Nikiendelea
kuitadhimini barabara hii, gafla nikastukia kuliona gari la mbele yetu,
nikinyanyuliwa hewani na kitu kama bomu kutegwa, likazunguka hewani
mara kadhaa na kutua chini, kitendo kilicho mfanya dereva wetu kufunga
breki za gafla, zilizo lifanya gari kuserereka na kuligonga gari lililo
anguka na kulisukumia bondeni, kwenye korongo refu, huku matairi ya
mbele ya gari letu yakianza kutangulia kwenye korongo, huku ya nyuma
yakijitahidi kubaki barabarani.
ENDELEA SASA
Macho
yangu yote, yakahamia kwenye gari inayo kuka nyuma yetu kwa kasi kubwa,
huku dereva wake akijitahidi kufunga breki zake, akitumia juhudi zake
zote
Nikajiluta
nikiyafunga macho yangu, kwani kitu kinacho fwata sekunde chache, ni
dereva huyo, kutusindikiza kwenye korongo kama alivyo fanya dereva wetu,
kwenye gari lilil kua mbele yetu.
Dakika
kama mbili, hivi niliendelea kusikilizia ni nini kitatokea, kwetubila
haikuwa hivyo. Mwanga mkali wa taa za gari lililo kua nyuma yetu,
ukaendelea kunipiga machoni, ni sentimita chache sana, toka lilipo
simama gari lililopo nyuma yetu, huku gari letu, likianza kunesa
taratibu.
"Tutulie hivi hivi"
Dereva
alizungumza huku akihema sana, askari walio kwenye magari ya nyuma
wakashuka kwa haraka, kwenye magari yao, wakaja nyuma ya gari letu na
kuanza kujitahidi kulivuta kwa nyuma. Kutokana na uzito wa gari ikawa ni
kazi ngumu sana kwao kulivuta. Ikawalazimu kulishikilia na kutuomba
tushuke haraka.
Sikutaka
nipoteze muda, nikaufungua mlango wa nyuma katika siti niliyo kaa na
kutoka nje haraka iwezekanavyo, huku walinzi nilio kua nao ndani ya gari
wakitokea kupitia mlango nilio pitia mimi.
Walinzi
wakaliachia gari, likaporomoka kwenye korongo. Nikiwa ninatazama huku
na kule, nikawaona watu wakiwa juu kidogo ya mlima wakijipanga kwa ajili
ya kufanya shambulizi
"Shitiii"
Bila
hata ya kuomba, nikachomoa bastola moja ya mlizi aliyo ichomeka kiunoni
mwake. Nikafyatua risasi mbili kwa jamaa aliye shika bunduki aina ya
'Snaiper' ambayo ni hatari sana, kutokana na uwezo wake mkubwa.
Mashambulizi yakaanza rasmi, na watu hawa ambao ndio walio tegesha bomu
barabarani. Ikawa ni ambushi moja ambayo hakuna aliye itarajia kama
inaweza kutokea kwa wakati huu, askari wawili wakapigwa risasi na kufa
hapo hapo.
"Gari la balozi ni lipi?"
Nilimuuliza
mlinzi mmoja, niliye simama naye karibu, tukiendelea kujibu
mashambulizi ya wavamizi hawa, ambao wanapig a risasi kama wendawazimu
"Lile la mwisho"
"Nilinde"
Jamaa
akaendelea kuwafyatulia majambazi risasi, huku mimi nikikimbia
pembezoni mwa kuta ya mlima huu, jambo lililo gumu kwa majambazi kuweza
kuniona. Nikafika lilipo gari la balozi, nikamkuta akiwa ameinama kwenye
siti yeye pamoja na wanae, wakimuomba Mungu wao
"Muheshimiwa unaniamini?"
Nilimuuliza balozi mara baada ya kuingia ndani ya gari na kukaa, katika siti ya dereva.
"Ndio nakuamini."
Kutokana
gari halikuzimwa, likanirahisishia wepesi wa kufanya jaribio la
kumuokoa balozi pamoja na familia yake. Nikaangalia upenyo ulio achwa na
gari, lililo simaba barabarani, nikaamini unanitosha kupita.
