab na akamvua, wote wakabakiwa kama walivyo
zaliwa.
ITAENDELEA
0 Comments
on