Watumiaji
wa usafiri wa mabasi ya umma ya UDART sasa wataweza kuongeza pesa
katika kadi zao kwa kupitia M-PESA, Vodacom inakuwa ndiyo kampuni ya
kwanza ya simu kuwapatia wateja wake uwezo wa kuongeza pesa katika kadi
za kusafiria katika mabasi haya ya UDART.
Kadi zinazotumika katika usafiri huo wa UDA
UDART
walitangaza kusitisha tiketi za karatasi na hivyo kuhimiza watumiaji wa
usafiri huu mpya kununua kadi ambazo ndizo pekee zitatumika, hatua hii
iliacha changamoto moja tu kwamba kuongeza pesa katika kadi ama kujua
kiasi cha pesa kilichobaki katika kadi yako ilikubidi kupanga foleni
katika kituo kitu ambacho hakikuwa kizuri sana kwa watumiaji.
Vodacom
wameliona hilo na kuamua kuleta huduma ya M-PESA kwa wateja wake ambao
wanatumia UDART, kuanzia sasa wateja wa Vodacom hawatahitaji kukaa
foleni kusubiri kuongeza salio katika kadi zao UDA bali wataweza kufanya
hivyo kwa kutumia M-PESA.
Kuongeza salio katika kadi yako ya UDA fuata hatua zifuatazo:-
Piga *150*00# chagua LIPA KWA M-PESA,
Chagua DART,
Weka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba ya kadi yako ya DART,
Weka KIASI (Mfano 2000, 5000, 10000 n.k),
Weka PIN yako ya M-Pesa,
Bonyeza 1 kukamilisha muamala.
Utapokea ujumbe mfupi kuthibitsha muamala wako.
0 Comments
on