Mlinzi
akanipa ishara nipite, yeye anaendelea kupambana na wavamizi hawa.
Nikafanya kama alivyo agiza, kalilazimisha gari kupita kwenye uwazi wa
gari lililopo barabani, chakushukuru Mungu likapita, ikawa kazi ni
kwangu kuhakikisha ninasonga mbele.
Japo
kuna risasi kadhaa zilipigwa kwenye gari letu, ila hapakuwa na iliyo
adhiri matairi zaidi ya kuvunja vioo vya pembeni. Kwa mwendo kasi wa
gari hili, ulinifanya niwe makini kwa kila kona ninayo kunja barabarani.
"Ohhh Mungu wangu! tunafwatwa nyuma"
Kaka
yake Casey alizumgumza huku, akichungulia kwenye kioo cha nyuma kilicho
jaa matundu ya risasi. Sikutaka hata kutazama nyuma kuzihofia kona za
papo kwa papo, huku nyengine zikiwa ni kali sana.
"Wapo wangapi?"
”Pikipiki mbili na gari ndogo tatu"
"Muheshimiwa unaweza kutumia, silaha?"
"Eheee?"
Balozi
alibabaika kwenye kunijibu swali nililo muuliza. Sikuwa na jinsi zaidi
ya kuongeza mwendo kasi wa gari, ninalo liendesha. Tukafanikiwa kuingia
kwenye barabara iliyo nyooka, hapa ndipo nikapata wakati mzuri wa
kuwatazama wanao tufwata kupitia kioo changu cha pembeni.
"Hawa vijana ni kina nani?"
"Siwajui muheshimiwa"
Waendesha pikipiki, nikawaona wakilikaribia gari letu, kutokana na mwendo wao mkali. Nikapunguza mwendo taratibu
"Mbona unapunguza mwendo?"
Balozi aliniuliza huku akitetemeka, hata sauti yake haikutoka vizuri
"Najua nini, nafanya"
Nilimjibu
kwa kujiamini, huku macho yangu yote yakiwa kwenye kioo cha pembeni
nikiwatazama jinsi majambazi hao wakija kwa kasi, Nikakanyaga breki kwa
nguvu zangu zote, huku nikilizungusha gari kwa mtindo wa duara, jambo
lililo wafanya waendesha pikipiki hawa kulivaa gari letu, na kila mmoja
akarushwa vibaya na kuangukia upande wake wa barabara.
Kutokana
na uhodari wa gari hili, halikuweza kuyumba wala kuzima. Ila kilicho,
niogopesha ni jinsi gari ilivyo geuka na kutazama tulipo tokea ambapo
kuna gari mbili ndogo zinatufwata, na mbaya zaidi zipo karibu kutufikia.
Ikanilazimu kulirudisha gari kinyuma nyuma ili nipate, japo nafà si la kuligeuza, nitakavyo jua mimi.
Nikiwa
ninaendelea kurudi nyuma kwa mwendo wa kasi japo si sana nikaliona,
gari tulili liacha sehemu tuliyo vamiwa likaja kwa kasi nyuma ya gari
hizi mbili ndogo, zinazo tukimbiza.
"Ohhh wamelichukua hata hili"
Nilizungumza
huku nikijitahidi kupata nafasi ya kuligeuza gari hili, ila kwa bahati
mbaya upande nilio kuawepo mimi kuna gari kubwa la mizigo, likija kaa
kasi huku dereva wake akijitahidi kunipigia honi, nimpishe upande wake,
lasivyo anatugonga.
Nikalirudisha
kwa haraka upande wa kushoto ambapo ndipo ninapo stahili kupita, dereva
wa gari ambaye alikuwa upande mmoja na mimi, nikastukia akigongana uso
kwa uso na gari hilo la mizigo, tukio lililo mstusha mwenzake ambaye
nipo naye upande mmoja. Akajikuta akifunga breki, bila hata ya kutegemea
gari lililo kuwa nyuma yake, likamvaa na yote kwa pamoja yakatoka nje
ya baranara huku yakizunguka, na kutimua vumbi jingi, huku vyuma vya
magari yao vikisagika ikiashiria kwamba yana gongonga kwenye mawe
makubwa yaliyopo pembezoni mwa barabara.
Nikakanyaga breki, kusimamisha gari. Nikashusha pumzi nyingi, huku nikilitazama vumbi likielea angani.
"Kila mmoja yupo salama?"
"Ndio"
"Ndio"
"Ndio"
Kila
mmoja alijibu kwa wakati wake, nikatazama upande wa mbele tulipo tokea,
sikuona gari lolote likija, saa iliyopo pembeni yangu inaonyesha ni saa
kumi na moja alfajiri. Taratibu nikaliemdesha gari hadi, hadi zilipo
gari hizi mbili.
"Bakini ndani ya gari"
Nilizungumza
kwa kujiamini, nikaichukua bastola yangu niliyo kuwa nimeiweka pembeni
mwa siti, niliyo kalia. Nikafungua mlango wa gari na kushuka, huku
nikiwa makini sana na tayari kwaa lolote litakalo jitokeza mbele yangu.
Nikafika
ilipo gari ndogo, na kumkuta dereva akiwa amelalia mskani wake, ulio
mbana maeneo ya kifuani. Nikamchunguza na kugundua bado anahema kwa
shida, huku damu zikimtoka puani na mdomoni.
"Ni...ss..aid..ie"
Aliniomba msaada huku akinitaza kwa macho yaliyo mtoka. Mithili ya mtu aliye kwabwa na kitu kizito kooni.
"Nani aliye kutuma?"
"Nisa....i..die...ni.tamtaj....a"
Nikaikoki
bastola yangu kuziandaa risasi kutoka, kidole changu kimoja kikianza
kuivuta traiga, taratibu, huku nikiwa nimemuelekezea bastola kichwani
kwake.
"Nakuuliza kwa mara ya mwisho. Ninani aliye watuma?"
Jamaa alipo litazama shimo dogo, la kutolea risaai la bastola, akayarudisha macho yake usoni mwangu.
"J....oh..n"
Jamaa,
alinijibu kwa shida kubwa sana, na kichwa chake kikalegea, akiashiria
ameiaga dunia. Kwa hasira nikamsindikiza huko aendapo kwa risasi moja
iliyo tua kichwani mwake.
Nikasikia sauti ya mtu akikohoa kwenye gari, tulilo liacha sehemu ya tukio.
Nikaanza
kutembea kwa umakini, huku bastola yangu nikiishikilia vizuri,
nikamkuta yule amlinzi tuliye muacha eneo la tukio, akiwa amekaa chini
huku ameliegemea gari, mkono wake mmja akiwa amejishika tumboni mwake,
kunapo vuja damu nyingi, sura yake ikiwa imechanika chanika kwa kuchwana
na vipande vya vioo vya gari.
Alipo niona akatabasamu kidogo, huku akikohoa na kumwaga madonge ya damu mdomoni mwake.
"Muheshimiwa yu..po salama?"
"Ndio yupo salama"
Nilimjibu, huku nami nilipiga goti chini, nikijaribu kumtazama ni nini kilicho mpata sehemu ya tumbo.
"Asante kwa msaada wako, wewe ni mwanaume shujaa."
Alizungumza huku, akitabasamu na kukohoa juu.
"Damu nyingi, imenitoka. Suwezi pona"
Alizumgumza maneno haya baada ya kujaribu, kumpa huduma ya kwanza. Akanishika mkono wangu wa kulia
"Toa pochi yangu, kwenye......mfuko wa nyuma"
Nikaitoa pochi, akaniomba niifungue na kitu cha kwanza kukiona na kitambulisho chake chenye jina la George Jr.
"Fungua, upande wa pili"
Nikafungua
na kukuta, picha mbili moja akiwa mdogo na nyingine akiwa amesimama na
msichana aliye nifanya niitumbulie mimacho picha hiyo.
"Chukua hii chane, naomba umtafute dada yangu anaitwa Victoria, umkabidhi hii cheni."
George
Jr. Alinikabishi cheni aliyokua ameivaa shingoni mwake. Huku taratibu,
akianza kuyapepesa macho yake. Akanyayua mkono wake taratibu, huku
alitetemeka, akanipigia saluti na kukata roho.
Taratibu
machozi yakaanza kunimwagika, nikayafunika macho yake kwa kupitia
kiganja cha mkono wangu wa kulia. Nikageuka nyuma, nikamkuta baloIi
akiwa amesimama na watoto wake, huku Casey machozi yakimwagika.
Nikanyanyuka taratibu, na kwenda lilipo gari na kuingia. Nikaitazama
picha ya George aliyopiga na Victoria. Nikajikuta donge la hasira
likinibana kifuani mwangu.
Nikasikia milio ya helcoptar, nikawasha gari kaa haraka, ila Casey akanikimbilia
"Eddy tupo, salama hao ni wanajeshi wa Marekani, wanakuja"
Casey
alizumgumza huku, akichungulia dirishani. Helcoptar mbili zikashuka
hewani na kusimama, katikati ya barabara. Wakashuka wanajeshi wengi,
wenye bunduki mikononi. Balozi akaanza kuzumgumza nao, huku kaka yame
Casey, akipewa nguo ajisitiri mwili wake.
Wakatuchukua, sote wanme na kuondoka huku, Helcoptar nyingine ikibaki, na wanajeshi kadhaa wakiupima pima mwili wa George Jr.
Tukafika
makao, makuu ya jeshi la Marekani lililopo hapa, nchini Afrika kusini.
Tukapewa huduma za kwaza ikkwemo vifungua kinywa, kwani hatukupa chakula
kwakipindi kirefu. Matumbo yalipo kaa sawa, nikatambulishwa mm wa
baadhi ya wakuu wa jeshi. Wengi wao wakanisifu kwa kazi nzuri na pevu,
niliyo ifanya.
Tukapelekwa
kwenye moja ya hoteli kubwa, tukiwa chini ya uangalizi mkali wa jeshi.
Balozi Brayan Daniel, hakusita kunitambulisha kwa kila rafiki yake
ambaye, huku akinimwagia sifa kedekede.
Tukakaa hotelini, kwa siku nne, ambapo Balozi Brayan Daniel akaendelea na majukumu yake ya kazi, huku akiniomba niwaliende watoto wake kwa kipkndi kifupi kabla hatujaenda Marekani, kuhudhuria mazishi ya askari walio kumbwa na tukio la uvamizi.
Tukakaa hotelini, kwa siku nne, ambapo Balozi Brayan Daniel akaendelea na majukumu yake ya kazi, huku akiniomba niwaliende watoto wake kwa kipkndi kifupi kabla hatujaenda Marekani, kuhudhuria mazishi ya askari walio kumbwa na tukio la uvamizi.
Mida ya saa sita mchana, ikafika gari katika hoteli tuliyopo, huku
akija muwakilishi wa balozi, akituomba twende ofisini kwake, tukakutane
na baadhi ya viongozi wa hapa nchini Afrika kusini. Tukajiandaa, kila
mmoja akavalia mavazi tuliyo numuliwa siku kadhaa, tumaingia ndani ya
gari, huku mimi nikiwa makini kuhakilisha Casey na kaka yake wapo salama
salmini.
Tukafika
kwenye ofisi za ubalozi wa Marekani, tukapokelewa vizuri na kupelekwa
kwenye ofisi za balozi, ambapo tulimkuta yupo na watu baadhi, wanao
onyesha kua ni viongozi. Tukakaa kwenye viti vilivyo andaliwa kwa ajili
yetu.
"Jamani mutatiwia radhi kidogo kwa kuchelewa kufika kwenye halfa hii"
Sauti
ya John, ilisikika kutokea mlangoni, akiingia akiwa ameongozana na
Victoria, mpenzi wake.Pasipo kutazama waliopo ndani ya ofisi John na
Victoria, wakakaa kwenye viti vyao na kukamilisha idadi ya watu ishirini
na tano, tuliomo humu ndani, Nikaivua miwani yangu nyeusi niliyo ivaa,
nikamuona John, akilegeza mdomo wake kwa kunishangaa, huku naye Victoria
akiinamisha kichwa chini kwa aibu, wasiju nini cha kufanya. Huku
nikiwakazia macho yaliyo jaa hasira kali kama Simba.
SORRY MADAM 78
Ukimya wa sekunde kadhaa, ukakatiza huku macho yangu nikiyahamisha
kutoka kwa John, kwenda kwa Victoria. Swali la kwanza kujiuliza ni
kuhusiana na John anahusika kivipo kwenye huu mkutano, hiyo moja mbili
anamahusiano gani na balozi wa Marekani bwana Brayan Daniel.
"Nashukuru kwa kufika kwenu, kwa maana nyinyi ni wachache kati ya wengi nilio tamani wafike hapa."
Balozi B.Daniel alizungumza huku akiwa amesimama.
"Lengo langu la kuwaita hapa, ndugu zangu, ni kumtambulisha shujaa wangu, aliye jitolea kuyaokoa maisha yangu na familia yangu.”
"Huyu ninaye mzungumzia hapa si mwengine bali ni Eddy Godwin."
Balozi alininyoonyea mkono, watu wote wakapigaiwemo Jonh na Victoria.
"Japo
nimepatwa na pigo, lakuwapoteza vijana wangu, kumi katika shambulio
lile, Ila kusema ukweli ni jbo la kumsukuru sana Mungu, kwa kijana Eddy
kujitokeza na kuweza kuitetea nafsi yangu. Pasipo kujali yeye ni nani,
ila ni kitu kikubwa sana kufanywa na mtu wa kawaida."
Kila
muda ulivyo zidi kwenda, ndivyo nilivyo jikuta nikizidi kupandwa na
hasira kali, hata yañayo zungumzwa ndanivya hichi chumba sikuweza
kuyasikia hata kdogo.
Matukio
baadhi aliyo yafanya John, yakanza kunisumbua akilini mwangu, taratibu
nikajikuta nikitokwa na machozi ya uchungu sana. Casey akaniangalia kwa
muda, kwa haraka akanifwata nilipo kaa
"Eddy una tatizo gani?"
Watu
wote wakabaki wakitutizama mimi na Casey. Mapigo ya moyo hayakusita
kunienda mbio hadi nikaanza kujihisi kizungu zungu. Nikaanza
kujishangaa, baada ya kuona jinsi matone ya damu yakianza kunitoka puani
"Muiteni dokta"
Nikajaribu kunyanyuka, ila kizunguzungu kikali, kikaniyumbisha kabla sijaenda chini, Casey aksniwahi, akisaidiana na kaka yake.
Macho
yakaanza kujaa ukungu mwingi ulio nifanya niwaine watu wawili wawili.
Nikamuona John, akitabasamu. Huku akinyanyuka kwenye kiti alicho
kikalia.
"Tupeni nafasi, tumuhudumie."
Sauti za madkari, nilizisikia kama sauti ya kengele zinazo gongwa.
"Nakufa"
Nilizungumza kwa sauti ya chini, sana, huku nikizidi kujihisi vibaya.
***
Nikastuka gafla, kabla sijanyanyuka, nikastukia nikirudishwa chini, kitandani na dada mmoja aliye valia mavazi meupe.
"Tulia kaka yangu."
"Nipo wapi?"
"Hospitali"
"Kwañi ninaumwa?"
"Ndio"
Nikatizama
pembeni, nikaona dripu la maji likishusha kiwango cha maji kwenye,
mishipa ya mkono wangu wa kushoto, kupitia mrija wake mwembamba ulio
unganishwa na sindano yake na kuchomwa kwenye sehemu ya kukunjia mkono.
"Unajisikiaje?"
"Vizuri"
"Basi tulia, dripu hili likiisha, unaweza kuruhusiwa"
"Litachukua muda gani?"
"Mmmmm masaa kama mawili hivi, kwani ndio nimekuwekea muda huu"
Nikajichnguza
mwili wangu, na kujikuta nikiwa na mavazi niliyo yavaa, mchana. Saa ya
ukutani inaonyesha ni saa moja jioni. Nesi akatoka ndani ya chumba,
dakika jadhaa akaingia Casey na kaka yake.
"Unaendeleaje Eddy?" Çasey alizungunza.
"Nipo poa"
"Pole kaka Eddy"
"Asante Bruño"
"Baba yupo, na daktari, wanazungumza kuhusiana na tatizo lako"
"Daktari amesema nina tatizo gani?"
"Amesema kwamba, una...."
Bruno akamziba Casey mdomo asizungumze, anacho taka kukisema kwa muda huu.
"Hapana kaka Eddy, huna tatizo mwaya."
Nikatabasamu huku nikimtazama, Bruno na Casey, nikatambua kwamba kuna tatizo tu, ila nahisi wameambiwa wasizungumze.
"Mbona umemziba mwenzako mdomo?"
"Hapana, anapenda kuongea ongea sana huyu."
"Si uniaçhe, nizungumze.."
Bruno akamziba tena mdomo, Casey na kujikuta wakianza kugombaba, kama jawaida yao.
"Heii jamani acheni kugombana”
Casey
akatoka chumbani kwa hasira na kuubamiza mlango. Bruno akaachia msunyo
mkali na kukaa katika sofa lililomo ndani ya hichi chumba.
"Bruno hivi, mbona unapenda kugombana na Casey?"
"Ahaa domo lake, lipo wazi sana"
"Sawa, hivi yule jamaa aliye ingia, baada ya sisi kufika una mfahamu?"
"Yule ndio nina mfahamu, ni rafiki mkubwa sana wa baba"
"Tangu lini?"
"Kivipi yani?"
"Namaanisha wamejuana lini?"
"Tangu mwaka jana, tunakuja hapa Afrika kusini, tukitokea Marekani."
"Ahaaa"
"Tena yule John, ana roho nzuri sana. Haswa yule mke wake."
"Chanzo
cha baba, kua rafiki na yule John. Walitoa Hotel yao sisi kuishi tangu
tunakuja hadi tulipo pewa nyumba, tuliyo andaliwa. Kwani balozi aliye
pita kabla ya baba, alifariki kwa ajali ya ndege."
"Kwa
hiyo vitu vyake havikuamishwa, kwenye ñyumba tunayo ishi, sasa hivi.
Ikatulazimu kuishi Hotelini, John akajitolea hoteli yake tuishi bure kwa
kipindi chote"
"Ahaaa"
"Hata ile Hotel tunayo kaa sasa hivi ni ya John na mke wake"
"Kweli?"
"Ndio"
"Kumbe nimatajiri dana ehee?"
"Ndio nimatajiri sana, ila nasikia kwamba utajiri wao ni wakuridhi, kutoka kwa baba yake Victoria, ambaye kwa sasa ni marehemu"
Nikastuka,
huku nikimtazama Bruno, akili yangu ikaenda moja kwa moja katika tukio
walilo lifanya John na Victoria kutaka kumuua baba yangu.
"Huyo baba yake, Victoria anaitwa nani?"
"Kwakeli simfahamu, ila nilisikia kwamba baba yake alijinyonga, chumbani kwake. Inasadikika alikuwa na ugonjwa wa kichaa"
Nikahisi
mwili wangu, ukisisimka, kwani John amechukua, kila kitu kwenye maisha
yangu. Kuanzia mali za baba yangu. Hadi familia yañgu.
Muda
wa kuruhusiwa, ukawadia. Daktari akaniomba azungumze na mimi. Tukaingia
ofisini kwake na kukaa kwenye viti vilivyomo humu ndani.
"Tumekufanyia
uchunguzi wa kina, tukakukuta na matatizo mawili kwenye mwili wako.
Endapo hayata fanyiwa uharaja wa matibabu, unaweza kupelekea kifo chako.
Bwana Eddy."
Daktari alizungumza huku akinitazama machoni mwangu. Wasiwasi haukuacha kunitawala usoni nwangu.
"Ninaumwa na nini Daktari?"
"Tatizo
la kwanza, ni hasira iliyo pitiliza kiwango. Ambayo ikikupanda sana,
inapelekea mfumo wako wa mapigo ya moyo kukuenda kasi sana. Moyo
unapeleka kasi damu kwenye mishipa mbali mbali mwilini mwako. Na ndipo
kuna baadhi ya damu, zinatoka puani mwako."
"Ukishindwa kujizuia hasira yako, itapelekea mishipa ya damu kupasuka, hapo utakua ni mwisho wako wa kuishi duniani"
"Tatizo la pili, tumegundua kwamba, unayemelewa na ungonjwa wa Saratani, ya damu."
Nikahisi mwili mzima ukifa ganzi, kwani sikifikiria kama nitaumwa nà ugonjwa wa Canser, tena ya damu
"Ila
usiwe na wasi, nimezungumza na muheshimiwa, utakwenda kufanyiwa
matibabu Marekani. Na saratani itakwenda kupona, kwani ndio ipo kwenye
hatua za mwanzoni mwanzoni."
Daktari akanikabidhi dawa, za kunywa pale nitakapo jihisi vibaya.
"Siwezi kufa hadi nirudishe, kila kitu alicho kichukua John kutoka mikononi mwangu.”
Nilizungumza kimoyo moyo huku, nikitoka chumba cha daktari, nikajumuika na balozi, pamoja na wanae kurudi hotelini.
***
Siku
mbili, zikapita na hali yangu ikazidi kuimarika. Kila asubuhi nikawa na
jukumu la kufanya mazoezi, ili kuuimarisha mwili wangu. Nikiwa
nimevalia nguo za mazoezi, raba pamoja na earphone, nikibrudika kwa
mziki, kupitia Ipad aliyo nipa Casey, jana usiku. Nikaendelea kukimbia
barabanani, huku saa yangu ya mkononi, ikinionyesha ni saa kumi na moja
alfajiri.
Katika
barabara ninayo kumbia, hakuna wa watu wengi, zaidi ya mtu mmoja mmoja,
ninao kutana nao wakifanya mazoezi kama mimi ya kukimbia.
Nikamkuta
dada mmoja aliye vali, suti ya kijivu, Akionekana kuchanganyikiwa,
kwani gari lake analo liendesha, limepata pacha tairi la mbele.
"Samahani kaka"
Aliniita baada ya kumpita kidogo, nikavua earphone zangu, na kugeuka kumsikiliza ahahitaji kuzungumza na mimi kitu gani.
"Ndio"
"Nakuomba, unisaidie kubadilisha tairi la hili gari."
Nikamtazama juu hadi chini, pasipo kumjibu chochote. Nilipo ridhika na udadisi wangu, nikamsogelea.
"Kwani ilikuaje?"
"Nimekuta tu tairi, likiisha upepo"
"Toa hilo jengine"
Akazunguka
nyuma ya gari lake kwa haraka, akatoa tairi pamoja navifaa vingine vya
kusaidia kubadilishia tairi la gari. Nikaanza kazi ya kulifungua tairi
lenye pancha, huku yeye akiwa na kazi ya kunibadilisha kila spana
nitakayo muomba anipatie.
Haikuchukua muda sana, nikamaliza kumfungia tairi lake jipya.
"Asante sana"
"Usijali"
Akafungua
mlango wa upande wa dereva, na kutafuta kitu. Kutokana sikuhitaji
kulipwa, nikaanza kuondoka babla sijapiga hatua hata sita nikasikia
akiniita.
"Kaka subiri uchukue zawadi yako"
Nikageuka, sikuamini macho yangu kwani, nikakutana na bastola aliyo ishika huyu dada, akinielekezea mimi
"Tulia hivyo hivyo, ukijaribu kupiga hatua nitakufumua ubongo wako."
Alizungumza huku akiwa ameishika, bastola yake kwa mkono mmoja, huku mkono mwingine akiwa na simu.
"Ninaye hapa"
Alizungumza
kupitia, simu yake. Wala sikujua à nazungumza na nani. Mbaya zaidi
siwezi fanya chochote kutokana hii barabara imenyooka sana, na haina
sehemu ya kujificha. Gari nne nyeusi, zenye muundo wa gari kama zinazo
bebea pesa za mabenki, zikafunga breki katika eneo tulilopo. Wakashuka
watu walio valia ñguo nyeusi, makofia meusi yaliyo waficha sura zao, na
kubakishs macho yao tu. Kila mmoja mkononi mwake ameshika bundiki, na
wote wakanizungu huku wakinitazama kwa umakini.
==> ITAENDELEA
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia adam64.com
0 Comments
on